Tafuta

Papa Francisko amependa kuwahakikishia watu wa Mungu nchini Ethiopia walioathirika na maporomoko ya udongo yaliyotokea tarehe 22 Julai 2024 uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala na sadaka yake. Papa Francisko amependa kuwahakikishia watu wa Mungu nchini Ethiopia walioathirika na maporomoko ya udongo yaliyotokea tarehe 22 Julai 2024 uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala na sadaka yake.  

Maporomoko ya Udongo Yasababisha Watu Zaidi ya 260 Kupoteza Maisha Ethiopia

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 28 Julai 2024 kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, amependa kuwahakikishia watu wa Mungu nchini Ethiopia walioathirika na maporomoko ya udongo yaliyotokea tarehe 22 Julai 2024 uwepo wake kwa njia ya sala na sadaka yake. Watu zaidi ya 260 wamekwisha kupoteza maisha na wengine wengi hawajulikani mahali walipo; msaada wa dharura unahitajika.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Maporomoko ya udongo yaliyotokea tarehe 22 Julai 2024 katika eneo la Geze Gofa, Kencho Shasa Gozdi Kebele, Geze Gofa na Woreda, maeneo yaliyoko Kusini mwa Ethiopia yamepelekea watu zaidi ya 260 kufariki dunia, na idadi kubwa ya watu hawajulikani mahali walipo! Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu “UNOCHA” imesema kwamba, idadi hii inaweza kuongezeka maradufu. Watu zaidi ya 15,000 wameathirika kutokana na maporomoko ya udongo na kwamba, wanahitaji msaada wa dharura. Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 28 Julai 2024 kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, amependa kuwahakikishia watu wa Mungu nchini Ethiopia walioathirika na maporomoko ya udongo yaliyotokea tarehe 22 Julai 2024 uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala na sadaka yake.

Maporomoko ya ardhi: watu zaidi ya 260 wamepoteza maisha
Maporomoko ya ardhi: watu zaidi ya 260 wamepoteza maisha

Baba Mtakatifu anapenda kuwatia shime wale wote wanaowahudumia waathirika, kuendelea kuonesha moyo wa upendo na mshikamano wa udugu wa kibinadamu. Kwa upande wake Kardinali Berhaneyesus Demerew Souraphiel, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Addis Ababa nchini Ethiopia ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ethiopia anapenda kuwahakikishia waathirika wote mshikamano wa upendo kutoka kwa Kanisa Katoliki katika kipindi hiki kigumu katika historia ya maisha na utume wao. Takwimu zinaonesha kwamba, familia 5,776 zinahitaji hifadhi ya dharura na kati ya watu wote hawa, kuna idadi ya watoto 1, 367.

Maafa Ethiopia
29 July 2024, 14:22