Papa amepyaisha maombi ya kwa ajili ya Sudan
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya tafakari la Neno la Mungu, Dominika tarehe 2 Juni 2024 ambapo Mama Kanisa ameshsherekea Siku Kuu ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo, Baba Mtakatifu Francisko baada ya Sala ya Malaika wa Bwana ametoa kwa upya mwaliko wa “kuiombea Sudan, ambako vita vilivyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja bado havijapata suluhisho la amani. Silaha zinyamazishwe na kwa kujitolea kwa mamlaka za mahalia na Jumuiya ya kimataifa, msaada uletwe kwa idadi ya watu na kwa watu wengi waliokimbia makazi yao; Wakimbizi wa Sudan wanaweza kupata kukaribishwa na ulinzi katika nchi jirani.”Alsisitiza Papa.
Baba Mtakatifu aidha amesema: “Na tusisahau Ukraine iliyoteswa, Palestina, Israel, Myanmar. Na ametoa “wito kwa hekima ya walio madarakani kusitisha ongezeko hilo na kufanya kila juhudi kushiriki katika mazungumzo na majadiliano.”
Papa amewasalimu mahujaji kutoka Roma na kutoka sehemu mbalimbali za Italia na ulimwenguni, hasa wale kutoka Kroatia na Madrid. Amewasalimu waamini wa Bellizzi na Iglesias; Kituo cha Utamaduni cha “Luigi Padova” huko Cucciago; Mapostulanti wa Binti wa Mlimani na kikundi cha “Baiskeli, wale ambao hawawezi”, waliokuja kwa baiskeli kutoka Faenza hadi Roma. Amewasalimu watoto wa Moyo Safi wa Bikira Maria. Na hatimaye amewatakia wote Dominika Njema na tafadhali wasisahu kumuombea. “Mlo Mwema, mchana mwema na kwaheri ya kuonana.” Papa amesema.