Tafuta

2024.08.24  missione Mediterranea Saving Humans 2024.08.24 missione Mediterranea Saving Humans 

Baraka za Papa kwa Shirika la Kuokoa Binadamu katika utume na Wahamiaji

Ujumbe mfupi kutoka kwa Papa kwa Padre Mattia Ferrari,paroko wa Shirika lisilo la kiserikali,ambaye meli ya Mare Jonio,kwa sasa inajishughulisha na Utume wa SAR kwa kushirikiana na Mfuko wa Baraza la Maaskofu wa Italia(CEI)."Ninawaombea.Asante sana kwa ushuhuda wenu.Bwana awabariki na Mama yetu awalinde."

Na Joseph Tulloch - Trapani

 Katika ujumbe uliotumwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa Padre Mattia Ferrari, paroko wa Parokia ya Huduma ya Shirika la Kibinadamu la Mediterranea,  akiwa ndani ya Bahari ya Ionio, aliandika kuwa: "Mpendwa kaka asante kwa barua pepe yako” pamoja na kutuma baraka zake kwa wafanyakazi wa Huduma hiyo ya kibinadamu na Wahamiaji”. Papa anaandika:  “Ninawaombea, huku akishukuru Shirika hilo lisilo la Kiserikali(NGO)linalohusika katika kuwaokoa wahamiaji, kwa ushuhuda wao na pia kuombea baraka za Mungu na Mama Yetu.”

Ujumbe wa kwanza wa pamoja

Trapani ndiyo mahali pa kuanzia kwa utume wa  SAR yaani (utafutaji na uokoaji) iliyozinduliwa tarehe  23 Agosti 2024 na Mediterranea Saving Humans, yaani  shirika la kibinadamu lililoanzishwa na Luca Casarini ambalo limekuwa likiokoa watu wanaojaribu kuvuka baharini hatari tangu mwaka 2018. Huu ni utume wake wa kwanza kuandaliwa kwa pamoja na Mfuko wa Wahamiaji wa Baraza la Maaskofu wa Italia(CEI). Shukrani kwa uungwaji mkono wa maaskofu, kwa  boti ya kuvuta pumzi iliyotumika tena kwa shughuli za SAR ya Mediterranea  ambayo itaunganishwa na meli ya usaidizi iliyobeba wafanyakazi wengine wa kujitolea na wafanyakazi wa matibabu, pamoja na mpatanishi wa kiutamaduni na kikundi kidogo cha waandishi wa habari.

Waliopo kwenye meli ya utume wa uokoaji
Waliopo kwenye meli ya utume wa uokoaji

Kwa mujibu wa maelezo ya Padre Mattia Ferrari  na wakurugenzi wawili wa Jimbo la kutoka Fano na Caltanissetta kwenye bodi ni kwamba:“ Ni boti ya usaidizi iliyoandaliwa pamoja na Wahamiaji. Hii ni sehemu nyingine ya ushirikiano na Kanisa ambayo imekuwa ikiendelea kwa miaka mingi na ambayo imeundwa juu ya mahusiano mengi na katika ngazi mbalimbali kutoka parokia hadi majimbi , hadi Kanisa la ulimwengu wote.” Ushirikiano, ambao unaona Kanisa na watu wenye mapenzi mema wameungana, kutoka katika ulimwengu mbalimbali wa kijamii na kiutamaduni, wameunganishwa katika upendo wa pamoja kama Injili inavyoonesha, kwa kaka  na dada zetu wahamiaji.” Kwa kusisitiza zaidi Padre huyo alibainisha: “Hii ni safari ambayo inafanywa pamoja, pia kwa njia ya uokoaji baharini na kwa kuokoa watu kutoka kwa ajali ya meli, kutoka kwa kukataliwa, tunatoa mwili kwa udugu wa ulimwengu wote ambao hauwezi kubaki thamani ya kufikirika, lakini lazima ufanyike mwili kwa njia yetu. miili yetu, maisha yetu, mahusiano yetu. Kwenda baharini, kwa hiyo, kunamaanisha pia kuvunja ukuta huu wa simanzi na kutojali, ili kuamsha dhamiri, kwa sababu jamii imekengeushwa sana na hatuwezi kuendelea kuvumilia mauaji haya yanayoendelea ya ajali za meli na kukataliwa. Tunahitaji kuvunja haya yote, sio kuwa washiriki ndani yake,” ndiyo wito wa Padre  Mattia.

