Tafuta

Papa Francisko:unahitajika ubunifu wa kujenga wakati ujao,demokrasia haifanyi kazi

Katika hotuba yake ya kwanza kwenye Kituo cha Mikutano huko Trieste katika Toleo la Juma la kijamii,Italia Papa Francisko amesisitiza juu ya sintofahamu kuwa ni saratani ya demokrasia na kutoa mwaliko wa ushiriki ambao lazima ufanyiwe mazoezi,mshikamano na ushirikishwaji kwa sababu udugu uweze kuchanua mahusiano ya kijamii.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika hotuba ya kwanza ya Baba Mtakatifu Francisko kwa washiriki wa Juma la 50 la Mafundisho ya Kijamii kwa Wakatoliki nchini Italia Dominika tarehe 7 Julai 2024, ikiwa ndiyo hitimisho, Papa ameanza akisema kuwa alisikia kwa mara ya kwanza wanazungumza Trieste kutoka kwa babu yake aliyekuwa amefanya kazi hapo kwa miaka kumi na nne. Yeye alikuwa anawafundisha nyimbo nyingi na mmoja ulikuwa kuhusu Treste: Jenerali Cadorna alimwandikia malkia: 'Ikiwa unataka kutazama Trieste, iangalie kwenye postikadi.” Na hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kusikia kuhusu jiji." Papa amesemea. Akijikita katika hotuba yake ameendelea kusema kuwa historia ya Juma la Kijamii inasukana na historia ya Italia na hiyo inasema mengi: “Inasema Kanisa moja nyeti katika mabadiliko ya kijamii, na yanaoelekea kuchangia wema wa pamoja. Uzoefu huu wa nguvu,ni  ambao wamependa kujikita nao katika tema kubwa ya sasa: “Katika moyo wa demokrasia, Ushiriki kati ya Historia na wakati ujao.

Mara baada ya kufika Trieste Papa ametia saini katika kitabu
Mara baada ya kufika Trieste Papa ametia saini katika kitabu

Baba Mtakatifu amesema kuwa Mwenyeheri Giuseppe Torniolo, aliyeanzisha mpango huo, kunako mwaka 1907, alikuwa amesema kuwa demokrasia inaweza kujieleza “utaratibu huo wa kiraia ambapo nguvu zote za kijamii, kisheria na kiuchumi, katika utimilifu wa maendeleo yao ya daraja, hushirikiana sawa na manufaa ya wote, na kusababisha matokeo ya mwisho kwa manufaa yaliyopo ya tabaka la chini.”Katika nuru ya ufafanuzi huo ni wazo kwamba katika ulimwengu wa leo, demokrasia haina afya nzuri. Na hii inatuhusu na inatupatia wasiwasi kwa sababu ndani mwake kuna mchezo wa wema wa binadamu na hakika kile ambacho ni cha kibinadamu kinaweza kuwa sintofahamu.

Papa Francisko huko Trieste
Papa Francisko huko Trieste

Nchini Italia ukomavu wa kawaida wa demokrasia uliibuka baada ya vita vya II vya dunia, shukrani hata kwa mchango na msimamo wa wakatoliki. Inawezekana kujivunia historia hii, ambapo imejikita hata uzoefu wa Juma la Kijamii na bila kufikiria historia za kizamani, lazima kupata ndani mwake mafundisho ili kuchukua jukumu la uwajibikaji wa kujenga jambo zuri katika wakati wetu. Hiyo tabia inayopatikana katika jarida ambamo mnamo 1988,Baraza la Maaskofu Italia walianzisha Juma la Kijamii. Papa Francisko amenukuu: “Kutoa maana kwa dhamira ya kila mtu katika mabadiliko ya jamii; kuzingatia watu ambao wanabaki nje au pembezoni mwa michakato na mifumo ya kiuchumi iliyofanikiwa; kutoa nafasi kwa mshikamano wa kijamii katika aina zake zote; kutoa msaada kwa urejeshaji wa maadili ya kutafuta faida ya wote [...]; kutoa maana kwa maendeleo ya nchi, inayoeleweka [...] kama uboreshaji wa kimataifa katika ubora wa maisha, kuishi pamoja, ushiriki wa kidemokrasia, na uhuru wa kweli".

