Jimbo kuu la Quebec, lililoko nchini Canada linaadhimisha Jubilei ya Miaka 350 tangu kuanzishwa kwake. Jimbo kuu la Quebec, lililoko nchini Canada linaadhimisha Jubilei ya Miaka 350 tangu kuanzishwa kwake.   (Vatican Media)

Jubilei ya Miaka 350 Tangu Kuanzishwa Kwa Jimbo kuu la Quebec Nchini Canada

Ni katika muktadha wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 350 tangu kuanzishwa kwa Jimbo kuu la Quebec, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Kardinali Jean-Marc Noël Aveline wa Jimbo kuu la Marseille lililoko nchini Ufaransa kuwa Mwakilishi wake maalum katika hitimisho la Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka Miaka 350 tangu kuanzishwa kwa Jimbo kuu la Quebec. Maadhimisho haya yatahitimishwa kuanzia tarehe 20 hadi tarehe 22 Septemba 2024.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Jimbo kuu la Quebec, lililoko nchini Canada linaadhimisha Jubilei ya Miaka 350 tangu kuanzishwa kwake. Jubilei hii ilizinduliwa tarehe 8 Desemba 2023 na itahitimishwa rasmi kuanzia tarehe 20 hadi 22 Septemba 2024. Uzinduzi huu umefanyika kwenye Kanisa kuu la kihistoria la “Notre-Dame-de-Québec.” Sherehe hii ya kiliturujia imewakumbusha waamini matendo makuu ya Mungu toka mwanzoni mwa historia ya ukombozi wa binadamu. Baada ya dhambi ya Adam na Eva, Mungu hakutaka kuwaacha binadamu peke yao katika maovu. Kwa sababu hiyo alimtazama Bikira Maria na akamfikiria kwa upendo, na akataka awe Mama wa Mkombozi wa wanadamu. Mbele ya ukubwa wa dhambi, Mungu akajibu kwa msamaha kamili. Huruma ya Mungu itakuwa daima kubwa kuliko dhambi yoyote, na hakuna awezaye kuuwekea mipaka upendo wa Mungu anayesamehe daima. Siku hii Mlango Mtakatifu wa Miaka 350 tangu kuanzishwa kwa Jimbo kuu la Quebec umefunguliwa.

Jubilei ya Miaka 350 ya Jimbo kuu la Quebec, Canada
Jubilei ya Miaka 350 ya Jimbo kuu la Quebec, Canada

Kumbe, ni Mlango wa Huruma ya Mungu, ambao kwa njia yake yeyote aingiaye ataonja mapendo ya Mungu: anayefariji, anayesamehe, na anayewapatia waamini tumaini. Jubilei ya Miaka 350 tangu kuanzishwa kwa Jimbo kuu la Quebec ni kipindi cha Mwaka Mtakatifu unaosimikwa katika toba na wongofu wa ndani; ni wakati wa kujitafutia rehema kamili, neema na baraka katika maisha. Ni kipindi cha hija takatifu za maisha ya kiroho na kwamba, kuanzia Mwezi Julai 2023 hadi Mwezi Oktoba 2024 Mlango wa Huruma ya Mungu utafunguliwa.

Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 350 ya Jimbo kuu la Quebec: neema
Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 350 ya Jimbo kuu la Quebec: neema

Inasadikiwa kwamba, Mtakatifu Yakobo Mtume alizikwa Kanisani humo. Ni katika muktadha wa Maadhimisho ya Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili, Mlinzi na Mwombezi wa Jimbo kuu la Quebec, tarehe 8 Desemba 2023, Baba Mtakatifu Francisko, aliwatakia heri na baraka katika Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 350 tangu kuanzishwa kwa Jimbo kuu la Quebec. Hili ni jimbo la kwanza kabisa kuanzishwa nchini Canada. Baba Mtakatifu akawaweka watu wa Mungu Jimbo kuu la Quebec chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili. Ni katika muktadha wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 350 tangu kuanzishwa kwa Jimbo kuu la Quebec, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Kardinali Jean-Marc Noël Aveline wa Jimbo kuu la Marseille lililoko nchini Ufaransa kuwa Mwakilishi wake maalum katika hitimisho la Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka Miaka 350 tangu kuanzishwa kwa Jimbo kuu la Quebec.

Jubilei ya Kipindi cha shukrani, neema na baraka, toba na wongofu wa ndani
Jubilei ya Kipindi cha shukrani, neema na baraka, toba na wongofu wa ndani

Itakumbukwa kwamba, Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo inanogeshwa na kauli mbiu “Peregrinantes in spem” yaani: “Mahujaji wa Matumaini.” Jubilei hii ni muda muafaka wa kupyaisha imani, matumaini na mapendo thabiti, kwa kuishi kama ndugu wamoja, sanjari na kusikiliza pamoja na kujibu kilio cha Dunia Mama na Kilio cha Maskini. Ni muda wa toba na wongofu wa ndani na wa kiikolojia, tayari kusimama kidete kulinda na kutunza mazingira nyumba ya wote. Ni muda muafaka kwa waamini kujikita katika kutangaza na kushuhudia imani na matumaini yanayomwilishwa katika huduma ya upendo kwa Mungu na jirani; kwa kukazia umoja na utofauti wa wateule watakatifu wa Mungu. Jubilei ni muda uliokubalika na Mwenyezi Mungu wa kuhakikisha kwamba, waamini wanajitahidi kumwilisha karama na mapaji yao kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Lengo ni kutangaza na kushuhudia imani na furaha ya Injili kwa watu wa Mataifa. Kumbe, kama sehemu ya maandalizi ya Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo, waamini wanahamasishwa kujikita katika sala, chemchemi ya baraka na neema zote.

Jubilei miaka 350 Quebec
20 July 2024, 13:11