Papa Francisko Alhamisi tarehe 15 Agosti 2024 ameyaekezeka mawazo yake nchini Ugiriki, ambayo kwa sasa inapambana na moto mkubwa unaotishia maisha, ustawi na maendeleo ya watu wa Mungu nchini Ugiriki. Papa Francisko Alhamisi tarehe 15 Agosti 2024 ameyaekezeka mawazo yake nchini Ugiriki, ambayo kwa sasa inapambana na moto mkubwa unaotishia maisha, ustawi na maendeleo ya watu wa Mungu nchini Ugiriki.   (AFP or licensors)

Athari za Mabadiliko ya Tabianchi Nchini Ugiriki: Janga la Moto

Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Sherehe ya Bikira Maria Kupalizwa mbinguni mwili na roho, Alhamisi tarehe 15 Agosti 2024 kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, ameyaekezeka mawazo yake nchini Ugiriki, ambayo kwa sasa inapambana na moto mkubwa unaotishia maisha, ustawi na maendeleo ya watu wa Mungu nchini Ugiriki. Hiki ni kipindi cha kuoneshana mshikamano wa upendo na udugu wa kibinadamu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Nchi ya Ugiriki ni kati ya nchi ambazo zimeathirika vibaya kutokana na mabadiliko ya tabianchi yaliyosababisha ukame wa kutisha, joto kali vikiambatana na upepo mkali na hivyo kuzua janga la moto kuzunguka mji mkuu wa Athens nchini Ugiriki. Moto huu umesababisha madhara makubwa kwa maisha na makazi ya watu, miundombinu na kwamba, kuna watu kadhaa wamehamishwa kutoka katika miji midogo na vijiji zaidi ya 25, ili kuokoa maisha yao. Hii ni vita ya kupambana na janga la moto ikiongozwa na askari 700 wa Kikosi cha Zima, chenye magari zaidi ya 200 na ndege za kuzimia moto zipatazo 35, lakini moto bado ni mkali sana.

Athari za mabadiliko ya tabianchi wimbi la joto kali
Athari za mabadiliko ya tabianchi wimbi la joto kali

Ni katika muktadha wa janga la moto nchini Ugiriki, Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Sherehe ya Bikira Maria Kupalizwa mbinguni mwili na roho, Alhamisi tarehe 15 Agosti 2024 kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, ameyaekezeka mawazo yake nchini Ugiriki, ambayo kwa sasa inapambana na moto mkubwa unaotishia maisha, ustawi na maendeleo ya watu wa Mungu nchini Ugiriki. Moto huu umeenea sana upande wa Kaskazini Mashariki mwa mji mkuu wa Athens nchini Ugiriki. Tayari baadhi ya watu wamekwisha hamishwa kutoka katika maeneo ya hatari na kwamba, watu wengi wamejikuta hawana tena makazi, baada ya nyumba zao kuungua kwa moto na kwamba, janga hili na moto limesababisha madhara makubwa kwa watu na mazingira ya yao. Baba Mtakatifu Francisko anasema anawakumbuka na kuwaombea waathirika, majeruhi na wale wote waliopoteza maisha yao kutokana na janga la moto nchini Ugiriki. Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, watu wa Mungu watakuwa mstari mbele kuwaonesha mshikamano wa upendo wale wote walioathirika kwa janga la moto nchini Ugiriki.

Janga la Moto
16 August 2024, 15:22