Kila tarehe 11 Agosti ni siku kuu ya Mtakatifu Clara wa Assisi. Kila tarehe 11 Agosti ni siku kuu ya Mtakatifu Clara wa Assisi. 

Papa atawakia matashi mema Waklara katika Siku kuu ya Mtakatifu wao

Papa Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana,tarehe 11 Agosti amekumbusha Kumbukizi ya Mtakatifu Clara wa Assisi na kuwatakia matashi mema Watawa wa Ndani Waklara hasa wa Monasteri ya--- ambao amesema wana urafiki sana na yeye.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 11 Agosti 2024, Baba Mtakatifu amekumbusha pia kumbukizi ya Mtakatifu Clara wa Assisi, mfuasi wa Mtakatifu Francis wa Assisi. Papa alisema: “Leo nakumbuka siku kuu ya Mtakatifu Clara. Na wazo langu la upendo kwa Waklara wa ndani  wote  hasa wale wa Vallegloria ambao nina urafiki mzuri unaonifunga.”

Tunaweza kujifunza nini kwa chupikizi  cha Mtakatifu Francis?

Mtakatifu Clara alizaliwa tarehe 16 Aprili 1194 huko Assisi na kifo chake mnamo tarehe 11 Agosti 1253. Kaburi lake liko kwenye Basilika ya Mtakatifu Clara Assisi. Alikuwa na ndugu zake Agnes wa Assisi, Penenda na Beatrice, baada ya baba yake kufariki, mama yake alijiunga pia na utawa, na kwa hiyo ndani ya conventi wakawa watawa watatu ndugu. Alitangazwa kuwa Mtakatifu mnamo mwaka 1255 na Papa Alessandro IV katika Kanisa Kuu la Anagni Italia. Mtakatifu Clara anajulikana kuwa ni msimamizi wa wahusika wa Televisheni. Je tunaweza kujifunza nini kutoka kwa Mtakatifu Clara? Mtakatifu anatuhimiza leo hii kuwa na mtindo wake unaoegemea juu ya Kristo aliye maskini na aliyesulubiwa ili kulinda wema wa wote, kushinda ulinzi wa upande na maslahi ya wachache, kutoa huduma kwa wale wote wanaohitaji.

Madhabahu na Monasteri ya Waklara Assisi
Madhabahu na Monasteri ya Waklara Assisi

Mtakatifu Clara anatukumbusha nini?

Clara anatukumbusha kuendelea na safari ndani ya upeo wa mtazamo wa macho ya Mungu na kutazama na kuona maisha kwa mtazamo mpya ambao umefanya kuwa na uwezo wa kuona asiyeonekana-mungu katika maisha ya kila siku. Je, Clara wa Assisi anatoa ujumbe gani leo hii na ushuhuda wake wa maisha ya kiinjili? Ni kukutana na Kristo maskini na msulubiwa, akifuata mfano wa Fransis, kunamruhusu kuitikia kwa ari wito wa kuishi Injili kwa sababu, tendo la Clara, la kukutana na Bwana 'wake' ilikuwa chanzo cha maisha yake yote kama mwanamke, aliyeishi katika ishara ya kuwa mali Yake kabisa” (Massimo Fusarelli, Mkuu wa Shirika la Ndugu Wadogo). Clara anatualika kupata maana ya kutoa maisha yetu katika wakati huu ambao inaonekana kuwa karibu kutoweka kutoka katika  upeo wa mtazamo wa mwanadamu: mara nyingi tunatafuta ustawi wetu binafsi! Tukiwa tumeshangazwa na kelele nyingi, hatuzingatii tena maombi, ukimya wa kina, kutafuta uwepo wa Mungu ndani yetu, kutunza mahusiano na kufurahia uzuri wa kazi ya uumbaji. Katika kutafuta faida ya mtu binafsi mara nyingi tunageuzwa sisi wenyewe kulima mashamba yetu wenyewe na mitandao ya kijamii na hatuwezi kusikiliza na kukuza wema wa kweli miongoni mwa watu.

Hawa ni Masisita wa ndani wa Mtakatifu Clara huko Mikuli  Kroatia
Hawa ni Masisita wa ndani wa Mtakatifu Clara huko Mikuli Kroatia

Kuishi uhusiano na Bwana na kuwa karibu na wengine

Tukiangalia baadhi ya kurasa za Mtakatifu Clara tunafahamu juhudi na nguvu ambayo kwayo anasimulia uzoefu wa kibinafsi wa imani uliowekwa alama na nyakati za kutafakari za kuzamishwa katika mambo ya ndani. Na ni pale hasa ambapo uwepo wa ajabu wa Mwenyezi Mungu unaonekana na kuwasili kwa utambulisho ulio wazi zaidi na wa kweli zaidi, ambao hutoa msukumo na nguvu kwa ajili ya kuanza upya na kwa mahusiano ya ukaribu, utunzaji na kukubalika kwa wengine. Hata katika historia zetu kama waamini, kujali maana ya maisha mara nyingi hukosekana: tunafuata dini, lakini hatuishi kwa imani. Mara nyingi tunachanganya maarifa ya kiakili ya Neno la Mungu lenyewe na safari ya kiinjili.  Imani inafanyika sio tu katika Liturujia na pia wakati uzoefu wa kuwa pamoja na Bwana unaoneshwa na kuonekana katika uhusiano na watu wote walio hai. Lakini Je imani yetu inatafsiri vipi katika maisha ya kila siku? Wale wanaoishi katika uhusiano unaoendelea na Bwana na wanatambua kuwa daima mbele zake huchagua kushuhudia kwa uthabiti tendo la Kristo ambaye alitoa maisha yake kwa upendo. Clara alimwomba Agnese amtazame Yule aliyewekwa juu ya mti wa msalaba na kumwalika aseme kwa sauti moja kwa Yesu kwamba: “Kumbukumbu yako haitaniacha kamwe” (4LAg 26: FF 2904).

