2024.06.20 Washiriki wa Mkutano ulioandaliwa na Specola Vatican. 2024.06.20 Washiriki wa Mkutano ulioandaliwa na Specola Vatican.  (Vatican Media)

Papa:sayansi iwe kwa huduma ya mwanadamu na si kwa uharibifu wake

Imani na sayansi vinaweza kuunganishwa katika upendo, ikiwa sayansi inawekwa kwa huduma ya wanaume na wanawake wa wakati wetu, na sio kupotoshwa kwa madhara yao au hata uharibifu wao,ni maneno ya Papa,Juni 20 kwa washiriki wa Mkutano uliohamasishwa na Kundi la kisayansi la Vatican.Mada:George Lemaître:“Mashimo meusi,mawimbi ya mvuto na umoja wa nafasi ya anga.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Alhamisi tarehe 20 Juni 2024, Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na Washiriki wa Mkutanano wa II wa Specola Vatican, katika kufanya kumbu kumbu ya George Lemaître: Mashimo meusi, mawimbi ya mvuto na umoja wa muda wa anga. Akianza hotuba yake kwa wanasayansi hao, ametoa salamu kuanzia na Kardinali Kevin Farrell na Katibu wa Mji wa Vatican Sr Raffaella na  kwamba kwa sasa, wanawake wanaanza kutawala ndani humo…, na amewafanya wacheke... Kwa njia hiyo amewa karibisha kwa moyo mkunjuu na kuwashukuru kwa ziara yao. Kwa namna yake amefurahishwa na Ndugu

Guy Consolmagno na wajumbe wengine wa Jumuiya ya Kisayansi ya Specola Vatican kwa kuanzisha mpango huo. Papa Francisko amebainisha jinsi walivyoksanyika huko Castel Gandolfo kwa ajili ya mkutano unaongozwa kwa heshima ya kumbukizi ya Monsinyo George Lemaître, miaka saba baada ya toleo lililopita. Wakati huo huo, thamani ya kisayansi ya kuhani wa Ubelgiji na mtaalamu wa unajimu  imetambuliwa zaidi na Umoja wa Kimataifa wa Elimu ya anga ambao umeamua kuwa sheria inayojulikana ya Hubble inapaswa kuitwa vizuri zaidi sheria ya Hubble-Lemaître. Baba Mtakatifu amesema kuwa siku hizi wao  wanajadili maswali ya hivi karibuni  yaliyoletwa na utafiti wa kisayansi katika kosmolojia,  matokeo tofauti yaliyopatikana katika kipimo cha Hubble mara kwa mara, asili ya fumbo ya umoja wa ulimwengu (kutoka mlipuko mkubwa hadi shimo nyeusi) na mada ya sasa ya mawimbi ya mvuto.

Hotuba ya Papa Specola Vatican

Kanisa liko makini na utafiti huo na kuukuza, kwa sababu unashtua usikivu na akili ya wanaume na wanawake wa wakati wetu. Mwanzo wa ulimwengu, mageuzi yake ya mwisho, muundo wa kina wa nafasi na wakati ambapo wanadamu wanakabiliwa na utafutaji wa haraka wa maana, katika mazingira makubwa ambapo wana hatari ya kupotea. “Hili inatufanya tugundue tena umuhimu wa maneno haya ya mtunga-zaburi: “Nizionapo mbingu zako, kazi ya vidole vyako, / mwezi na nyota ulizoziweka, / mwanadamu ni kitu gani hata umkumbuke,  mwana wa binadamu? kwanini unamjali? Hakika umemfanya mdogo kidogo kuliko mungu, umemvika taji ya utukufu na heshima” (Zab 8:4-7).  Kwa hiyo ni wazi kwamba mada hizi zina umuhimu fulani kwa taalimungu, falsafa, sayansi na pia kwa maisha ya kiroho. George Lemaître alikuwa Padre na mwanasayansi wa mfano. Safari yake ya kibinadamu na ya kiroho inawakilisha kielelezo cha maisha ambacho sote tunaweza kujifunza.

Papa akutana na washiriki wa Mkutano wa kisayansi
Papa akutana na washiriki wa Mkutano wa kisayansi

Ili kutekeleza matakwa ya baba yake alisomea uhandisi; aliandikishwa katika Vita vya Kwanza vya Kidunia na akapata mambo ya kutisha.” Akiwa mtu mzima alifuata wito wake wa kipadre na kisayansi. Hapo awali yeye ni - kama wasemavyo – “mpatanishi,” yaani, anaamini kwamba kweli za kisayansi zimewekwa katika Maandiko Matakatifu kwa namna iliyofunikwa. Uzoefu wake wa kibinadamu na ufafanuzi unaofuata wa kiroho basi hulimpeleka kuelewa kwamba sayansi na imani hufuata njia mbili tofauti na zinazofanana, ambazo hakuna mgongano. Hakika, njia hizi zinaweza kuoanisha kila mmoja, kwa sababu sayansi na imani, kwa mwamini, zina msingi sawa(Mati) katika Ukweli kamili wa Mungu. Safari yake ya imani ilimpeleka kwenye ufahamu kwamba uumbaji na mlipuko mkubwa ni mambo mawili tofauti, na kwamba Mungu anayemwamini hawezi kuwa kitu kinachoainishwa kwa urahisi na akili ya kibinadamu, lakini ni “Mungu aliyefichwa,” ambaye daima anabaki katika mwelekeo wa siri, isiyoeleweka kabisa.