Utume unaendelea

Vyombo vya habari vya Vatican navyo vinafuatilia kwenye meli ya Wahamiaji ambayo, pamoja na Meli hiyo kwenye bahari ya Jonio, walisafiri kutoka Trapani. Baada ya kuondoka kwenye maji ya Italia, Mediterranea ilitoa matangazo mawili muhimu. Kwanza, ilisisitiza kuwa kwa kuzingatia ongezeko la unyanyasaji wanaokumba wahamiaji nchini Tunisia, haitashirikiana tena na walinzi wa pwani ya Tunisia katika shughuli za utafutaji na uokoaji. Msimamo ambao tayari umechukuliwa kuelekea Libia, kwa sababu hiyo hiyo; pili, Meli hiyo ya Mediterranea, kwa kuzingatia maagizo ya serikali ya Italia ambayo mara nyingi imeamuru kuteremshwa kwa wahamiaji katika bandari zilizo mbali sana na eneo la uokoaji, imetangaza kwamba haitakubali tena amri za kushuka katika bandari nje ya Sicilia.

Wahusika wa uokoaji wa kibinadamu katika Meli ya uokoaji
Wahusika wa uokoaji wa kibinadamu katika Meli ya uokoaji

Pia kwenye meli hiyo yumo Ibrahimu Lo, mpatanishi wa kiutamaduni kutoka Senegal, ambaye alifika Italia kupitia njia ya Libia, mwandishi wa vitabu viwili vinavyoelezea maafa ya wahamiaji na ambaye, pamoja na Padre Mattia Ferrari na Luca Casarini, walikutana na Papa Francisko katika Nyumba ya Mtakatifu Marta nchini Vatican, tarehe 2 Juali 2024. Kwa mujibu wake alisema: “Niko kwenye meli kwa sababu nilipokuwa na umri wa miaka 16 niliokolewa baharini, nilikuwa kwenye mtumbwi na watu wengine 120. Sasa niko kwenye meli inayokwenda kuokoa maisha, ambayo inarudi mahali nilipookolewa na nitafanya vivyo hivyo na kaka na dada zangu.”

Kuunganishwa na upendo wa ndani

Ingawa huu ni ubia wao rasmi wa kwanza wa pamoja, ushirikiano kati ya Kanisa na Mediterranea ulianza miaka kadhaa nyuma. Papa Francisko mara nyingi amekutana na wanachama wa shirika hilo, akielezea hadharani uungaji mkono wake. Mwaka 2019 aliweka msalaba uliopambwa kwa koti la ukoaji, alilokabidhiwa na Mediterranea, katika Jumba la Kitume la Vatican. Maaskofu wengi wa Italia pia wameeleza kuunga mkono shirika hilo, ambalo linashirikiana kwa karibu na Baraza la Kipapa la kuhamaisha Huduma Fungamani ya Binadamu.

Askofu wa Trapani na Ibrahimu
Askofu wa Trapani na Ibrahimu

Kabla ya kuondoka, Askofu, Pietro Maria Fragnelli, wa Trapani alitembelea meli ya usaidizi ili kutoa baraka zake na kuwapa wafanyakazi Picha  iliyoundwa maalum. “Huu  ​​ni utume wa upendo unaokuja kwetu moja kwa moja kutoka kwa Injili.” Alieleza Askofu. Ujumbe wa leo, kulingana na Askofu, unaonesha ushirikiano ambao unapaswa kuongezeka zaidi na zaidi kati ya vikosi vya kiraia na kijeshi na nani anajua kama utamaduni wetu pia utashinda aina hii ya wazo kwamba Mediterania ni kizuizi na si daraja.” Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa, mwaka 2023 pekee, zaidi ya wahamiaji na wakimbizi elfu 212 walijaribu kuvuka Bahari ya Kati wakianzia Algeria, Libia na Tunisia. Takriban watu elfu tatu walipoteza maisha baharini, takwimu ambayo hakika ilikuwa mbali na ile halisi.

Ujumbe wa Papa kwa wahudumu wa wakimbizi katika bahari Ionio
24 August 2024, 14:18