Je tunajua jinsi kila mtu anaishi kwa mtazamo wa Mungu?

Swali jingine la kujiuliza ni kwamba: Je, sisi sote tunaamini kwamba kila mtu daima anaishi chini ya mtazamo wa Mungu hata tunapokengeushwa na mambo mengine? Mtakatifu Klara wa Assisi, kama ilivyo kwa Mtakatifu Fransis, alitoa urithi wake kwa maskini na, bila kumiliki chochote, alimfuata Kristo maskini na aliyesulubiwa na kujisalimisha kwake. Alifanya mapatano na umaskini mtakatifu na aliupenda sana hata hakutaka kitu kingine isipokuwa Bwana Yesu, na hakuwaruhusu binti zake kumiliki chochote,” (LegsC 9: FF 3183) hawa Watawa wa ndani waclara. Kufuata nyayo za Kristo kunamaanisha kujiweka huru njiani kutoka kwa kila kitu ambacho hakituruhusu kumwilisha Injili. Utambuzi unaoendelea hutusaidia kuthibitisha kama kila neno linalosemwa, kila hisia inayoonyeshwa, kila tendo linalofanywa linatoka kwa Bwana au kutoka kwa mtu mwenyewe. Wale wanaochagua kuishi Injili huchukua mtindo wa Bwana Mfufuka, wakitangaza uwepo wa Mungu kwa maisha yao. Clara aliishi katika maisha ya kila siku kulingana na utii wa imani na, akimsikiliza Yule anayemvutia (Taz. 4LAg 30: FF 2906), alijifunza kukutana na kila mtu mwingine kwa heshima na kwa mantiki ya kutoa.

Tabia kuu ya Waklara ni kuabudu Yesu wa Ekaristi
Tabia kuu ya Waklara ni kuabudu Yesu wa Ekaristi

Clara:Uchaguzi wa kumfuata Kristo kwa utiifu bila chochote 

Kwa upande wa Clara, kama vile kwa Mtakatifu Francis wa Assisi, uchaguzi wa kumfuata Kristo kwa utiifu, bila kitu chochote cha mtu mwenyewe, katika usafi wa moyo na umoja mtakatifu, ni njia ya kuibua Injili kwa njia ya maisha madhubuti. Kwa kutambua zawadi ya kuwapo, hulinda mahusiano na, bila uhusiano wowote, huwafikia wengine. Clara aliwaomba watawa wenzake waanzishe uhusiano wa kibinadamu na wa kiinjili na kushiriki hisia na uzoefu katika udugu: “Kwa kujiamini wakieleza mahitaji yao kwa kila mmoja (RsC VIII, 15: FF 2798). Clara hakujali  historia na jamii ya wakati wake tu, kiukweli yeye pia alikuwa makini na hatima ya Assisi, wakati wa uvamizi wa Saracens. Alisali kwa imani pamoja na watawa wenzake akiwa na uhakika kwamba wavamizi hao wangeondoka bila kusababisha madhara na, pengine sana kulingana na dhana fulani (Felice Accrocca), aliwasiliana na Elia, ambaye wakati huo alikuwa amefukuzwa kazi yake kama waziri mkuu, karibu kwa Mflame Frederick II, kuzuia uvamizi wa Assisi.

Picha ya Mtakatifu Clara wa Assisi
Picha ya Mtakatifu Clara wa Assisi

Clara leo hii anatuhimiza kuegemea Kristo aliye maskini

Ndugu msomaji kwa njia hiyo Mtakatifu Clara anatuhimiza leo hii kwa mtindo wake unaoegemea juu ya Kristo aliye maskini na aliyesulubiwa ili kulinda manufaa ya wote, kushinda ulinzi wa upande mmoja na maslahi ya wachache, kutoa huduma kwa wale wote wanaohitaji. Anatukumbusha kuendelea na safari ndani ya mtazamo wa  Mungu na kutazama na kuona maisha kwa macho mapya ambayo yameifanya kuwa na uwezo wa kuona asiyeonekana-mungu katika maisha ya kila siku. Hivyo tunaweza kupendelea ukimya, mambo ya ndani, mtazamo wa unyenyekevu ulio wazi kwa ulimwengu kama alivyojifunza kutoka kwa Fransisko ambaye bado anazungumza katika wakati wetu. Leo hii maisha yake yanatuongoza kujitoa ili “kila mtu apate kukutana na Yesu Kristo aliyefanyika mwili, aliyefanywa mwanadamu, historia iliyofanywa, alisema hata Papa Francisko.

Mtakatifu Clara :anatuhimiza nini?

 

11 August 2024, 12:10