Papa atoa wito kwa ajili ya amani kwa watu waliokandamizwa na hofu ya vita
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 14 Julai 2024 akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume mjini Vatican, ametoa wito wa kusali kwa ajili ya Ukraine inayoteswa, Palestina, Israel, Myanmar”. Ni maombi aliyo walekeza waamini wanaokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, bila kuogopa jua kali sana, jijini Roma ili kumwomba Mungu na Maria ambaye Papa amewakabidhi maeneo hayo yaliyokumbwa na vurugu. Vile vile Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha sikukuu ya kiliturujia ya tarehe 16 Julai, iliyoanzishwa ili kukumbuka Tokeo la Bikira wa Mlima Karmeli mnamo mwaka 1251. Kwa njia hiyo ameomba kwa maombezi yake: “Aawape faraja na kupata amani kwa watu wote wanaokandamizwa na hofu ya vita.”
Nchi iliyojeruhiwa na ghasia
Papa Francisko katika kutaja hali halisi aliorodhesha nchi zilizokumbwa na vita moja baada ya nyingine kuanzia na Ukraine, ambako mashambulizi ya Urusi, yamejikita zaidi katika maeneo ya Kharkiv na Kherson, na kuua raia katika siku za hivi karibuni na kusababisha majeraha mengi, hata watoto; Nchi Takatifu, iliyoshtushwa na mauaji ya hivi karibuni na mengine, huko Khan Yunis na waathriwa 90, wengi wao wakiwa wanawake na watoto; Myanmar iliyoharibiwa, zaidi ya miaka mitatu baada ya mapinduzi, na mapigano ya umwagaji damu, ambayo mara nyingi hupuuzwa na maoni ya umma ya kimataifa.
Maombi kwa mabaharia
Papa Francisko ametoa pia wito kwa ulimwengu kwa nchi hizi na ameomba maombi. Na ndiyo hizo hizo aliombea pia mabaharia wote, katika afla ya Dominika ya Mabaharia inayoadhimishwa kila Dominika ya Pili ya Mwezi Julai kila mwaka. “Tunawaombea wale wanaofanya kazi katika sekta ya bahari na wale wanaowajali.”
Chapisho la Papa kwa ajili ya Dominika ya Baharia
Tayari katika chapisho kwenye akaunti yake aliombea kwa familia zao, na ili Mungu awaongoze kwenye njia ya kuelekea Kristo.” Katika Ujumbe wa maadhimisho ya kilele cha Sikuhuu, uliotolewa tarehe 24 Juni 2023, uliotiwa saini na Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu aliwaalika Makanisa kutoa uonekanaji kwa wale wanaofanya kazi katika sekta ya bahari, ili kukuza utu na haki zao. Na alihimiza mabadilishano na mshikamano kati ya watu na dini kwamba “Hatuwezi kuwa wazi kwa uwezekano wa maisha ikiwa tunapendelea starehe tulizozizoea.”Kardinali Czerny aliandika.
Salamu kwa mahujaji
“Kaka na dada! Nawasalimu ninyi, Waroma na mahujaji kutoka Italia na nchi nyingi, hasa ninawasalimu washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Walei wa Shirika la Mtakatifu Augustino; Nawasalimu Masista wa Familia Takatifu ya Nazareti, wanaoadhimisha Mkutano Mkuu wao; Nawasalimu vijana kutoka parokia ya Luson (Alto Adige), ambao wamesafiri kupitia Njia ya Francigena; Baraza la Vijana la Mediterania, ambalo linamaanisha ujumbe wa Giorgio La Pira; vijana washiriki katika Kozi ya Kimataifa ya Waundaji wa Regnum Christi. Ninatuma salamu zangu kwa waamini wa Poland waliokusanyika katika Madhabahu ya Maria Mweusi huko Częstochowa, katika hafla ya hija ya kila mwaka ya familia ya Radio Maria. Ninawasalimu watoto wa Immaculate Conception.” Na hatimaye “Nawatakia wote Dominika njema. Na tafadhali msisahau kuniombea. Mlo mwema , Mchana mwena na kwaheri ya kukuona!