Askofu Trevisi:Kanisa la Trieste linataka kuwa maabara ya amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Askofu Enrico Trevisi, wa Jimbo la Trieste, akitoa salamu na shukrani kwa Papa, mara baada ya Misa Takatifu katika Uwanja wa Muungano wa Italia huko Trieste, Dominika tarehe 7 Julai 2024, alisema kuwa: "Sisi ni familia, jiji ambalo limejengwa kupitia mchango wa tamaduni nyingi na watu wengi lakini pia kwa mateso mengi na vurugu: na tunataka kuchukua changamoto ya kuwa maabara ya amani na mazungumzo pia kwa nchi nyngine ambazo bado wamegubikwa na mivutano na vita. Aidha alitoa shukrani “kwa niaba ya wazee na watoto wengi waliotufuatilia kwenye televisheni. Zawadi ya kwanza tunayokupati ni hizi mamia ya barua ambazo wazee na watoto walianza kumwandikia kwa hiari na ambazo basi tunavuna. Wao ni kama kubembeleza watu wengi, ishara za mapenzi na huruma zinazotoka kwao.” Alisema
Askofu huyo aliendelea kumweleza Papa: “Utakapohisi uchovu kidogo jioni, fikiria kuhusu kubembelezwa kwa mikono hii uliyopokea huko Trieste. Pia tunakuachia tafsiri ya kis asa ya picha ya Maria wa Afya iliyoundwa na mchoraji Amedeo Brogli, ambaye kwa watu wa Trieste amejitolea sana. Trieste ni jiji lisilo la kidini lakini ambalo bado linajua jinsi ya kujipatia furaha ya kumsifu Maria katika makanisa mengi yaliyowekwa kwake wakfu. Na katika shule ya Maria tumejitolea kuwaangalia kaka walio hatarini zaidi na akina dada, kuwasindikiza katika taabu zao. Tunaomba baraka zako,” lilikuwa ni ombi la Askofu kwa Baba Mtakatifu: "tunaomba kwa ajili ya Manuel, kijana anayesumbuliwa na ALS na wale wote wanaosumbuliwa na ALS na aina nyingine mbaya.
Tunaomba baraka zako kwa ajili ya Laura, Rita, Padre Carlo, Romana, Duja na wazee wote ili waweze kufurahia furaha ya kuwa familia ya Mungu kila wakati Simone na Anna, Lorenzo na Elisa waliofunga ndoa jana: na wapate furaha ya kujenga upendo wao juu ya upendo wa Mungu. sisi wenyewe kuwa wajasiri katika kuvumbua mifumo ya akili ili wakaribishwe kama wapendwa wa Mungu na si kama vitisho. Baraka pia kwa wafungwa wetu: inatia moyo kufikiria kwamba walichangia kuchora michoro miwili zinazopamba Altare hii. Katika Kanisa letu na kwa Kanisa zima la Italia tunaomba baraka zako katika kujua jinsi ya kuishi furaha ya Injili na kujua jinsi ya kuishiriki na mtu yeyote tunayekutana naye katika mitaa ya miji yetu.” Alihitimisha.