Tafuta

2024.07.04 Kitabu "Katika moyo wa Demokrazia(LEV). 2024.07.04 Kitabu "Katika moyo wa Demokrazia(LEV). 

Papa:demokrasia ni kutatua matatizo ya wote kwa pamoja!

Katika tukio la ziara ya PapaT rieste,Dominika Julai 7,kwa ajili ya kuhitimisha Juma la 50 la Mafundisho ya Kijamii kwa Wakatoliki Italia,gazeti la ‘Il Piccolo’lilichapisha maandishi ambayo hayajachapishwa ya Papa Francisko.Ni utangulizi wa anthologia ya hotuba na ujumbe wa Papa,kichwa:'Katika moyo wa demokrasia'.Kitabu kimehaririwa na LEV.Kitasambazwa bila malipo,Dominika kama kiambatisho cha gazeti.Uwasilishaji ni Kadinali Zuppi,Rais wa CEI.

Papa Francisko

Nina furaha kusema maneno haya ili kutambulisha andiko hili ambalo gazeti la ‘Il Piccolo” yaani 'Mdogo' na Nyumba ya Vitabu la Vatican (LEV) zinatoa kwa wasomaji, sanjari na ziara yangu ya Trieste katika hafla ya Juma la Kijamii. Uwepo wangu huko Trieste, jiji lenye ladha kali ya Ulaya ya Kati kutokana na uwepo wake wa pamoja wa tamaduni, dini na makabila mbalimbali, unatokea sanjari na tukio ambalo Baraza la Maaskofu wa Italia huandaa katika mji huu, Juma la  Mafundisho ya  Kijamii kwa  Wakatoliki nchini Italia, iliyojitolea mwaka huu na mada: Katika moyo wa demokrasia. Kushiriki kati ya historia na siku zijazo.”

Demokrasia, kama tunavyojua vyema, ni neno lililozaliwa katika Ugiriki ya kale ili kuonesha uwezo unaotumiwa na watu kupitia wawakilishi wao. Aina ya serikali ambayo, ikiwa kwa upande mmoja imeenea duniani kote katika miongo ya hivi karibuni, kwa upande mwingine inaonekana kuteseka na matokeo ya ugonjwa hatari, ule wa “mashaka ya kidemokrasia.” Ugumu wa demokrasia katika kuchukua jukumu la ugumu wa wakati huu,  fikiria shida zinazohusiana na ukosefu wa kazi au nguvu nyingi za dhana ya kiteknolojia - wakati mwingine inaonekana kutoa nafasi kwa mtazamo wa kiitikadi ambao, kwa misingi ya kanuni na mipango iliyochochewa kwa ujumla(populism).

Demokrasia ina thamani kubwa na isiyo na shaka iliyomo ndani yake: ile ya kuwa pamoja, ya ukweli kwamba utekelezaji wa serikali hufanyika ndani ya muktadha wa jamii inayojikabili yenyewe, kwa uhuru na kidunia, katika sanaa ya faida ya wote; ambayo si kitu bali ni jina tofauti kwa kile tunachokiita siasa. Pamoja ni sawa na kushiriki. Padre Lorenzo Milani na vijana wake tayari walisisitiza hili katika Barua yao ya ustadi kwa mwalimu: “Nimejifunza kwamba matatizo ya watu wengine ni sawa na yangu.

Kujiondoa pamoja ni siasa, kujiondoa peke yako ni ubadhirifu.” Ndiyo, matatizo tunayokabili ni ya kila mtu na yanahusu wote. Njia ya kidemokrasia ni kuijadili pamoja na kujua kwamba kwa pamoja tu matatizo haya yanaweza kupata suluhisho. Kwa sababu katika jamii kama binadamu mtu hawezi kujiokoa peke yake. Na wala del mors tua vita mea, yaani kusema kifo changu, maisha yangu.

