Nia za Papa Francisko kwa Mwezi Julai 2024:kwa ajili ya uchungaji wa wagonjwa!

Katika nia za Papa kwa Mwezi Julai 2024 zinazosambazwa na Mtandao wa Utume wa Sala Kimataifa wa Papa mada ni:“kwa ajili ya Uchungaji wa wagonjwa” ambapo Papa anawaalika waamini kwamba:“Tuombe ili Sakramenti ya Mpako wa wagojwa iwapatie watu wanaipokea na wapendwa wao nguvu za Bwana na wageuka daima kwa wote zaidi kuwa ishara inayoonekana ya huruma na ya matumaini.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika nia za sala kwa Mwezi Julai 2024 zinazosambazwa na Mtandao wa Utume wa Sala Kimataifa unaongozwa na  mada: “kwa ajili ya Uchungaji wa wagonjwa,” ambapo kwa njia ya video  akizungumza kwa lugha ya kihispania, Papa anasema: “Mpako wa Wagonjwa  sio sakramenti  tu ya  wale wambao wako karibu ya kufa. Hapana! Ni muhimu kwamba hilo lieleweke wazi. Wakati Padre anamkaribia mtu kwa ajili ya kumpatia Mpako wa wagonjwa, si kwamba yupo anamsaidia ili aage maisha. Kufikiria hivyo maana yake ni kukataa kila tumaini.” Baba Mtakatifu katika ujumbe huo aidha anakazia kusema kuwa: hiyo “utafikiri ni kama kusema kuwa baada ya Padre, anafika yule anayekuja kuchukua maiti. Tukumbuke kwamba Mpako wa wagonjwa ni moja ya “Sakramenti ya uponyaji”  ya kutibu” ambayo inatakasa roho.”

Mtu akiwa naumwa sana anashauriwa apewe mpako wa Wagonjwa na pia wazee

Baba Mtakatifu Francisko vile vile amefafanua kuwa “Wakati mtu ambaye anaumwa sana inashauriwa kutoa Mpako wa wagonjwa. Na ikiwa mtu ni mzee ni vizuri kupokea Mpako wa wagonjwa. Tuombea ili Sakramenti ya Mpako wa wagonjwa iweze kuwapatia watu ambao wanaipokea na wapendwa wao, nguvu ya Bwana na wageuke kuwa daima kwa wote zaidi ishara inayoonekana ya huruma na matumaini.”

Kipimo cha jumuiya ya sakramenti kukuza imani na joto kidugu

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari katika kuwasilisha Video ya Papa, inabainisha kwamba “Sakramenti za Kanisa ni zawadi, ni njia ambazo Yesu anajifanya kuwa sasa ili kubariki, kuhimiza, kusindikiza na kufariji. Na hivyo ndivyo ilivyo pia katika utoaji wa sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa, sakramenti inayotoa faraja kwa wale wanaougua magonjwa na wapendwa wao. Basi ni sakramenti ya asili ya jumuiya. Katika taarifa hiyo pia inakumbusha kile ambacho Papa Francisko alizungumza kwenye katekesi ya  tarehe 26 Februari 2014 kwamba: “Wakati wa uchungu na ugonjwa hatuko peke yetu: Padre  na wale wanaokuwepo wakati wa Mpako wa Wagonjwa wanawakilisha jumuiya nzima ya Wakristo ambao  kama kundi moja, hukusanyika karibu na wale wanaoteseka na familia zao, kukuza imani na matumaini kwao, na kuwaunga mkono kwa sala na joto la kidugu.”

Picha za video ni kutoka majimbo ya Marekani

Picha za Video ya Papa, zilizopigwa katika majimbo ya  Marekani ya Allentown, Pennsylvania, na Los Angeles, na California, zinashuhudia hili kwa kusimulia historia mbili tofauti, lakini zinazohusishwa na neema ya sakramenti, na kuweka nuru ya mazingira tofauti ambayo yanaweza kusimamiwa.

Padre Fornos: hatusiti kupendekeza Mpako wa Wagonjwa

Ikiwa Mpako wa Wagonjwa haupaswi kuonekana kama ishara ya kimuujiza ya kumponya mgonjwa, pia haupaswi kuzingatiwa kama ishara ya kifo cha karibu. Badala yake, unahakikisha ukaribu wa Yesu kwa maumivu ya mgonjwa, faraja yake na msamaha wake. Tena katika Katekesi ya  2014, Papa Fransisko alisisitiza kuwa Mpako wa Wagonjwa ni, na mara nyingi, ni sakramenti iliyosahaulika au inayotambulika kidogo wakati  ina maana yake nzuri.” Kwa maoni ya  Padre Frédéric Fornos S.J., mkurugenzi wa kimataifa wa Mtandao wa Sala ya Kimataifa  ya  Papa, amesema “Ingawa wengi wamegundua tena kina cha sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa, bado inaeleweka kama njia ya kuwatayarisha wagonjwa katika kifo na mara nyingi kwa hivyo huahirisha, kwa njia hiyo: “Kuna wazo kidogo kwamba baada ya Padre kufika nyumbani basi mazishi yatafika,” anaandika Padre Fornos.

Padre kutoa Mpako wa Wagonjwa
Padre kutoa Mpako wa Wagonjwa

Ni kwa sababu hiyo basi, “Baba Mtakatifu Francisko anatamani mwezi huu tuweze kugundua tena undani na maana ya kweli ya sakramenti hiyo ya kwamba  sio tu kama maandalizi ya kifo, bali ni sakramenti inayotoa faraja kwa wagonjwa wakati wa magonjwa mazito, kwa wapendwa wao na nguvu kwa wale wanaowasaidia.” Mkurugenzi wa Mtandao wa Kimataifa amehitimishwa  kwa mwaliko huu: “Sote tunawajua wagonjwa, tunawaombea, na ikiwa tunaamini kwamba wanakabiliwa na ugonjwa mbaya - au labda ni wazee katika hali mbaya zaidi – tusisite kupendekeza kwao ili kupata sakramenti hii ya faraja na matumaini.”

Nia za Papa kwa mwezi Julai 2024:uchungaji kwa wagonjwa
02 July 2024, 17:24