Tafuta

2024.07.02 Papa alikutana na kundi la Wahamiaji katika nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican. 2024.07.02 Papa alikutana na kundi la Wahamiaji katika nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican.  

Papa na kundi la wahamiaji:Yeye ni kama Baba wa sisi sote!

Papa alikutana na Wahamiaji wawili wa Senegal na Gambia katika Nyumba ya Mtakatifu Marta,waandishi wa vitabu vinavyo simulia matukio waliyokumbana nayo katika utafutaji wa maisha mapya.Aliyewasindikiza ni Padre Mattia Ferrari,Msimamizi wa Kikanisa wa Shirika la Huduma ya kibinadamu ya Mediterania.

Vatican News.

Padre Mattia Ferrari amesimulia Jumanne tarehe 2 Julai 2024 kwa vyombo vya habari, kila ambacho kilitokea mapema huko Mtakatifu Marta mahali ambapo kwa mara nyingine tena alisindikiza kikundi cha wahamiaji wanaopenda kumfahamu Papa Francisko. Kwa njia hiyo alisema hii siyo kwa mara ya kwanza kufanya mkutano kwa namna hii. Na kila mara nikurudia kusema  kuwa ni wakati mkubwa wa neema, kwani kukutana na Papa zaidi ya hayo kwao ni baba, kwa sababu ndivyo wanavyohisi,”alisisitiza Padre Mattia. Wote bila ubaguzi katika hali zao za watu wasio na ardhi, Wakatoliki na Waislamu, ni mchungaji wa wote.”

Historia kati ya kuzimu na matumaini

Wahusika wakuu wa mkutano huu wakati huu walikuwa vijana wawili, Ibrahim Lo, walitoka Senegal na kupitia njia ya Libya, njia hiyo hiyo ya kushangaza na Ebrima Kuyateh, wa Gambia. Na kwa wote wawili wameandika vitabu, hasa Ibrahim, kimoja kiitwacho: “Mkate na Maji. Kutoka Senegal hadi Italia kupitia Libya na ya cha pili ni “Sauti yangu.  Kutoka pwani ya Afrika hadi mitaa ya Ulaya.” Historia nyingine yenye ladha kama hiyo ni ile ya Ebrimam yenye: kichwa: “Nina miguu yangu wazi, na dibaji, pamoja na mambo mengine, ya askofu mkuu Erio Castellucci, askofu  Mkuu wa Carpi, Modena na Nonantola na na pia maneno ya baadaye ya Stefano Croci, mkurugenzi wa Wahamiaji. Pia katika mkutano na Papa walikuwepo Padre  Mattia Ferrari, Stefano Croci, mkurugenzi wa Migrantes Carpi, Giulia Bassoli, mfanyakazi wa kujitolea wa sehemu hiyo hiyo, na Luca Casarini, mwanzilishi wa  utume wa Mediterranea Saving Humans na mgeni maalum wa Sinodi ya Maaskofu. Pia pamoja nao alikuwa ni Sr Adriana Dominici, wa harakati ya kikanisa ya Spin Time Labs jijini Roma.

Kukumbatiana upya na Pato

Padre  Mattia alisema kuwa Papa Francisko, alitaka kusikiliza historia  zao "na alimshukuru kila mtu kwa kile anachofanya na kile anachoishi na kuwatia moyo kusonga mbele. Kando ya kijana huyo kutoka Senegal na Gambia pia alikuwapo Pato, ambaye tayari alikutana na Papa mnamo Novemba 2023  yeye akiwa ni mume wa Fati na baba ya Marie, mama na msichana mdogo waliokufa kwa kiu jangwani mwaka 2023, ambao kiukweli walikufa kama onyo kwa dhamiri katika kumbatio lao la mwisho na la kuvunja moyo ambaoi taarifa zao zililozunguka ulimwengu mzima. Kwa njia hiyo historia za kuzimu lakini pia za matumaini, ambazo kila mtu alitaka kuzikabidhi mikononi mwa PapaFrancisko. Yale yote yaliyojionesha ya kutia ndani ukaribisho kutoka katika vijana hao, yanaonesha  jinsi ulivyo ukweli wa uzoefu unaopatikana baharini na nchi kavu, yaani, tunaposaidia au kuwakaribisha maskini, wahamiaji, wanawasaidia,  ndio wanaotusaidia na kuokoa. Na katika upendo, katika udugu unaoishi na maskini, na wahamiaji, wokovu ni uzoefu,” Padre Mattia alisema.

Papa alikutana na wahamiaji

 

03 July 2024, 15:36