Kinyume chake. Hata biolojia ya viumbe hai inatudokezea kuwa mwanadamu yuko wazi kimuundo kwa mwelekeo wa wengine na kukutana na  yeye ambaye yuko mbele yetu. Giuseppe Toniolo mwenyewe, mhamasishaji na mwanzilishi wa Juma la Mafundisho ya Kijamii, alikuwa msomi wa uchumi ambaye alielewa vyema mipaka ya uchumi wa homo oeconomicus,(hili  ni neno linalotumiwa kwa ukadiriaji au mfano wa Homo sapiens ambao hufanya kazi ili kupata ustawi wa juu zaidi kwao wenyewe kutokana na taarifa zinazopatikana kuhusu fursa na vikwazo vingine, vya asili na vya taasisi, juu ya uwezo wao wa kufikia malengo yao yaliyopangwa mapema.), yaani maono hayo ya kianthropolojia yenye msingi wa materialistic utilitarianism, yaani matumizi ya vitu, kama alivyoifafanua, ambayo humfanya mtu huyo atimize, na kukata mwelekeo wao wa kimahusiano.

Hapa, ningependa kusema hivi, nikifikiria leo juu ya nini maana ya moyo wa demokrasia: kwa pamoja ni bora kwa sababu peke yako ni mbaya zaidi. Kwa pamoja ni nzuri kwa sababu peke yako ni huzuni. Kwa pamoja inamaanisha kuwa moja jumlisha moja hailingani na mbili, bali tatu, kwa sababu ushiriki na ushirikiano hutengeneza kile ambacho wanauchumi wanakiita ongezeko la thamani, yaani, ile hisia chanya na karibu halisi ya mshikamano inayotokana na kushirikiana na kuendeleza mbele, kwa mfano katika ushindani, umma, masuala ambayo unaweza kupata muunganisho.

Hatimaye, ni hasa katika neno Ushiriki ambapo tunapata maana ya kweli ya demokrasia,  maana ya dhati ya kwenda kwenye moyo wa mfumo wa kidemokrasia. Katika serikali ya takwimu au za anayeunga mkono siasa  hakuna mtu anayeshiriki, kila mtu anasaidia, bila kutarajia. Demokrasia, kwa upande mwingine, inahitaji ushiriki, mahitaji ya kuweka juhudi ya mtu mwenyewe ndani yake, kuhatarisha makabiliano, kuleta maadili ya mtu, na sababu za mtu katika suala husika na kujiahatarisha. Lakini hatari ni ardhi yenye rutuba ambayo uhuru huota. Wakati  wanaposimama kwenye balikoni, kukaa karibu na  dirisha, mbele ya kile kinachotokea karibu nasi, haikubaliki tu kimaadili lakini pia, kwa ubinafsi, sio busara na wala haifai.

Kuna masuala mengi ya kijamii ambayo kwayo, katika kidemokrasia, tunaitwa kuingilia kati; hebu tufikirie juu ya makaribisho ya kiakili na ya ubunifu, ambao  ushirikiana na kufungamana wa watu wahamiaji, jambo ambalo Trieste wanalifahamu vyema kwa vile liko karibu na njia inayoitwa Balkan; tufikirie majira ya kupungua kwa watu  ambayo sasa inaathiri sana Italia yote, na hasa baadhi ya maeneo; tufikirie juu ya uchaguzi wa sera halisi za amani, ambazo zinaweka sanaa ya mazungumzo mbele na sio chaguo la kuweka silaha tena.

Kwa kifupi, ili ya kuwajali wengine ambayo Yesu anaendelea kutuonesha katika Injili kama mtazamo halisi wa kuwa watu. Kutoka Trieste, mji unaoelekea Bahari ya Mediterania, chemchemi ya tamaduni, dini na watu tofauti, mfano wa udugu wa kibinadamu ambao tunatamani katika nyakati hizi zilizotiwa giza na vita, inaweza kusababisha kujitolea kwa uhakika zaidi kwa maisha shirikishi ya kidemokrasia yanayolenga manufaa ya kweli ya pamoja.

Papa na Demokrasia

 

06 July 2024, 09:34