Tafuta

Papa amewaandikia vijana wa Amerika Kusini na visiwa vyake kwamba wasiwe na hofu ya Mungu kuingia katika maisha yao. Papa amewaandikia vijana wa Amerika Kusini na visiwa vyake kwamba wasiwe na hofu ya Mungu kuingia katika maisha yao.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa vijana:acheni Kristo abadilishe matumaini ya asili kuwa upendo wa kweli

Papa Francisko ametuma ujumbe katika fursa ya Mkutano wa XXI wa wahusika kichungaji wa vijana kitaifa,barani Amerika Kusini na visiwa vya Caribbien,kuanzia tarehe 15-20 Julai 2024.Kuhusu mada,Papa anasema:kuamka tena hakumaanishi wajibu wa vizazi vipya tu,bali hata nia ya Kristo kuwaona vijana wanakuwa wapya na nguvu za kuishi maisha ya hadhi.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Papa Francisko ametuma ujumbe wake katika hafla ya Mkutano wa XXI wa Viongozi kitaifa wa Vijana kichungaji  wa Baraza la Maaskofu Katoliki barani Amerika ya Kusini na Visiwa vya Caribbean (ELARNPJ) ambao unaendelea huko Asunción, nchini Paraguay, tangu tarehe 15 hadi 20 Julai 2024.  Barua hiyo  imetumwa kwa Askofu Pierre Jubinville, mkuu wa huduma ya Kichungaji ya vijana huko  Paraguay, na ujumbe mfupi moja kwa moja kwa vijana waliopo katika mji mkuu wa nchi ya Amerika ya Kusini, barua mbili zikiwa katika lugha ya Kihispania.

‘Kijana inuka’

Mada ya inayoongoza mkutano huo ni: “Kijana, nakuambia, inuka!”, iliyotolewa katika usemi unaojulikana sana wa Injili ya Luka ambapo Yesu alimfufua mwana wa mjane wa Naini. Baba Mtakatifu katika ujumbe huo anabainisha: “ Ujana ni awamu ya maisha ambayo kawaida huoneshwa na matumaini ya asili, nguvu na matumaini. Hebu Kristo abadilishe matumaini yenu ya asili kuwa upendo wa kweli, upendo unaojua jinsi ya kujitolea, ambao ni wa dhati, na kweli na hivyo ujana wenu utakuwa zawadi kwa Yesu na kwa ulimwengu.”

Msiogope kumruhusu Kristo aingie katika maisha yenu

Katika barua aliyomtumia Askofu huyo, Baba Mtakatifu anatoa tafakari ya kina juu ya vijana kama zawadi ya kutoa kwa Bwana. Kuhusu mada ya mkutano,  Papa ameakisi jinsi ambavyo mwaliko wa 'kuamka tena' haumaanishi wajibu wa vizazi vipya tu, bali pia nia ya Kristo ya kuwaona vijana wakijipyaisha, waliojawa na nguvu za kuishi maisha yenye heshima na ukamilifu, kufanikiwa, kwa vitendo vya maisha mapya katika ushirika naye. Papa aidha anawaalika vijana wasiwe na hofu kuwa: "Msiogope Bwana anayepita karibu nasi na kutunong'oneza masikioni mwetu, akiinama kuelekea kwetu na kutupatia mkono wake ili kutuinua kila tunapoanguka, anatutaka  tusimame na kufufuliwa. Msiogope kumruhusu aingie katika maisha yenu," Amekazia Papa.

Wahusika wakuu wa Sinodi na Kanisa la kimisionari

Katika Ujumbe huo, aidha Papa amewahimiza vijana  pamoja na watoto, watu wazima na wazee, ili kuwa katika ushirika wa vizazi na waweze kuwa wahusika wakuu wa Kanisa linalozidi kuongezeka la kisinodi, kuwa  wanafunzi na wamisionari". Kwa njia hiyo amehitimisha kwa kushukuru tena vijana wa Paraguay kwa kufanya kazi ya kujitolea kuandaa mkutano huo huko Asunción, huku wakiombea maombi kwa ajili ya huduma yao ya kichungaji. Vile vile, Papa amepongeza mbinu iliyopendekezwa kwa kazi hiyo na kuwahimiza washiriki, daima kutafuta umoja kati ya tofauti ili kuimarisha imani na ushuhuda wa Kikristo katika uanachama wa jumuiya zao.

Papa alituma ujumbe kwa vijana wa Amerika Kusini
17 July 2024, 16:03