Madhabahu kimsingi ni mahali pa: Sala na Ibada kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa, anayetoa machozi ya faraja kwa wale wanaoteseka na kuhuzunika huku Bondeni kwenye machozi. Madhabahu kimsingi ni mahali pa: Sala na Ibada kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa, anayetoa machozi ya faraja kwa wale wanaoteseka na kuhuzunika huku Bondeni kwenye machozi. 

Madhabahu Ni Kitovu cha Uinjilishaji wa Kina: Kiroho na Kimwili

Maelfu ya mahujaji kutoka ndani na nje ya Ukraine wamekuwa wakifika madhabahuni hapo kwa ajili yak usali, lakini kwa namna ya pekee wakati huu wa ghadhabu ya vita, ili kumlilia Mama wa Mungu amani, furaha, ustawi na maendeleo ya watu wa Mungu nchini Ukraine. Bikira Maria katika vizazi vyote ameonesha unyenyekevu wa kustaajabisha, amekuwa ni mwalimu wa amani katika ulimwengu na Kanisa katika ujumla wake, kamwe hajawaacha wanaokimbilia ulinzi wake!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Madhabahu ni mlango wazi wa uinjilishaji mpya unaokita mizizi yake katika moyo wa: Ukarimu kwa mahujaji; maisha ya sala, lakini zaidi kwa kuwasaidia waamini kujifunza kusali: Sala ya Kanisa sanjari na maadhimisho ya Sakramenti za Kanisa, hususan Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na Upatanisho, Mahakama ya huruma ya Mungu! Baba Mtakatifu Francisko anasema, Madhabahu yawe ni mahali pa sala na ukimya, ili kutoa nafasi kwa mahujaji kuzungumza na Mwenyezi Mungu kutoka katika undani wa maisha yao! Madhabahu ni mahali pa kuonjeshana upendo na ukarimu, ili kila hujaji anapofika mahali hapa aweze kujisikia kuwa yuko nyumbani anakaribishwa, kuthaminiwa na kupendwa. Mara nyingi watu wanafanya hija kutokana na kuvutwa na Mapokeo, utajiri wa sanaa, uzuri wa mazingira pamoja na kufuata ushauri kutoka kwa jirani zao! Mahujaji kama hawa wanapoonja ukarimu, mioyo yao inafunguka na hivyo kuanza kujenga urafiki na hatimaye, kujiaminisha kwa Kristo na Kanisa lake! Watu wanaweza kukata tamaa, ikiwa kama hawataonja ukarimu kutoka kwa wenyeji wao!

Kardinali Parolin kumwakilisha Papa nchini Ukraine, Siku ya Kuombea Amani
Kardinali Parolin kumwakilisha Papa nchini Ukraine, Siku ya Kuombea Amani

Madhabahu kimsingi ni mahali pa: Sala na Ibada kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa, anayetoa machozi ya faraja kwa wale wanaoteseka na kuhuzunika huku Bondeni kwenye machozi. Ni mwombezi wa watu waliovunjika na kupondeka moyo; watu waliokata tamaa na kwamba, Bikira Maria anajaribu kujibu sala ya kila mwamini anayekimbilia ulinzi na tunza yake ya daima. Madhabahu ni mahali ambapo panapaswa kukuza na kudumisha ari na moyo wa Sala ya Kanisa, maadhimisho ya Sakramenti za Kanisa kama sehemu ya kazi ya ukombozi. Ni mahali pa shuhuda za: imani, matumaini na mapendo, kielelezo cha Kanisa linalokesha na kusali daima! Madhabahu ni mahali pa ukimya unaopaswa kububujika kutoka katika undani wa mahujaji, tayari kuomba: baraka, neema na rehema pamoja na kudumisha upendo kwa Mungu na jirani! Madhabahu ni mahali pa kuonja huruma na upendo wa Mungu unaofumbatwa katika Sakramenti ya Upatanisho, Mahakama ya huruma ya Mungu. Maeneo kama haya yanahitaji wakleri waliofundwa barabara, watakatifu, vyombo na mashuhuda wa huruma na upendo wa Mungu kwa waja wake. Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, katika madhabahu, kamwe hawatakosekana Wamisionari wa huruma, mashuhuda wa upendo wa Mungu unaokoa na kuponya! Madhabahu yawe ni mahali pa kumwilisha upendo, kielelezo cha utekelezaji wa Amri ya Upendo kwa Mungu na jirani!

Tarehe 21 Julai 2024 Siku ya Kuombea Amani nchini Ukraine
Tarehe 21 Julai 2024 Siku ya Kuombea Amani nchini Ukraine

Ni katika muktadha huu wa hija ya watu wa Mungu, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kuwa ni Mwakilishi wake katika maadhimisho ya kufunga hija ya watu wa Mungu kutoka katika Madhehebu ya Kilatini kutoka sehemu mbalimbali za Ukraine, Dominika tarehe 21 Julai 2024 kwenye Madhabahu ya Bikira Maria ya Berdychiv. Kardinali Parolin, katika Ibada hii anafuatana na Padre Ruslan MYKHALKIV, Gambera wa Seminari ya Jimbo Katoliki la Kyiv-Zhytomir; pamoja na Padre Andriy LEHOVICH, Katibu muhtasi wa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Lviv, nchini Ukraine. Madhabahu ya Bikira Maria wa Berdychiv yalitambuliwa kuwa ni Madhabahu ya Kitaifa kunako mwaka 2011 na yanasimamiwa na kuendeshwa na Watawa wa Bikira Maria wa Mlima Karmeli, huduma inayotekelezwa kwa ibada na uaminifu. Maelfu ya mahujaji kutoka ndani na nje ya Ukraine wamekuwa wakifika madhabahuni hapo kwa ajili yak usali, lakini kwa namna ya pekee wakati huu wa ghadhabu ya vita, ili kumlilia Mama wa Mungu amani, furaha, ustawi na maendeleo ya watu wa Mungu nchini Ukraine. Bikira Maria katika vizazi vyote ameonesha unyenyekevu wa kustaajabisha, amekuwa ni mwalimu wa amani katika ulimwengu na Kanisa katika ujumla wake.

Bikira Maria Malkia wa Amani awaombee Ukraine haki na amani.
Bikira Maria Malkia wa Amani awaombee Ukraine haki na amani.

Kardinali Pietro Parolin, anakwenda kuwatia shime watu wa Mungu nchini Ukraine, ili wasikate tamaa kutokana na changamoto wanayokabiliana nayo, na kwamba, huu ni ushuhuda wa mshikamano wa pekee na Khalifa wa Mtakatifu Petro kwa watu wa Mungu nchini Ukraine. Baba Mtakatifu Francisko anawasihi waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, tarehe 21 Julai 2024 kumlilia Bikira Maria Malkia wa Amani kuwafikishia maombi yao mbele ya Mwenyezi Mungu ili hatimaye, aweze kusitisha vita sehemu mbalimbali za dunia. Mwenyezi Mungu ambaye amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao, amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi, na wanyonge amewakweza. Rej. Lk 1: 51-52. Baba Mtakatifu Francisko anamsihi Kardinali Pietro Parolin awafikishie watu wa Mungu salam na matashi mema, watu wote wa Mungu ndani na nje ya Ukraine, watakaohudhuria Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kufunga hija kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Berdychiv. Baba Mtakatifu Francisko anasema, ataungana nao kiroho katika maadhimisho haya.

Hija Ukraine

 

18 July 2024, 14:26