Papa kwa watawa:andikeni kurasa za ajabu za upendo,ubunifu,ujasiri na unabii
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 15 Julai 2024, amekutana na washiriki wa Mikutano mikuu ya Mashirika 6 kitawa ambapo kwanza kuwauliza swali wana manovisi wa kike na kiume wangapi? Walijibu lakini bila kuleweka na kusema kuwa watakufa bila kuwa na wafuasi hivyo wasali. Wengine walijibu ishirini,na akawauliza kwamba wanafanyaje, na kwamba wanatoka wapi, walijibu wanatoka Asia, Afrika na Amerika Kusini, Baba Mtakatifu alisema huko ndiko kuliko na uhai kweli. Kwa njia hiyo wanapaswa waongezze miito na kwamba anapenda kuuliza hilo kwa sababu ya wakati ujao wa mashirika yao. Baba Mtakatifu akianza hotuba yake kwa washiriki hao alisema wanawakilisha taasisi na mashirika mbali mbali ya waazilishi tofauti ambao asili yao ni ya karne ya 16 na 20. (Shirika la Watawa wadogo, Mpadre na wabrudia Wadogo wa Kawaida, Masista Waagostiniani wa Upendo wa Mungu, Mapadre wa Mtakatifu Viatore, Masista wa Reparators wa Moyo Mtakatifu na Wamisionari wa Mtakatifu Anthoni Maria Claret.
Katika utofauti huo, wao ni taswira hai ya fumbo la Kanisa, ambamo: “Kila mmoja hupewa ufunuo wa pekee wa Roho Mtakatifu kwa faida ya wote”(Rej.1Kor 12:7), ili kuakisi katika utukufu wake wote duniani. Si kwa bahati mbaya kwamba Mababa wa Kanisa walifafanua njia ya kiroho ya wanaume na wanawake waliowekwa wakfu: kama “philokalia,” yaani, upendo kwa uzuri wa Mungu, ambao ni mionzi ya wema wa kimungu(Mtakatifu Yohane Paulo II Hati ya Kitume ya Maisha ya wakfu 19). Na katika barabara hiyo, ni umbali gani na mapambano gani ya ndani ambayo mara nyingi hujitokeza? wakati mwingine kutokana na masilahi mengine yasiyokuwa ya upendo. Kwa hiyo Papa amependa kusimama na kutafakari na wao juu ya vipengele viwili vya maisha yao ambavyo vinahusiana sana na haya yote:(bellezza e la semplicità) yaani uzuri na urahisi. Kwanza: uzuri.
Baba Mtakatifu amesema: “Kwa hakika historia zao, katika hali, nyakati na mahali mbalimbali, ni historia za uzuri, kwa sababu ndani yake neema ya uso wa Mungu hung’aa: ile ambayo katika Injili tunaiona ndani ya Yesu, mikononi mwake iliyokusanyika katika maombi katika nyakati za urafiki na Mungu. Baba (taz. Mt. 14:23), moyoni mwake akiwa amejaa huruma (rej.Mk 6:34-44), machoni pake akiwa na bidii anapokemea udhalimu na unyanyasaji(rej. Mt. 23:13-33), katika miguu yake iliyotiwa alama kwa matembezi marefu ambayo kwayo alifika hata kwenye viunga vya nchi yake vilivyokuwa na hali mbaya zaidi na vilivyotengwa (rej. Mt 9:35).”
Waanzilishi wao wa kike na kiume, chini ya msukumo wa Roho Mtakatifu, waliweza kufahamu sifa za uzuri huu, na kuitikia kwa njia tofauti, kulingana na mahitaji ya nyakati zao, kuandika kurasa za ajabu za upendo halisi, ujasiri, ubunifu na unabii, wakijikita katika kuwatunza walio dhaifu, wagonjwa, wazee na watoto, katika majiundo ya vijana, katika utangazaji wa kimisionari na katika kujitolea kijamii; kurasa ambazo wamekabidhiwa leo, ili waweze kuendeleza kazi waliyoianza. Mwaliko, basi, kutoka kwa Papa katika kazi zao za sura hizi ni “kuchukua ushuhuda wao, na kusonga mbele, kuendeleza, kama wao, kutafuta na kupanda uzuri wa Kristo katika ukamilifu wa safu za historia, wakijiweka kwanza juu ya yote na kila kitu kusikiliza Upendo uliowahuisha, kisha kukuacha wahoji njia walizojibu: kwa kile walichochagua na kwa kile walichokataa, labda kwa mateso, kuwa kioo wazi cha uso wa Mungu kwa watu wa wakati wao.
