Tafuta

2024.08.27 Papa Francisko  akisali katika kikanisa kidogo mbele ya kaburi la Mtakatifu Monica katika Basilika ya Mtakatifu Agostino. 2024.08.27 Papa Francisko akisali katika kikanisa kidogo mbele ya kaburi la Mtakatifu Monica katika Basilika ya Mtakatifu Agostino. 

Papa amesali mbele ya masalia ya Mtakatifu Monica katika kumbukizi yake

Baba Mtakatifu Jumanne alasiri tarehe 27 Agosti ameacha mji wa Vatican kwenda katika Kanisa la Mtakatifu Agostino,Roma mahali ambapo yamehifadhiwa masalia ya mama wa Askofu wa Hippo.Katibu Mkuu wa Shirika la Waagostinani alisema:“Monica ana ujumbe sana wa sasa ambapo daima alikuwa mwanamke wa amani."

Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika taarifa kupitia telegram ya Vatican imebanisha kuwa alasiri ya tarehe 27 Agosti 2024 katika Kumbukizi ya Mtakatifu Monica, Mama wa Mtakatifu Agostino wa Hippo, “Baba Mtakatifu Francisko aliacha mji wa Vatican na kwenda katika Basilika ya Mtakatifu Agostino, Roma ambapo alikaa kwa kitambo katika kikanisa kidogo, mahali ambapo kuna masalia ya  Mtakatifu Monica na baadaye mbele ya picha ya Mama wa Wanahija. Wakati wa kutoka aliwasalimia Ndugu Waagostiniani, watawa na wanahija waliokuwapo katika Kanisa na baadaye akarudi mjini Vatican,” taarifa inahitimishwa.

Padre Di Lernia: Papa, ana ibada maalum kwa mtakatifu Monica

Ziara ya ghafla, ni ile ya Papa Francisko katika Basilika ya Mtakatifu Agostino jijini Roma, lakini ambayo sio jambo geni kwake. Tayari mnamo 2018 na 2020, kiukweli, Papa, aliyejitolea sana kwa Mtakatifu Monica kama alivyokuwa mama yake mzazi na alikwenda kwenye kaburi lake siku ya kumbukumbu ya kiliturujia ya  mnamo tarehe 27 Agosti kusali na kutoa heshima kwake. Kwa njia hiyo katika fursa hii tena alikaribishwa na mmoja wa Watawa wa Mtakatifu Agostino  na kutumia dakika chache pamoja naye ambapo pia aliomba aweze kusimama mbele ya Mama Maria wa Wanahija. Ni  picha ya mchoraji Caravaggio, kama  alivyoeleza katibu mkuu wa Shirika la Waagostiniani, Padre Pasquale Di Lernia kwa Vyombo vya habari vya Vatican kati ya wale waliosimama kuzungumza na Papa Francisko.

Kaburi la Mtakatifu Monica katika Basilika ya Mtakatifu Agostino
Kaburi la Mtakatifu Monica katika Basilika ya Mtakatifu Agostino

Padre Pasquale tueleze kuhusu ziara hii ya ghafla ya Papa Francisko kwenye kaburi la Mtakatifu Monica.

Tunafahamu vizuri sana jinsi Baba Mtakatifu Francisko alivyojitolea kwa ibada ya Mtakatifu Monica, ibada ambayo yeye, kama alivyokuwa akirudia mara kwa mara, aliirithi kutoka kwa mama yake, mshirika wa dhati wa Chama cha akina Mama Wakristo wa Mtakatifu Monica. Kwa hiyo, mwaka huu, Papa Francisko alitaka kurudi hapa, kwenye Basilica ya Mtakatifu Agostino, ambapo masalio ya mwili wa Mtakatifu Monica, huhifadhiwa,na ambapo ibada hii kubwa, iliyoenea sana hasa kati ya akina mama, imehifadhiwa.

Je, unaweza kueleza baadhi ya maelezo ya ziara hii ya pekee?

Papa Francisko aliwasili muda wa saa kumi jioni na alionekana mwenye afya na furaha. Ziara hii pengine ilikuwa ni ziara iliyotarajiwa kwa upande wake. Baada ya kusalimiana na Mkuu wa Nyumba ya jumuiya, alikwenda kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Monica, ambako mara moja alikuwa na shada la maua meupe na limewekwa kwenye kaburi la Mtakatifu Monica na baadaye akakaa kimya, katika maombi. Mwishoni mwa sala hii aliomba kusindikizwa mbele ya Mama  wa Wanahija inayopendwa sana na Waroma wengi, ambayo kwa hakika itakuwa hivyo zaidi wakati wa Jubilei kutokana na maana ambayo inachukua. Alizungukwa na watu wengi ambao kwa wakati huo walikuwa wameanza kukusanyika katika Basilika, bada ya kufunguliwa, wakati huohuo kwa ajili ya ibada ya waamini, Papa alibaki akitafakari uchoraji na kisha akasalimia, kwa urafiki wake wa kawaida, wanawake wengi, watawa, mapadre, waliofika kusali mbele ya kaburi la Mtakatifu Monica. Baada ya kusalimiana tena na Jumuiya ya mapadre wa Agostino, aliondoka.

Ulipata fursa ya kubadilishana maneno machache?

Kwanza kabisa, tulimhakikishia maombi yetu kwa ajili ya huduma yake, kwa ajili ya nafsi yake, zaidi ya yote kwa ajili ya Kanisa zima, naye akaitikia kwa kichwa, akashukuru kwa usikivu huu, na akatualika kudumu katika sala hii. Pia alitaniana na Mkuu wa nyumba ambaye alikuwa akiwatambulisha Waagostiniani, alimuuliza kama sisi tulikuwa Waagostiniani wazuri na hii iliamsha tabasamu kwa kawaida.

Je, ziara ya Papa Francisko inaleta nini kwenye sherehe za Monica na Agostino 27 na 28 Agosti ?

Inatuthibitisha katika imani, kwa kuwa yeye ni mchungaji wa Kanisa zima, anatuthibitisha pia katika ibada kwa Mtakatifu Monica, kwa Mtakatifu Agostino. Inatuthibitisha zaidi ya yote katika kufuata maadili fulani. Mtakatifu Monica ni mwanamke mvumilivu, mwanamke aliyepo sana katika maisha ya watoto wake, kama akina mama wengi leo. Hapa, Monica anatufundisha kwamba Bwana husikiliza maombi ya wanyenyekevu, husikiliza maombi ya wale wote ambao, kwa uvumilivu, kwa uaminifu, kwa uthabiti, wanamwomba Bwana matunda mema katika maisha yao wenyewe na katika maisha ya wengine. Na ninadhani ni ujumbe ambao pia unapitia katika ziara hii ya Baba Mtakatifu Francisko, ambaye kwa hakika atakuwa ameomba matunda mengi ya mema kwa Kanisa, kwa binadamu wote, zaidi ya yote kwa ajili ya kupatikana kwa amani. Monica alikuwa mwanamke wa amani, Monica alikuwa na sanaa hii, uwezo huu wa kuleta amani katika mazingira ambayo yeye mara kwa mara.

Papa alitembelea kaburi la Mtakatifu Monica
28 August 2024, 09:24