Papa:Bila Roho Mtakatifu Kanisa haliendi mbele,halikui&halihubiri!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ameanza tena katekesi yake mara baada ya muda wa mapumziko mwezi Julai. Kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican tarehe 7 Agosti 2024 ameanza kwa salamu kwa wote na kueleza jinsi ambavyo “tunaingia katika hatua ya pili ya historia ya Wokovu. Mara baada ya kutafakari juu ya Roho Mtakatifu katika kazi ya Uumbaji,” Papa amesema: “ tuttafakari kwa majuka kadhaa ya kazi ya Wokovu, yaani wa Yesu Kristo.” Baba Mtakatifu ameanzia kwa hiyo na Agano la Kale na kutazama Roho Mtakatifu katika Agano Jipya kwamba tema ya Siku ni “Roho Mtakatifu katika Neno lililofanyika mwili.” Katika Injili ya Luka, tunasoma kuwa: “Roho Mtakatifu atashuka juu yako (Maria) na nguvu zake za Aliyejuu zitakufunika kama kivuli (Lk 1,35). Mwinjili Matayo anathibitisha tendo hili msingi ambapo linatazama Maria na Roho Mtakatifu akisema kuwa Maria “alijikuta na mimba kwa njia ya Roho Mtakatifu(Mt1,18). Na Kanisa lilikusanya tukio la ufunuo huo. Na kupokea mapema katika moyo wa Alama ya imani.
Katika Mtaguso wa Kiekumene wa Costantinopoli, mnamo 381 ambao ulifafanua utakatifu wa Roho Mtakatifu, tendo hilo lilingia katika kanuni ya Imani, ambayo inaitwa ya Nicea- Constantinopoli na ndiyo tunayosali wakati wa misa. Hiyo inathibitisha kwamba Bwana wa Mungu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kwake yeye Bikira Maria akawa Mwanadamu. Kwa njia hiyo hili ni tendo la imani la kiekuemeni, kwa sababu wakristo wote wanasadiki pamoja Alama ile ile ya imani. Inafaa kabisa kurudia pamoja kwa kusema maneno: “Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Ndimi mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyonena, Neno la Bwana akatwaa mwili, na akakaa kwetu.”
Kanuni hiyo ya imani ni msingi ambayo inaruhusu kuzungumza ya Maria kama Mchumba hakika ambaye ni Sura ya Kanisa. Kiukweli Mtakatifu Leo Mkuu aliandika: “kiukweli kama alivyozaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na Bikira Maria Mama, hivyo analifanya Kanisa, kuwa Bibi-arusi wake asiye na doa, kuzaa matunda kwa pumzi muhimu ya Roho yule yule. Ulinganisho huo ulichukuliwa katika Katiba ya Kidogma ya Lumen gentium ambayo inasema kuwa: “Kwa imani na utii wake Maria alimzaa Mwana wa Mungu yule yule hapa duniani, bila kuwasiliana na mwanadamu, bali alifunikwa na Roho Mtakatifu.”[...] Naam, Kanisa, likitafakari utakatifu wa ajabu wa Bikira, likiiga upendo wake na kutimiza kwa uaminifu mapenzi ya Baba, kwa njia ya Neno la Mungu lililokubaliwa kwa uaminifu, pia linakuwa mama, kwa kuwa kwa mahubiri na ubatizo huzalisha watoto, waliochukuliwa mimba na Roho Mtakatifu na kuzaliwa na Mungu, kwa uzima mpya na usioweza kufa” (rej.63,64).
BabaMtakatifu Francisko akiendelea alisema: “Tunahitimisha kwa tafakari ya vitendo katika maisha yetu, yanayopendekezwa na msisitizo wa Maandiko juu ya vitenzi “mimba” na “kuzaa.” Katika unabii wa Isaya tunasikia: “Tazama, bikira atachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume.” (Is 7.14); na Malaika alimwambia Maria: “Utachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume, (Lk 1,31). Maria alichukua mimba kwanza, kisha akamzaa Yesu: alimkaribisha ndani yake, moyoni mwake na katika mwili wake, kisha akamzaa. Hili pia linatokea kwa Kanisa: kwanza linakaribisha Neno la Mungu, linaacha lizungumze katika moyo wake” (taz Hos 2:16) na “kulijaza matumbo yake” (taz Ez 3:3), kulingana na semi mbili za kibiblia ili kuweza kuakisi katika mwanga wa maisha na kuhubiri.
Operesheni ya pili ni tasa bila ya kwanza. Maria aliyeuliza: je itakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako(Lk 134). Hata Kanisa, linakabiliwa na kazi zaidi ya nguvu zake, kwa kawaida huuliza swali lile lile: “Hii inawezekanaje?” Inawezekanaje kumtangaza Yesu Kristo na wokovu wake kwa ulimwengu unaoonekana kutafuta ustawi tu, katika dunia hii? Jibu pia ni sawa na wakati huo: “Mtapokea nguvu kutoka kwa Roho Mtakatifu […]Na mtakuwa mashuhuda wangu (Mdo1,8)). Bila Roho Mtakatifu Kanisa haliwezi kwenda mbele, Kanisa haliwezi kukua, Kanisa aliwezi kuhubiri,” Papa amesisitiza.
Yesu Mfufuka kwa hiyo aliwambia Mitume karibu kwa maneno sawa na aliyoeleza Maria katika tangazo. Kile ambacho Kanisa kwa Ujumla kinasema, kinatuhusu hasa sisi, kwa kila mmoja yaani mbatizwa. Kila mmoja wetu wakati mwingine hujikuta katika hali ya maisha ambayo ni zaidi ya nguvu zetu na kujiuliza: “Ninawezaje kukabiliana na hali hii? Papa amesema kuwa “Inasaidia katika kesi hizi, kukumbuka na kurudia maneno yake yale ambayo Malaika alimwambia Bikira Maria, kabla ya kuondoka kwake kwamba:“Hakuna kisichowezekana kwa Mungu(Lk 1,37). Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Francisko ameomba kwamba: “Hebu basi pia tuendelee na safari yetu, kila wakati, tukiwa na uhakika huu wa kufariji mioyoni mwetu: “Hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Na tukiamini hili, tutafanya miujiza. Hakuna lisilowezekana kwa Mungu.”