Papa akumbuka miaka 30 ya shambulio la Amia:amani itawale juu ya chuki na migawanyiko
Vatican News.
Katika Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko uliotolewa wakati wa kuadhimisha miaka 30 ya shambulio dhidi ya makao makuu ya Amia ya Wanachama wa Israeli wa Argentina(Argentina Israelte Mutual Association)huko Buenos Aires amebainisha kuwa:"Fanyeni kazi bila kuchoka kwa ajili ya ulimwengu wa kidugu zaidi, ambapo haki na amani vinakumbatiana, kwa sababu bila haki hakutakuwa na amani ya kudumu na yenye matokeo. Maadhimisho hayo yaliadhimishwa, Alhamisi tarehe 18 Julai 2024 katika nchi ya Amerika ya Kusini. Hii ni kumbukizi ya siku hiyo hiyo ambapo mnamo mwaka 1994, kiukweli, ilikuwa saa 3:53 za asubuhi, ambapo gari lililokuwa limebeba mabomu lililipuka katika maegesho ya magari ya jengo mahali ambapo Ofisi za Amia zilikuwa. Jengo hilo liliporomoka na kusababisha vifo vya watu 85 na majeruhi zaidi ya 300. Shambulizi hilo liliingia katika historia kama shambulio baya zaidi kuwahi kufanywa nchini Argentina.
Songa mbele kwa ujasiri
Katika muktadha wa amri ya maombolezo ya kitaifa nchini, ujumbe wa Baba Mtakatifu umehimiza juu ya tafakari na sala, kwa ajili ya kuwakumbuka wahanga wa janga hilo la giza na kutoa mwaliko wa kudumisha dhamira ya kudumu ya haki. “Tunachagua ukimya unaoeleweka sio kama utupu, lakini kama uwepo unaoonekana wa wale ambao hawapo tena. Kwa hakika, ukimya ni maombolezo na matumaini na huturuhusu kuhisi mwangwi wa maisha kupunguzwa na uzito wa kutokuwepo, na nguvu ya kukabiliana na ukweli wa uovu na uthabiti wa kusonga mbele,” Papa ameandika.
Kamwe vitendo hivyo vya unyanyasaji visirudie
Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amehimiza kutazama kumbukumbu hiyo kama mwongozo wetu, ambao ni, “kama chombo cha kukumbuka yaliyopita na kujionesha kwa matumaini kuelekea siku zijazo ambapo vitendo hivyo vya unyanyasaji visirudiwi tena.” Kwa mtazamo huo, ombi la Papa Fransisko ni thabiti la “kutokukata tamaa katika kutafuta haki, kueleweka na si kulipiza kisasi au kinyongo, bali kama ukweli na malipizi”. Kipengele muhimu kwa familia za waathiriwa na kwa mshikamano wa mfumo wa kijamii wa kitaifa, “haki inahusisha, kwa hakika, heshima kwa kila maisha ya binadamu na utu na kwa hivyo lazima itawale juu ya chuki na migawanyiko.” Wito wa Papa anabainisha kuwa “Huu ndio msingi wa kujenga wema wa wote sio tu kuwaheshimu wale ambao tumepoteza, lakini pia kulinda vizazi vijavyo.”
Maombi kwa ajili ya waathirika na walionusurika
Hatimaye, Baba Mtakatifu amewaalika “watu wote wa imani na wote wenye mapenzi mema kuungana katika sala na matendo”, huku Papa akisali kwa ajili ya familia zote ambazo bado zinaomboleza wapendwa wao na wale wote waliosalia na kuwaombea faraja ya Mungu wa amani”.