Ni Matumaini ya Papa wataendelea kujadili masuala wanayoyajadili kwa moyo wa uaminifu na unyenyekevu. Uhuru na ukosefu wa hali, wanaoupata uzoefu  katika mkutano huo, unaweza kuwasaidia kuendelea katika nyanja zao kuelekea Ukweli, ambao kwa hakika ni dhihirisho la Upendo wa Mungu. Imani na sayansi vinaweza kuunganishwa katika upendo, ikiwa sayansi inawekwa kwa huduma ya wanaume na wanawake wa wakati wetu, na sio kupotoshwa kwa madhara yao au hata uharibifu wao. Papa Francisko amewahimiza waingie kwenye viunga vya maarifa ya kibinadamu: ni hapo kwamba wanaweza kupata uzoefu wa Mungu wa Upendo, ambaye hutosheleza na kukidhi kiu ya mioyo yetu.  Amewabariki sana wote  na kazi za upendo. Na nakuwaomba wamuombee tafadhali.

Je alikuwa nani Lemaître

Georges Henri Joseph Édouard Lemaître alizaliwa Charleroi, Ubelgiji, mnamo 17 Julai 1894 , na kifo chake tarehe 20 Juni 1966, akiwa ni mtoto mkubwa kati ya watoto wanne. Baba yake Joseph Lemaître alikuwa mfumaji tajiri wa viwandani na mama yake alikuwa Marguerite, née Lannoy. Baada ya elimu ya kiutamaduni katika shule ya Sekondari ya Kijesuit, katika Chuo cha Moyo Mtakatifu huko Charleroi, Ubelgiji, alianza kusomea uhandisi wa ujenzi katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Louvain akiwa na umri wa miaka 17.  Mnamo 1914, alikatiza masomo yake na kutumika kama afisa wa silaha katika jeshi la Ubelgiji kwa muda wa Vita vya Kwanza vya Dunia. Mwishoni mwa uhasama, alipokea Msalaba wa Vita wa Ubelgiji wa mitende. Baada ya vita, alisoma fizikia na hisabati, na akaanza kujiandaa kwa ukuhani wa jimbo, sio kwa Wajesuit. Alipata udaktari wake mwaka wa 1920 kwa tasnifu iliyoitwa Ukadiriaji wa kazi za vigeu kadhaa halisi, iliyoandikwa chini ya uongozi wa Charles de la Vallée-Poussin. Alipewa daraja la Upadre tarehe 22 Septemba 1923 na Kardinali Désiré-Joseph Mercier.

Mshiriki wa utafiti wa unajimu chuo Kikuu cha Cambridge

Mnamo 1923, alikuwa mshiriki wa utafiti wa unajimu katika Chuo Kikuu cha Cambridge, akitumia mwaka mmoja katika Nyumba ya Mtakatifu Edmund (sasa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Edmund, cha Cambridge). Huko alifanya kazi na Arthur Eddington, Quaker na mwanafizikia ambaye alimtambulisha kwa Elimu Anga ya kisasa, unajimu wa nyota, na uchanganuzi wa namba. Alikaa mwaka uliofuata katika Chuo cha Harvard Observatory huko Cambridge, Massachusetts, na Harlow Shapley, ambaye alikuwa amejipatia umaarufu kwa kazi yake ya nebulae, na katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (MIT), ambapo alijiandikisha kwa programu ya udaktari katika sayansi.

Kwa njia hiyo Lemaître, alikuwa Padre wa Kikatoliki wa Ubelgiji, mwanafizikia wa nadharia, mwanahisabati, mnajimu, na profesa wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Louvain. Alikuwa wa kwanza kutoa nadharia kwamba mdororo wa galaksi zilizo karibu unaweza kuelezewa na ulimwengu unaopanuka, ambao ulithibitishwa kwa uchunguzi punde baadaye na Edwin Hubble. Kwa mara ya kwanza alitoa "Sheria ya Hubble", ambayo sasa inaitwa sheria ya Hubble-Lemaître na IAU, na kuchapisha makadirio ya kwanza ya Hubble constant mwaka 1927, miaka miwili kabla ya makala ya Hubble. Lemaître pia alipendekeza nadharia ya Big Bang ya asili ya ulimwengu, akiiita dhahania ya atomi ya awali, na baadaye akaiita mwanzo wa ulimwengu.

20 June 2024, 16:20