Tafuta

2024.06.25 Nembo ya Ziara ya Papa huko Ubelgiji na Luxembourg. 2024.06.25 Nembo ya Ziara ya Papa huko Ubelgiji na Luxembourg. 

Papa nchini Ubelgiji na Luxembourg:ratiba rasmi imechapishwa!

Papa Francisko atasafiri katika nchi hizo mbili za Ulaya kuanzia tarehe 26 hadi 29 Septemba 2024.Mikutano na mapadre,vijana na mamlaka imepangwa.Kwa Brussels kutembelea Mfalme wa Ubelgiji na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha kale cha Louvain

Vatican News

Mikutano mingi na  mipango itaadhimisha siku nne za ziara ya kitume ambayo Baba Mtakatifu Francisko ataifanya huko Ubelgiji na Luxembourg kuanzia tarehe 26 hadi 29 Septemba 2024. Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican imetangaza Ijumaa tarehe 19 Julai 2024  mpango rasmi wa safari ya kimataifa ya Papa.

Kuwasili  Luxembourg

Kituo cha kwanza kitakuwa Luxembourg ambapo Papa atawasili asubuhi ya Alhamisi tarehe 26 Septemba 2024, baada ya safari ya saa mbili kwa ndege. Kuondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rome-Fiumicino kumepangwa saa 2.05asubuhi; na saa 4.00 asubuhi, ndege ya Papa itatua katika Uwanja wa Ndege wa Findel, Luxembourg ambapo sherehe ya kuwakaribisha wageni itafanyika. Saa 4.45 atafanya ziara ya heshima kwa Mfalme wa Luxembourg katika Jumba la Kifalme, ikifuatiwa na mkutano na waziri mkuu saa 5.15 na, saa 5.50, na viongozi, mashirika ya kiraia na mashirika ya kidiplomasia katika Ukumbe wa Mji. Papa  Francisko atatoa hotuba yake ya kwanza huko.

Mkutano na jumuiya ya Kikatoliki na kuelekea Brussels

Baba Mtakatifu atatoa hotuba ya pili mchana, saa kumi na nusu jioni, kwa Jumuiya ya Wakatoliki ambayo ataiona katika Kanisa Kuu la Notre-Dame yaani Mama Yetu huko Luxembourg. Na kufuatia  kundoka saa 5.45 jioni kwa sherehe ya kuaga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Findel - Luxembourg. Kuondoka kuelekea Bruxels saa 12.15 jioni. Itawasili katika mji mkuu wa Ubelgiji saa 1.10 jioni, ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Melsbroek, ambapo sherehe ya kuwakaribisha itafanyika.

Mkutano na Mfalme wa Ubelgiji, kisha na mamlaka na maprofesa wa Chuo Kikuu cha Louvain

Siku ya pili ya Ziara, Ijumaa tarehe  27 Septemba 2024, itafunguliwa saa 3.15 asubuhi kwa ziara ya heshima kwa Mfalme wa Ubelgiji katika Ngome ya Laeken. Hii itafuatiwa saa 3.45 asubuhi na mkutano na Waziri mkuu na, saa 4.00, na mkutano na mamlaka na mashirika ya kiraia. Hotuba ya Papa inatarajiwa katika hafla hiyo. Alasiri, saa 10.30 jioni, Papa Francisko atakutanana maprofesa wa Vyuo vikuu katika Chuo Kikuu Katoliki cha Louvain, mojawapo ya vyuo vikuu vya kale zaidi barani Ulaya, ambacho mnamo mwaka 2025 kinaadhimisha miaka 600 tangu kuanzishwa kwake. Hotuba pia imepangwa katika hafla hii.

Kuzungumza na mapadre na vijana

Siku ya Jumamosi tarehe 28 Septemba 2024 itakuwa ni kwa ajili ya mkutano na maaskofu, mapadre, mashemasi, wanaume na wanawake waliowekwa wakfu, waseminari na wahudumu wa kichungaji katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu la Koekelberg. Papa atawahutubia pia. Mkutano huo utafanyika saa 4:30 asubuhi, baada ya hapo, kutakuwa na mipango mingine na wanafunzi wa chuo kikuu katika Ukumbi Mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki Louvain-La-Neuve; hotuba pia imepangwa hapa. Hatimaye, kama kawaida katika safari zote za kitume, atakuwa na mkutano wa faragha na washiriki wa Shirika la Yesu (Wajesuit) katika Chuo cha Mtakatifu Michel.

Misa ya mwisho

Safari nzima itakamilika Dominika tarehe 29 Septemba 2024 na Misa saa 4.00 asubuhi katika uwanja wa "King Baudouin". Baba Mtakatifu atatoa mahubiri yake  na kusali Sala ya Malaika wa Bwana pamoja na waamini watakao kuwepo. Kisha, saa 6.15 mchana atahamia Melsbroek Uwanja wa ndege kwa sherehe ya kuaga, iliyopangwa saa 12.15 mchana. Kuondoka kuelekea Roma saa 6.45 mchana, ambako imepangwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rome/Fiumicino kuanzia saa 8.55 alasiri.

20 July 2024, 13:37