Tafuta

Papa anaandika kuwa:Pete tano zilizounganishwa zinawakilisha roho ya udugu ambayo lazima iwe sifa ya tukio la Olimpiki na mashindano ya michezo kwa ujumla. Papa anaandika kuwa:Pete tano zilizounganishwa zinawakilisha roho ya udugu ambayo lazima iwe sifa ya tukio la Olimpiki na mashindano ya michezo kwa ujumla. 

Ujumbe wa Papa kwa matazamio ya Michezo ya Olimpiki jijini Paris!

Michezo ni lugha ya kimataifa inayovuka mipaka,lugha,rangi,mataifa na dini;ina uwezo wa kuunganisha watu,kuhimiza mazungumzo na kukubalika kwa pande zote; huchochea kujishinda, hufundisha roho ya dhabihu,inakuza uaminifu katika mahusiano ya kibinafsi;inatualika kutambua mipaka yetu wenyewe na thamani ya wengine.Ni katika Ujumbe wa Papa aliotuma katika matazamio ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki kuanzia tarehe 26 Julai hadi 8 Septemba.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tarehe 19 Julai 2024, asubuhi saa 4.00 katika Kanisa la Madeleine jiji Paris, imeadhimishwa Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuomba amani katika siku ambayo inazinduliwa kwa michuano ya Olimpiki ya Michezo ya Paris, iliyopendekezwa na Baraza la Maaskofu wa Ufaransa, Jimbo Kuu katoliki la Paris na timu ya Michezo. Maadhimisho haya yaliongozwa na Askofu mkuu Celestino Migliore, Balozi wa Kitume nchini Ufaransa kwa kushirikiana na Askofu Mkuu Laurent Ulrich, wa Jimbo Kuu la Paris, na  Askofu Emmanuel Gobilliard, wa Digne, mjumbe wa Baraza la Maaskofu wa Ufaransa kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki na Walemavu. Thomas Bach, rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, wanadiplomasia na wahusika wakuu wa michezo walikuwepo. Michuano ya Olimpiki, iliyopigiwa kura na Umoja wa Mataifa, huanza Juma moja kabla ya sherehe za ufunguzi rasmini wa Michezo zitakazoanza tarehe 26 Julai  na kumalizika Juma moja baada ya kumalizika kwa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu mnamo tarehe 8 Septemba.

Jumuiya zinajitayarisha kufungua milango na mioyo 

Katika fursa hiyo Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wa matashi mema kwa Askofu Mkuu Laurent Ulrich wa Jimbo Kuu la Paris. Papa anaungana na nia yake ya Misa wanayoadhimisha, kwa kuzingatia Michezo ya Olimpiki itakayofanyika hivi karibuni katika jiji lake. Anamwomba Bwana awajaze karama zake wale wote watakaoshiriki kwa njia moja au nyingine, Yeye, wanariadha au watazamaji  na pia kuunga mkono na kuwabariki wale wanaowakaribisha, hasa waamini wa Paris na maeneo mengine. “Ninajua, kwa hakika, kwamba jumuiya za Kikristo zinajitayarisha kufungua milango ya makanisa yao, shule zao, nyumba zao. Zaidi ya yote, na wafungue milango ya mioyo yao, wakishuhudia, kwa ukarimu na uchangamfu  wa kuwakaribisha wote, kwa Kristo anayeishi ndani yao na ambaye huwasilisha furaha yake kwao.” Baba Mtakatifu anawashukuru sana kwamba hajawasahau watu walio hatarini zaidi, hasa wale ambao wanajikuta katika hali mbaya sana, na kwamba upatikanaji wa sherehe unafanywa rahisi kwao.

Michezo itakuwa fursa ya maelewano kidugu

Kwa ujumla zaidi, Papa Francisko ameelezea matumaini yake kwamba shirika la Michezo litakuwa fursa nzuri kwa maelewano ya kidugu kwa watu wote wa Ufaransa, kuruhusu, zaidi ya tofauti na migogoro, kuimarisha umoja wa Taifa. Papa anapongeza kwa kufanyika kwa mashindano haya adhimu ya kimataifa ya michezo. Michezo ni lugha ya kimataifa inayovuka mipaka, lugha, rangi, mataifa na dini; ina uwezo wa kuunganisha watu, kuhimiza mazungumzo na kukubalika kwa pande zote; huchochea kujishinda, hufundisha roho ya sadaka, inakuza uaminifu katika mahusiano ya kibinafsi; inatualika kutambua mipaka yetu wenyewe na thamani ya wengine. Michezo ya Olimpiki, ikiwa kweli itabaki michezo, kwa hivyo inaweza kuwa mahali pa kipekee pa kukutana kati ya watu, hata wale wenye uadui zaidi.

Pete tano zilizounganishwa zinawakilisha roho ya udugu

Baba Mtakatifu amekazia kuwa: “Pete tano zilizounganishwa zinawakilisha roho hii ya udugu ambayo lazima iwe sifa ya tukio la Olimpiki na mashindano ya michezo kwa ujumla. Kwa hivyo natumaini kwamba Michezo ya Olimpiki ya Paris itakuwa fursa isiyoweza kukosa kwa wale wote wanaokuja kutoka nchi zote za ulimwengu kujigundua na kujithamini, kuvunja ubaguzi, kutoa heshima pale ambapo kuna dharau na kutoaminiana, urafiki ambapo kuna chuki. Michezo ya Olimpiki, kwa asili, ni kuleta amani na sio vita.”

Katika kipindi cha migogoro Mungu aangazie dhamiri za watawala

Ni katika wa roho hiyo kwamba “mtindo wa kizamani ulikuwa, wa busara, amba ulianzisha makubaliano wakati wa Michezo na kwamba enzi ya kisasa zinajaribu mara kwa mara kuanza tena mila hii ya furaha. Katika kipindi hiki cha misukosuko, ambapo amani ya dunia inatishiwa sana, ni matumaini yangu makubwa kwamba kila mtu atachukua tahadhari kuheshimu mapatano haya kwa matumaini ya utatuzi wa migogoro na kurejea kwa maelewano.  Mungu aturehemu! Aziangazie dhamiri za watawala juu ya majukumu mazito yanayowaelemea, awajaalie mafundi wa amani mafanikio katika mipango yao na awabariki.” Kwa kuwakabidhi Mtakatifu Genevieve na Mtakatifu Denis, wasimamizi wa Paris, na Mama Yetu wa Kupalizwa, Mlinzi wa Ufaransa, kuwa na mafanikio ya Michezo hiyo, Papa kwa moyo wote anawapa Baraka zake kwa Askofu Mkuu, pamoja na wale wote ambao watashiriki.”

Papa atuma ujumbe katika matazamio ya ufunguzi wa Olimpiki, Paris
19 July 2024, 15:27