Tafuta

2024.07.02 Papa na Ibrahimu akiwa na kitabu chake mkononi. 2024.07.02 Papa na Ibrahimu akiwa na kitabu chake mkononi. 

Ibrahimu:Papa alibembeleza makovu yangu na kuwaombea wanaotafuta usalama

Kijana wa Senegal,aliyepokelewa Jumanne tarehe 2 Julai 2024 na Papa Francisko Nyumba ya Mtakatifu Marta,Vatican,alisimulia hisia za mkutano na Papa ambaye alimweleza historia yake,iliyojumuisha mateso katika magereza ya Libia na kutoa kitabu chakekilichoandikwa kutoa sauti kwa wale ambao hawakufanikiwa kufika nchi za Usalama.

Na Francesca Sabatinelli – Vatican

Papa alibembeleza makovu yake, akifumba macho, kwa hisia kali na kuahidi kuwaombea waliolala chini ya bahari, wanaume, wanawake na watoto ambao bado wamefungwa katika kambi za mateso za Libya, kwa wale wanaovuka jangwa la Sahara wakitafuta  mahali salama. Na kisha kwa maskini duniani kote, kwa wale, hasa katika bara la Afrika, ambao hawana uwezekano wa kupokea tone la maji au kuwa na sahani ya chakula. Na zaidi kwa wale wanaokufa chini ya mabomu. Ibrahimu Lo ana umri wa miaka 23 leo, alikuwa na umri wa miaka 16 alipoondoka nchini  Senegal mnamo mwaka 2017, kuelekea Ulaya. Yeye, pamoja na Ebrima Kuyateh wa Gambia, na Pato, mume wa Fati na baba wa Marie, ambaye alikufa kwa kiu jangwani  na  ambaye tayari alikutana na Papa Franciskpomnamo Novemba 2023 , walipokelewa na Papa  Francisko, Jumanne alasiri tarehe  2 Julai 2024 katika Nyumba ya Mtakatifu Marta wakisindikizwa  miongoni mwa wengine, na Padre  Mattia Ferrari, ambaye ni Mhudumu wa Kikanisa katika Shirika la Huduma ya kibinadamu ya Mediterrane na Luca Casarini, mwanzilishi wa  Shirika lisilo la Kiserikali (NGO).

Mkutano na Papa Francisko

Niliguswa sana waliponipigia simu kwa sababu Papa alitaka kutuona, alisiema na kusisimka  alisema kijana  Ibrahima  na kwamba kwa kawaida unapomuona kwa mbali, amezungukwa na watu wengi, na badala yake siku ile nilikuwa naye chumbani na niliweza kumgusa mkono wangu. Na akaniambia: 'Ibrahima, nilikuona, hujambo,  unaishi wapi? Nilimpatia kitabu changu na kumsimulia  historia yangu na kumuomba asali kwa aji ya wale wanaoteseka, na zaidi kwa ajili ya rafiki yangu ambaye tukiwa Libya gerezani alikuwa anaota ndoto ya kufika Italia ili aweze kuwa mchezaji wa mpira.  Lakini hakufanikiwa, aliishia baharini, na Papa aliniambia ataomba. Pia nilimwambia kuwa mimi ni Muislamu, lakini nikajiunga kuwa skauti kwa sababu naamini udugu. Yeye aliniambia: 'Sisi sote ni ndugu na sisi sote ni watoto wa Mungu'. Hili lilinigusa sana.” Alisimumilia Ibrahimu.

Makovu ambayo hutoa nguvu

Ibrahimu  kwa sasa anaishi Venizia  na ndiye mwandishi wa vitabu viwili,  kilichopishwa cha pili hivi karibuni, tarehe 5 Juni 2024 chenye kichwa: “Safari Mpya - Sauti Yangu kutoka ufukweni mwa Afrika hadi mitaa ya Ulaya” na cha kwanza ni: “Mkate na maji. Kutoka Senegal hadi Italia kupitia Libya,” vitabu hivi vinatoa shuhuda za wanaume, wanawake na watoto, za wale waliofanikiwa na wale ambao hawakuweza kufanikiwa na kuishia katika kaburi la baharini.

Kitabu kinachoelezea makovu hayo yaliyoguswa na Papa na ambayo yanampatia Ibrahimu nguvu ya kuendelea kusimulia uzoefu wake, kile cha mvulana ambaye katika safari ya miezi sita, kuanzia Senegal, alitumia majuma matatu tu kuwa na uhuru, na mengine yote wakati alipokuwa katika magereza ya Libya, akipigwa na kuteswa kila siku. “Walibya hawa walipofika kwenye gereza, walituambia ili tutoke gerezani tutalazimika kulipa fedha ambazo hatukuwa nazo, wakatuamuru tuwape namba ya mtu anayeweza kutulipia. Sisi watatu, Wanigeria wawili na Mgambia, hatukuwa na mtu” na Walibya waliwaua mbele ya macho ya Ibrahimu. Utetezi wa mvulana huyu wa miaka 16 dhidi ya kupigwa kwa watesi wake ulikuwa mikono yake, kitu pekee alichoweza kufanya ni kuiinua ili “kulinda kichwa changu”, na ndiyo ambayo leo inabeba makovu yaliyoguswa na Papa.

Moussa, Farah na wale ambao hawakufanikiwa

Ibrahimu ana shangazi yake pekee huko Senegal, uamuzi wa kuondoka kwenda Ulaya ulitokana na kuwa yatima, mwenye ndoto ya kuwa “mwandishi wa habari kutoa sauti kwa wale ambao hawana sauti.” Na hata safari ngumu kama hiyo hakuruhusu kupata marafiki, ni watu unaokutana nao barabarani, ambao unabadilishana nao mawasiliano, ya wale kwenye mitandao ya kijamii. “Lakini ni wachache walionijibu,  na ina maana hawakufanikiwa, ni maumivu ya Ibrahimu.” Kumbukumbu ambayo daima ataibeba moyoni mwake  ni uokoaji wake na wa watu wote waliokuwa kwenye boti pamoja naye. Huo ndio ulikuwa wakati sahihi ambapo hofu ilikoma. “Ilikuwa hofu tuliyokuwa nayo nyuma yetu, sio mbele yetu, kwa sababu tuliogopa kutekwa tena na Walibya, na wakati huo ingekuwa bora kufia baharini badala ya kurudi Libya kupata mateso yasiyoisha.” Alilalamika.

Ibrahimu alikumbuka kwamba pamoja na mmoja wake kulikuwa na uokoaji mwingine, lakini pamoja na watu 4 tu, mia nyingine au zaidi waliokuwa kwenye boti walipandishwa kwenye mtumbwi wakiwa  katika mifuko nyeusi, na kisha nikagundua kuwa hawakufanikiwa kuokoka. Kama vile Moussa au Farah hawakufanikiwa, wa kwanza alikuwa “rafiki yangu ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa mwanasoka,” wakati, Farah, “alikuwa mwanamke mwenye kiburi, tulipokuwa Libya, Walibya walikuwa wakumchukua kwa nguvu zao nyumbani.” Papa alizungumza na Ibrahimu na Pato kuhusu makovu, yale ya mwili na ya moyo, ambayo, anaelezea kijana wa Senegal,  kuwa:  “hakuna dawa wala daktari au hata hospitali”, kwa sababu ni magonjwa ambayo watayabeba daima, Ibrahimu na wengine pamoja.

Ushuhuda wa Ibrahimu
05 July 2024, 17:48