Wakimkaribisha washiriki wa Juma la kijamii
Wakimkaribisha washiriki wa Juma la kijamii

Maono hayo, yaliyokita mizizi katika Mafundisho Jamii ya Kanisa, yanayokumbatia baadhi ya ukuu wa jitihada za kikristo na somo la Kiinjili la matukio ya kijamii ambavyo hayafai tu kwa muktadha wa Italia bali yanawakilisha onyo kwa jamii nzima ya kibinadamu na kwa ajili ya safari ya watu wote. Kiukweli kama ilivyo mgogoro wa demokrasia unapitia katika hali halisi tofauti na Mataifa, na wakati huo huo tabia ya uwajibikaji mbele ya mabadiliko ya kijamii yanaitwa kuelekea wakristo wote, mahali popote walipo wakiishi na kutenda kila sehemu ulimwenguni. Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa “Kuna picha ambayo inatoa mhutasari wa kile ambacho wao walichagua katika ishara ya tukio hilo: “ Moyo.” Kuanzia na sura hiyo Papa Francisko ametoa tafakari mbili ili kumwilisha mchakato wa wakati ujao.

Papa Francisko huko Trieste
Papa Francisko huko Trieste

Katika sehemu ya kwanza Papa amesema,  kufikiria mgogoro wa demokrasia, kama moyo uliojeruhiwa. Kile kinacholeta kizingiti cha ushiriki kiko mbele ya  macho yetu. Ikiwa ufisadi na uharamu vinajionesha katika moyo ulioshutuka, lazima kuwa na wasiwasi hata katika mitindo mingine ya ujumuishaji kijamii. Kila mara anapobaguliwa mtu, mwili wote wa kijamii unateseka. Utamaduni wa kubagua unaweka mji mahali ambapo hakuna nafasi kwa maskini, ukosefu wa watoto, watu wadhaifu, wagonjwa, watoto, wanawake na vijana. Unakuwa wa kibinafsi, yasiyo na uwezo wa kusikiliza na ya huduma kwa watu.

Katika muktadha huo Papa amemtaja pia Aldo Moro kuwa alikuwa anakumbusha kwamba: “Nchi haina demokrasia ya kweli ikiwa haimtumikii mwanadamu, ikiwa haina lengo lake kuu  la utu, uhuru, uhuru wa mtu, ikiwa haiheshimu mifumo ya kijamii ambayo mwanadamu kwa uhuru hukua na ambamo huunganisha utu wake mwenyewe.” Neno lenyewe Demokrasia, haliendi sambamba kirahisi na kura ya watu, bali linahitaji  kwamba iundwe hali kwa sababu watu wote waweze kujieleza na waweze kushiriki. Na ushiriki hauwezi kushtukizwa: unajifunza kuanzia wadogo, vijana na kuendeleza mazoezi, hata kwa maana ya kukosoa vishawishi vya kiitikadi na watu wengi.

Washiriki wa Juma la Kijamii Katoliki nchini Italia
Washiriki wa Juma la Kijamii Katoliki nchini Italia

Katika mantiki hiyo, Baba Mtakatifu aliongeza kusema, kama alivyopata fursa ya kukumbusha miaka iliyopita wakati akitembelea Bunge la Ulaya na Baraza la Ulaya , ni muhimu kufanya kuibuka: “Uhusiano wa  Ukristo ambao unaweza kutoa leo hii katika Maendeleo ya utamaduni na kijamii wa Ulaya kwa muktadha wa uhusiano thabiti kati ya dini na jamii” kwa kuhakikisha mazungumzo yenye matunda na jumuiya ya kiraia na kwa sera za kisiasa, kwa sababu kwa kutiwa nuru pamoja na kujikomboa na vizingiti vya kiitikadi, inawezekana kuanzisha tafakari ya pamoja ni juu ya mada zinazohusiana na maisha ya kibinadamu na kwa hadhi ya  mtu. Kwa lengo hilo, inabaki misingi yenye matunda ya mshikamano na ugawanyaji. Kiukweli watu wanazingatia pamoja kwa ajili ya mahusiano ambayo yanauwaunda, na mahusiano yanaweka nguvu wakati kila mtu anathamanishwa.

