2023.08.02 Partecipazione dei giovani armeni cattolici alla GMG di Lisbona

Papa awaandikia vijana wa Romania:tumieni mitandao ya kijamii na sambazeni maadili

Papa Francisko alijibu barua kutoka kwa washiriki wa mkutano wa kijimbo akiwaalika vijana kusambaza maadili yanayojenga kwenyemitandao yao ya kijamii kwa ujasiri na ubunifu,huku wakiepuka kuwa watumwa wa simu za mikononi.“Nenda ulimwenguni,mkawatazame kaka na dada zenu machoni.”

Vatican News

“Kuweni wabeba matumaini na wajenzi wa madaraja, mkitumia kila chombo kinachopatikana ili kupanda wema na upendo ulimwenguni.” Ni maneno ya  Baba Mtakatifu Francisko aliwaandikia  vijana wa Romania wa jimbo la Iasi, akijibu barua yao iliyotumwa katikati ya mwezi Mei mwaka huu kupitia kwa Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican ambaye  alishiriki katika mkutano wa vijana wa Jimbo huko Iasi mnamo  tarehe 18 na 19 Mei 2024 ulioandaliwa  na Askofu Iosif Păuleț.

Tumieni mitando ya kijamii kwa ujasiri na ubunifu mkisambaza maadili

Katika ujumbe wake, Baba Mtakatifu  aliwahimiza vijana kutumia mitandao ya kijamii “kwa ujasiri na ubunifu, kusambaza maadili ambayo yanajenga: urafiki, amani, mazungumzo kati ya makabila na tamaduni, familia na maadili ya Kikristo.” Na aliwasihi wajilinde dhidi ya kuwa watumwa wa simu za mikononi na kutoka katika kukwama kwa kujitenga katika maisha ya kawaida, kwa madhara ya maisha  yao ya kweli.

Utajiri wa kweli upo katika mahusiano ya moja kwa moja na ya dhati

“Nendeni ulimwenguni, kutana na watu, sikilizeni historia zao, tazameni kaka na dada zenu machoni. Utajiri wa kweli upo katika uhusiano wa kibinadamu unaopatikana kila siku, kwa mawasiliano ya moja kwa moja na ya dhati,” alibainisha Papa. Na zaidi ya hayo Baba Mtakatifu aliwaalika kushiriki katika mkutano wa vijana wa kitaifa, utakaofanyika mwezi Septemba katika Jimbo la Brasov. “Itakuwa fursa ya thamani kukua pamoja katika imani, kushiriki uzoefu na kuimarisha njia zenu katika Kikristo.” Na hatimaye aliandika Papa Francisko kuwa “Msisahau kuniombea,” kwani Msaada wenu wa kiroho ni zawadi isiyokadirika ambayo inanisaidia kutumikia Kanisa na ubinadamu.”

Papa awaandikia vijana wa Romania
06 July 2024, 09:05