Kard.Zuppi: Wakatoliki nchini Italia hawajiweki kando ni watetezi wa wote
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Matteo Maria Zuppi, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia, katika salamu zake kwa Baba Mtakatifu Francisko, mwanzoni mwa mkutano na washiriki 900 kutoka Italia yote katika Toleo la 50 la Juma ya kijamii la Wakatoliki nchini Italia, Dominika tarehe 7 Julai 2024, alitoa tathmini ya awali ya siku hizi walizojikita nazo huko Trieste kuhusu mada ya moyo wa demokrasia hasa. Kardinali Zuppi alisema: "Katika siku hizi hatujazungumza juu ya ushiriki tu bali tumeishi, kama katika miaka ya hivi karibuni katika mchakato wa njia ya Sinodi ya Kanisa la Italia. Na shauku imeongezeka, hamu ya kushiriki, kusaidia demokrasia hai katika nchi yetu na Ulaya, si ya ustawi wa mtu binafsi, lakini ya manufaa ya wote.
Akishirikisha juu ya Historia na Wakati Ujao, Askofu Mkuu wa Bologna alisisitiza kuwa "Wakatoliki nchini Italia hawana ukumbi wa kutetea masilahi fulani na kamwe hawatashiriki, kwa sababu sehemu pekee wanayoipenda ni ya mtu, kila mtu, mtu yeyote, tangu mwanzo wa maisha hadi mwisho wa uhai wake. Kardinali Zuppi katika hotuba hiyo alikumbusha kwamba: "kwa kuunganisha kiroho na kijamii kama Yesu anavyotuomba, tunaweza mara moja kuwa kile ambacho Mungu anataka: Wimbo wa Fratelli tutti", yaani wa 'Wote ni Ndugu wa kweli wa upendo na tofauti zinaimba utukufu wa Mungu na wa mwanadamu ambaye anamtunza na kumjali.”
Na akimgeukia Papa, Kardinali amemfafanua kama "mshairi wa kwanza wa kijamii, kwa sababu ya kiroho! kiongozi wa familia ambayo ni Kanisa la Italia na ambalo daima na kipekee lina mweka Yesu katikati yake na kwa sababu hiyo jirani, kuanzia yeye na ndugu zetu wadogo.” Kwa kutazama Trieste na Friuli Venezia Giulia ambao wamekuwa mwenyeji wa hafla hiyo, rais wa Baraza la Maaskofu Italia(CEI), aliwafafanua kama ardhi inayounganisha mashariki na magharibi, kaskazini na kusini, mahali pa kukutana na maarifa, yaani Uwanja wa kweli wa Muungano wa Italia.
Kardinali aidha alikumbusha kwamba wajumbe wa majimbo, vyama, harakati na vikundi mbalimbali walipata utamaduni mwingi unaounganisha, matokeo ya mapafu mawili maarufu muhimu kwa kupumua vizuri. Kardinali Zuppi alisema kuwa “Pia tulipata majeraha ya urithi wa maumivu ya kutisha kwa pande zote. Mikutano kama hii husaidia kuleta pamojazile tofauti kwa kile tulicho nacho cha utajiri kwa wote."
Kwa kufafanua zaidi, Kardinali Zuppi alisema: “Tunataka, kuzaa matunda ya demokrasia ya kweli, ya usawa, ya haki na wajibu kwa wote. Katika moyo wa demokrasia kuna watu na kuna mtazamo wa uaminifu na matumaini." Na akihitimisha kwa kulinganisha demokrasia na Bendi yenye vyombo vingi, na kila mwanamuziki ajiandaa, anavyopaswa kuwa, ili atoe kilicho bora. Kila ala ya muziki ni muhimu, lakini katika Bendi nzima kila mtu anahitaji kufanana na wengine. Kwa hivyo maelewano ya ajabu na sauti hupatikana. Na ndivyo hivyo tunavyofikiri kuhusu demokrasia."