Katika hayo yote ndiyo Baba Mtakatifu amesema inazaa neno la pili ambalo ni urahisi. Kila mmoja wao, katika hali tofauti, Papa amesema alichagua umuhimu - waliachana na yale yasiyo ya kawaida, wakajiruhus kuumbwa siku baada ya siku na usahili wa upendo wa Mungu unaong'aa katika Injili. Ndiyo, kwa sababu upendo wa Mungu ni rahisi na uzuri wake ni rahisi, si uzuri wa kisasa, la hasha. Ni rahisi kutumia. Kwa njia hiyo wanapojiandaa kwa ajili ya mikutano yao kwa hiyo, wao pia wamwombe Bwana kuwa sahili, binafsi na pia sahili katika mienendo ya kisinodi ya safari ya kawaida, wakijivua kila kitu ambacho hakihitajiki au kinachoweza kuzuia usikilizaji na makubaliano katika mchakato wao wa utambuzi; wakivua mahesabu, tamaa , lakini wivu, ambapo Papa amekazia kuonya kwamba “ni pigo katika maisha ya kuwekwa wakfu; wawe makini na hilo: “ni pigo la wivu ambapo ni mbaya katika maisha ya Jumuiya.” Papa amefafanua neno “wivu” kama “ugonjwa wa manjano” ni jambo baya, madai, ugumu na majaribu yoyote mabaya ya kujirejea.
Kwa hivyo Papa amesema wataweza kujifunza pamoja, kwa hekima, wakati uliopo, kufahamu “ishara za nyakati” (Katiba ya Kichungaji Gaudium et spes, 4) na kufanya maamuzi bora zaidi kwa siku zijazo.” Kama wanaume na wanawake watawa zaidi ya hayo, wanakumbatia umaskini kwa usahihi ili kujiondoa wenyewe kutoka katika kila kitu ambacho si upendo wa Kristo na kujiruhusu wajazwe na uzuri wake, hadi kufurika ulimwenguni (rej. Waraka wa Laudato si', Sala kwa ajili ya nyumba yetu), na hivyo popote pale ambapo Bwana anawatuma wao na kuelekea kwa kila kaka au dada wanaowekwa kwenye njia zao, hasa kwa njia ya utii.
Papa Francisko amekazia kusema: “na hii ni utume mkubwa! Na Baba anawakabidhi wao, wajumbe dhaifu wa mwili wa Mwanae, kwa usahihi ili kupitia ile Ndiyo yao ya unyenyekevu, nguvu ya huruma yake ionekane, ambayo inapita zaidi ya uwezekano wote, na ambayo inaingia katika historia ya kila moja ya jumuiya zao. Baba Mtakatifu amewasihi wasiacha Sala, na ni sala itokayo moyoni; wasiondoke tu mbele ya hema wakizungumza na Bwana, na kumruhusu Bwana aseme nao. Lakini sala kutoka moyoni, sio kama ya kasuku hapana, bali iwe ile inayotoka moyoni na inayotufanya tusonge mbele katika njia ya Bwana. Papa Francisko kwa Kaka na dada hao watawa, amewashukuru kwa wema mkuu wanaofanya katika Kanisa, katika sehemu nyingi za ulimwengu, na amewatia moyo kuendelea na kazi yao kwa imani na ukarimu! Papa amewaomba waombee miito. Ni muhimu kuwa na warithi ambao wanaendeleza karama. Amehimiza waombe sana na kuwa makini katika mafunzo na kuwatakia mema. Amewabariki na kuwaomba tafadhali waombe kwa ajili yake.