Papa Francisko:Ushirika na unyofu ni tunu muhimu kwa Kanisa la kweli la kimisionari

Injili haitangazwi peke yake,ni lazima turidhike na kile ambacho ni muhimu kwa sababu ni rahisi kusonga mbele pamoja.Hizi ndizo dhana mbili za Papa kabla ya sala ya Malaika wa Bwana alikazia kufuatia kifungu cha Injili ya siku:Wivu ni kitu cha kuua.Ni sumu!hewa nzito,maisha yanakuwa magumu na mikutano inakuwa nafasi ya wasiwasi,huzuni na kuvunjika moyo kuliko fursa ya furaha.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa tafakari yake Dominika 14 Juali 2024 kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana kwa Waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, ameanza kusema kuwa: “Injili ya leo inamzungumzia Yesu anayewatuma wafuasi wake katika utume(Mk 6,7-13).” Akiendelea amsisitiza kuwa “Anawatuma wawili wawili na kuwaonya wapeleke kile kilicho muhimu tu. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu ameomba kuzungumza kidogo juu ya picha hiyo: “mitume waliotumwa pamoja na wanapaswa kupeleka yaliyo ya muhimu tu.” Injili haitangazwi tu, lakini ni pamoja na kama jumuiya na ili kufanya ni lazima kujua namna ya kutunza unyofu (sobrieta) yaani kujua namna ya kutumia mambo kwa kiasi, kwa kushirikishana rasilimali, uwezo na zawadi na kuwa makini kwa zawadi zaidi, ili kuwa huru, na kwa sababu wote tuweze kuwa na kile kinachohitajika kuishi, kwa namna ya hadhi na kuchangia kwa uhai wote utume; na baadaye kuwa na unyofu katika mawazo na katika hisia kwa kuachana na maono ya kijujuu, dhana na ugumu ambao, kama mizigo isiyo na maana, inayoelemea na kusukana katika safari, na kunyume chake ili kusaidia na makabiliano na kusikiliza na kuwa namna ya dhati ya kushuhudia.

Papa wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana
Papa wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba, tufikirie kwa mfano, ni nini kinatokea katika familia zetu au katika jumuiya zetu: tunaporidhika na kile kilicho cha lazima, hata kile kidogo, kwa msaada wa Mungu tunafanikiwa kwenda mbele na kupatana, kwa kushirishana kile ambacho kipo,  kwa kujikatalia yote  ili kusaidia wengine (Mdo 4,32-35). Na hiyo tayari ni tangazo la kwanza la umisionari, na zaidi kabla ya maneno, kwa sababu linajimwilisha kwa uzuri wa ujumbe wa Yesu katika uthabiti wa Maisha. Katika familia au katika jumuiya ambayo wanayoishi kwa namna hiyo kiukweli katika mzunguko wao wanajiandalia mazingira tajiri ya upendo, ambao ni rahisi zaidi kujifungulia Imani na mapya ya Injili na ambayo yaananza na ubora ndani mwake na wana utulivu zaidi. Kinyume iwapo kila mmoja anakwenda peke yake, ikiwa kile kinachotazamwa ni vitu  tu, na ambavyo huwa havitoshi kamwe, na ikiwa hatusikilizani, na ikiwa kinachotawala ni ubinafsi, na wivu, hali inakuwa nzito, Maisha magumu na mikutano inakuwa fursa ya wasiwasi, huzuni na kukata tamaa badala ya furaha (Mt 19,22).

Waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwa Sala ya Malaika wa Bwana
Waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwa Sala ya Malaika wa Bwana

Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo alisema usirika na kiasi/unyofu ni maadili muhimu kwa ajili ya Maisha yetu ya kikristo na kwa ajili ya utume wetu, thamani ambazo ni muhimu kwa ajili ya Kanisa la kweli la kimisionari, kwa nyanja zote. Kwa njia hiyo: “Tujiuliza, je mimi ninahisi ladha ya kutangaza Injili, ya kuipeleka mahali ambapo ninaishi, furaha na nuru ambayo inakuja kutokana na kukutana na Bwana? Ili kufanya hivyo, je ninaweka juhudi ya kutembea pamoja na wengine nikishirikishana nao mawazo na uwezo kwa akili iliyo wazi na moyo wa ukarimu? Na hatimaye, Je ninajua kukuza mtindo mmoja wa Maisha ya kiasi na kuwa makini kwa mahitaji ya ndugu? Maria Malkia wa Mitume, atusaidie kuwa mtume wamisionari wa kweli, katika ushirika, katika maelewano kati yetu na katika unyofu wa maisha.

Tafakari ya Papa Angelus
14 July 2024, 14:48