Papa Francisko huko Trieste
Papa Francisko huko Trieste

Demokrasia daima inataka hatua za kutoka upande mmoja hadi ushiriki, kutoka kushabikia hadi kuzungumza. “Ikiwa  mfumo wetu wa kichumi na  kijamii utaendelee kuzaa tena waathirika na kuwa na  watu wanaobaguliwa, hakutakuwa na siku kuu katika udugu wa kibinadamu  ulimwenguni. Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa “Jumuiya ya kibinadamu na kidugu ina uwezo wa kufanyia kazi kwa ajili ya kuhakikisha vya kutosha na msimamo kwamba wote wanaweza kusindikizwa katika mchakato wa maisha yao, na sio tu kutazamia mahitaji msingi, bali kwa sababu wanaweza kutoa ubora wao, hata ikiwa shukrani zao hazitakuwa bora, hata kama watakwenda taratibu, hata kama ufanisi wao hautakuwa na umuhimu sana." Wote tunapaswa kuhisi kuwa sehemu ya mpango wa pamoja; hakuna ambaye haisi hana maana. Baadhi ya mifumo ya huduma ambayo haitambui hadhi ya watu ni unafiki wa kijamii. Na sintofahamu ni saratani ya demokrasia.” Papa amesisitiza tena neno la usaidizi hasi kwamba katika njia hii tu, ni adui wa demokrasia, ni adui wa upendo kwa wengine. Na aina fulani za usaidizi hasi ambazo hazitambui hadhi ya utu wa watu ni unafiki wa kijamii. Tusisahau hili. Na ni nini nyuma ya kujitenga huku na ukweli wa kijamii? Kuna kutojali, ambako  ni saratani ya demokrasia, kushindwa kushiriki.

Papa Francisko Trieste
Papa Francisko Trieste

Baba Mtakatifu akifafanua tafakari ya pili ni kutia moyo wa ushiriki ili demokrasia ifanane na moyo uliotakasika. Na kwa maana hiyo inahitaji kufanyia mazoezi ya ubunifu. Ikiwa tunazama karibu yetu, tutaona ishara nyingi za matendo ya Roho Mtakatifu katika maisha ya familia na jumuiya. Hadi katika nyanja za kiuchumi, za kiteknolojia, kisisa na kijamii. Tifikirie aliyetoa nafasi ndani ya shughuli za kiuchum kwa mtu mwenye ulemavu; kwa wafanyakazi ambao walikataa haki yao ili kutopoteza nafasi za kazi kwa wengine; kwa jumuiya za nishati mbadala zinazokuza ikolojia fungamani, kwa kujitwisha mzigo wa familia wenye umaskini wa nishati; kwa wasimamizi wanaosaidia kuzaliwa  watoto, kazi, shuleni, huduma za elimu, nyumba zinazowezakana kuingia kwa wote, ushirikishwaji wa wahamiaji. Udugu unafanya kuchanua  mahusiano kijamii; na kwa upande mwingine kushugulikia wengine kunahitaji ujasiri wa kufikiria kama watu. Kwa bahati mbaya, aina hii ya watu, mara nyingi inatafsiriwa vibaya, na inawezekana kupelekea kuondoa neno la “demokrasia”(governo del popolo). Hii licha ya hayo, kwa kuthibitisha kuwa jamii ni zaidi ya jumla ya watu binafsi, neno  muhimu ni ‘watu’.

Katika Moyo wa demokrasia ilikuwa tema ya Juma la kijamii Italia
Katika Moyo wa demokrasia ilikuwa tema ya Juma la kijamii Italia

Kwa hakika ni ngumu zaidi kulinda jambo la ukubwa kwa muda mrefu, usipopatikana unakuwa ndoto ya pamoja.” Kwa hiyo demokrasia kutoka moyo uliotakasika inaendelea kukuza ndoto ya wakati ujao, inaweka mchezo, inawaalika watu kujihusisha na kwa kijumuiya. Tusidandanganywe na suluhishi rahisi, Papa amesema. Kinyume chake tuwe na ari ya wema wa pamoja. Tunasubiriwa na kazi ya kutocheza na neno la demokrasia na wala kulibadilisha kuwa katika vichwa vilivyo vitupu kwa yaliyomo, yenye uwezo wa kuhalalisha tendo lolote. Demokrasia siyo sanduku tupu, lakini inahusishwa na thamani ya  mtu, ya udugu na ya ikolojia fungamani. Kama wakatoliki, katika upeo huo hatuwezi kuridhika na imani ya pembeni au binafsi. Hii ina maana kwamba si kujidai kuwa tumesikilizwa, lakini zaidi kuwa na ujasiri wa kufanya mapendekezo ya haki na amani katika mijadala ya umma. Tuna jambo la kusema, sio fursa ya kujitetea. Lazima kuwa sauti ambayo inatangaza na ambayo inapendekeza katika jamii ambayo mara nyingi wana sauti na mahali ambapo wengi hawana sauti  Huo ndiyo upendo wa kisiasa, ambao hauridhiki na kutunza upendo lakini kutafuta kukabiliana na sababu.

