Papa:Tupande mbegu ya Injili kwa uaminifu na uvumilivu kila eneo tunaloishi!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake Dominika tarehe 16 Juni 2024 akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume kwa kuwageukia waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican amesema: “Leo Injili ya Liturujia inatuzungumzia Ufalme wa Mungu kwa njia ya picha ya mbegu (Mk4,26-34). Mara nyingi Yesu anatumia mifano hii (rej. Mt 13,1-23; Mk 4,1-20; Lk 8,4-15), na leo hii anafanya kwa kutualika tutafakari kwa namna ya pekee inayohusishwa na mbegu tabia muhimu ile ya “kusubiri kwa matumaini.” Baba Mtakatifu amesema kiukweli katika kupanda, kwa kadiri ambavyo mkulima hupanda mbegu bora na nyingi ndivyo hiyo uandaa vizuri ardhi, na mimea aichomozi haraka: inahitaji muda! Kwa hiyo lazima baada ya kupanda, anapaswa kujua kusubiri kwa matumaini, ili kuruhusu mbegu ichupue kwa wakati unaofaa kwa kuibuka chipukizi kutoka ardhini na kukua, na inahitaji nguvu ya uhakika ili mwishowe, mavuno yawe mengi. (Mk 4, 28-29). Chini ya ardhi, muujiza tayari upo (Mk 4,27), kuna maendeleo makubwa lakini hayaonekani, inahitajika uvumilivu na wakati huo huo ni lazima kuendelea kupalilia, kumwagilia maji na kuhakikisha usafi, ingawa juu inaonekana hakuna kinachoendelea.
Hata Ufalme wa Mungu huko hivyo. Kwani “Bwana anaweka ndani mwetu mbegu za Neno lake, na za neema yake, mbegu nzuri na mbegu nyingi, na baadaye bila kuacha kutusindikiza, anasubiri kwa uvumilivu. Anaendelea kututunza, kwa tumaini la Baba, lakini anatupatia muda ili mbegu zichipuke, zikue na kuendelea hadi kutoa matunda kwa kazi nzuri. Na ndiyo sababu katika shamba lake inatajika kwamba pasiwepo chochote kipotee, na kwamba kila kitu kifikie ukomavu wake; na anataka kwamba sisi sote tuweze kukua kama masuke yaliyojaa mbegu. Na si hiyo tu. Baba Mtakatifu ameongeza: “kwa kufanya hivyo, Bwana anatupatia mfano kwani: anafundisha hata sisi kupanda kwa tumaini Injili mahali tulipo. Na baadaye kusubiri kwamba mbegu zilizopandwa zinaleta matunda kwetu sisi na kwa wengine, bila kukata tamaa, bila kuacha kusaidiana na kusaidia hata pale ambapo licha ya juhudi zetu tunaonekana kutoona matunda ya haraka. Mara nyingi kiukweli kati yetu, mbali na mtazamo wa kijujuu, muujiza tayari upo unaendelea na kwa wakati wake utazaa matunda mengi.
Baba Mtakatifu kwa njia hiyo amehitimisha kwa maswali: Je mimi niinaacha nipandwe Neno la Mungu? Je Mimi ninapanda kwa tumaini la Neno la Mungu katika maeneo ninayoishi?; Mimi ni mvumilivu kwa kusubiri, au ninakata tamaa kwa sababu sioni matunda haraka? Na ninajua kumkabidhi Bwana yote kwa utulivu, licha ya kufanya kila niwezalo kutangaza Injili? Bikira Maria aliyepokea na kufanya kukua mbegu yake ya Neno la Mungu, atusaidia kuwa wapandaji wakarimu na wa tumaini la Injili.