Papa:Mkate wa Ekaristi ni shukrani,kumbukumbu na uwepo halisi!

Shukrani,kumbukumbu na uwepo ni maneno matatu ambayo Baba Mtakatifu amefafanua katika mahubiri wakati wa Misa Takatifu iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano,katika Siku Kuu ya Mwili na damu ya Yesu ambapoilihitimishwa kwa maandamano na baraka takatifu mbele ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Sherehe ya Mwili na Damu ya Yesu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane huko Laterano, saa 11.00 jioni, tarehe 2 Juni 2024. Baada ya masomo yote, Papa Francisko ameanza mahubiri yake akisema: “Alitwaa mkate na akabariki(Mk 14,22). Ni ishara ambayo katika Injili ya Mtakatifu Marko inafungua simulizi ya kuanzishwa kwa Ekaristi. Na tunaweza kuanza kutoka katika ishara hii ya Yesu  ya kubariki mkate kutafakari juu ya sehemu tatu za Fumbo tunaloadhimisha: shukrani, kumbukumbu na uwepo.

Papa akihubiri katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano
Papa akihubiri katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano

Kwanza ni kushukuru. Baba Mtakatifu ameeleza kuwa: Neno “Ekaristi” kiukweli linamaanisha “asante”: kumshukuru” Mungu kwa zawadi zake, na kwa maana hii ishara ya mkate ni muhimu. Ni chakula cha kila siku, ambacho kwacho tunapeleka kwenye Altare kila kitu tulicho nacho na kuwa nacho: maisha, kazi, mafanikio, na hata kushindwa, kama inavyooneshwa na desturi nzuri ya tamaduni fulani za kuokota na kubusu mkate unapoanguka ardhini ili  kukumbuka kuwa ni wa thamani sana na siyo wa kutupwa, hata baada ya kuanguka. Ekaristi, kwa hiyio inatufundisha kubariki, kukaribisha na kubusu, daima, katika shukrani, zawadi za Mungu,na hii si tu katika adhimisho: pia hata katika maisha.

Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, Laterano
Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, Laterano

Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema kwa mfano kwa kutopoteza vitu na talanta ambazo Bwana ametupatia. Lakini pia kwa kusamehe na kuwainua wale waliokosea na kuanguka kwa sababu ya udhaifu au upotovu: kwamba kila kitu ni zawadi na hakuna kinachoweza kupotea, kwa sababu hakuna mtu anayeweza kubaki chini na kila mtu lazima apate fursa ya kuamka na kuendelea na safari. Na tunaweza pia kufanya hivyo katika maisha ya kila siku,” tukifanya kazi yetu kwa upendo, kwa usahihi, kwa uangalifu, kwa usahihi, kama zawadi na utume. Na kila wakati kuwasaidia wale ambao wameanguka: mara moja tu katika maisha yetu  tunaweza kumtazama mtu kutoka chini hadi juu wakati tunawasadia kuinuka. Na huu ndio utume wetu” wa kushukuru. Na tunaweza kuongeza mambo mengi ya kushukuru. Ni mitazamo muhimu wa “Ekaristi,” kwa sababu inatufundisha kufahamu thamani ya kile tunachofanya, na kile tunachotoa.

Waamini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, Laterano
Waamini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, Laterano

Kama kwanza ilikuwa ni kushukuru na pili: “Kubariki Mkate  ina maana ya kukumbuka. Kuhusu nini? Kwa Waisraeli wa kale lilikuwa ni jambo la kukumbuka kukombolewa kutoka utumwani Misri na mwanzo wa kutoka kuelekea nchi ya ahadi. Kwetu sisi ni kufufuka, Pasaka ya Kristo, Mateso yake na Ufufuko, ambayo kwayo alituweka huru kutoka katika dhambi na kifo. “Kukumbuka maisha yetu, kukumbuka mafanikio yetu, kukumbuka makosa yetu, kukumbuka ule mkono wa Bwana ulionyoshwa ambao hutusaidia kila mara kutuinua; na kukumbuka uwepo wa Bwana maishani mwetu.”

Wakati wa Misa
Wakati wa Misa

Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa: “Wapo wanaosema kwamba wanaojifikiria wao tu wako huru, wanaofurahia maisha na wale ambao kwa kutojali na pengine kwa majivuno wanafanya kila watakalo licha ya wengine. Lakini huu sio uhuru: huu ni utumwa uliofichwa, utumwa unaotufanya kuwa watumwa zaidi.” Uhuru haupatikani katika salama za wale wanaojikusanyia wenyewe, wala kwenye sofa za wale wanaojiingiza kwa uvivu na kujitenga na ubinafsi:uhuru unapatikana katika ukumbi ambamo, bila sababu nyingine yoyote isipokuwa upendo, tunainama mbele ya ndugu zetu ili kuwatolea huduma yetu, maisha yetu na  kama kuokolewa.

Altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane , Laterano
Altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane , Laterano

Hatimaye, mkate wa Ekaristi ni uwepo halisi. Na kwa hili anazungumza nasi juu ya Mungu ambaye hayuko mbali, asiye na wivu, lakini wa karibu na mshikamano na mwanadamu; ambaye hatutupi, bali anatutafuta, anatungoja na kutusindikiza, daima, hata kujiweka mikononi mwetu, bila kujitetea. Na kuwapo kwake pia hutualika kuwa karibu na ndugu zetu ambapo upendo unatuita. Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo amesisitiza kwamba, kuna hitaji kiasi gani katika ulimwengu wetu kwa mkate huu, kwa harufu yake na manukato yake, harufu nzuri inayoonja shukrani, inayoonja uhuru, na ladha ya ukaribu!

Uzuri wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, huko Laterano
Uzuri wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, huko Laterano

Kila siku tunauona katika mitaa mingi sana, labda mara moja ukinukia mikate ilioyokwa, ambayo imebaki milundo ya vifusi kutokana na vita, ubinafsi na kutojali! Ni hitaji la haraka kurudisha duniani harufu nzuri na safi ya mkate wa upendo, kuendelea kuwa na matumaini na kujenga upya bila kuchoka hata kidogo kile ambacho chuki huharibu.

Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, Laterano
Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, Laterano

Kwa njia hiyo “Hii pia ndiyo maana ya ishara ambayo tutafanya karibuni, pamoja na Maandamano ya Ekaristi: kuanzia Altareni, tutampeleka Bwana kati ya nyumba za jiji letu. Hatufanyi hivyo ili kujionesha, wala kudhihirisha imani yetu, bali kuwaalika kila mtu kushiriki, katika Mkate wa Ekaristi, katika maisha mapya ambayo Yesu ametupatia: tunafanya maandamano kwa roho hii. Asante.” Papa alihitimisha.

Wakati wa kuanza maandamano
Wakati wa kuanza maandamano

Mara baada ya misa Takatifu ilifuata maandamamo kutoka katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane huko Laterano kupitia njia ya Merlulana hadi Mtakatifu Maria Mkuu ambapo Baba Mtakatifu alikuwa aitimishe kwa baraka, kama ilivyokuwa imepangwa katika ratiba.

Mwili na damu ya Yesu
Mwili na damu ya Yesu
Maandamano
Maandamano
Mahubiri ya Papa 2 Juni 2024 katika siku kuu ya Mwili na damu ya Yesu
02 June 2024, 18:33