Ziara ya Papa Trieste
Ziara ya Papa Trieste

Ni mtindo wa upendo ambao unaruhusu sera za kisiasa kuwa na uwezo wa uwajibikaji wake na kwa katika ubaguzi, ambao hutafakarisha na hausaidii kuelewa na kukabiliana na changamoto. Katika upendo huo wa kisiasa, mwaliko ni wa jumuiya nzima ya kikristo, katika utofauti wake wa huduma na karama. Baba Mtakatifu ameomba wafundwe katika upendo huo, kwa kuweka katika mzungumzo katika ulimwengu ambao ni mfupi wa shauku ya kiraia. Wajifunze daima na zaidi na kuwa bora kutembea pamoja kama watu wa Mungu, ili kuwa chachu ya ushirik katikati ya watu ambao wanafanya kuwa sehemu yake. Papa ameongeza kusema:“Na hili ni jambo muhimu katika utendaji wetu wa kisiasa, hata kwa wachungaji wetu: kujua watu, kuwa karibu na watu. Mwanasiasa anaweza kuwa kama mchungaji anayetangulia mbele ya watu, kati ya watu na nyuma ya watu. Mbele ya watu kuonesha njia kidogo; kati ya watu, kuwa na ladha ya watu; nyuma ya watu ili kuwasaidia wale wasiojiweza. Mwanasiasa asiye na mtazamamo kwa wananchi ni mwananadharia. Anakosa kilicho cha msingi.”

Papa huko Trieste
Papa huko Trieste

Giorgio La Pira alikuwa amefikia kutoa kipaumbele cha mji, ambao hauna uwezo wa kufanya vita, lakini ambao unalipa gharama ya juu zaidi. Na hivyo alikuwa anafikiria mfumo wa “madaraja,” kati ya mji wa ulimwengu ili kuunda fursa za umoja na mazungumzo. Kwa njia hiyo mfano wa La Pira, amesema  hawakosekani walei wakatoliki Italia wenye uwezo huo wa “kuandaa matumaini, wenye uwezo na mipango mizuri ya kisiasa ambayo inaweza kuzaliwa kuanzia chini. Kwa njia hiyo Papa ameuliza maswali: Je kwanini wasianzishe kusaidia na juhudi nyingi kwa ajili ya mabadiliko ya kijamii na kisiasa ambayo yaanzie kwa vijana? Kwa nini wasishirikishane utajiri wa mafunzo ya kijamii ya Kanisa?

Ukutani ni kitambaa kilichokusanywa vipande vipande kutoka kila familia ya wanafunzi wa shule
Ukutani ni kitambaa kilichokusanywa vipande vipande kutoka kila familia ya wanafunzi wa shule

Baba Mtakatifu amebanisha kuwa inawezakana kutazamia sehemu za kukabiliana na za majadiliano ambayo yasaidie nguvu kazi kwa ajili ya wema wa pamoja. Ikiwa mchakato wa kisinodi umetupatia mazoezi ya mang’amuzi ya kijumuiya, matazamio ya Jubilei ijayo ituone kuwa watendaji, mahujaji wa matumaini, kwa Italia ya kesho. Kutoka kwa mitume wa fufuko tusiache kamwe kumwilishwa na imani, hakika kwamba wakati huko juu ya nafasi na kwamba kuanzisha mchakato ni busara zaidi ya kushika nafasi. Hii ndiyo jukumu la Kanisa: kujihusisha katika matumaini kwa sababu bila hiyo inawezekana kusimamia ya sasa lakini yajayo hayajengwi. Papa amewashukuru kwa jitihada zao. Amewabariki na kuwatakia kuwa mafundi wa demokrasia na mashuhuda wanaoambukiza ushiriki. Na amewaomba wasali kwa ajili yake.

Papa ametoa hotuba ya kwanza Trieste
07 July 2024, 10:10