Papa Francisko awaombea waathirika wa ajali mbaya ya ndege huko Brazil
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 11 Agosti 2024 akiwageukia waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican amesali kwa ajili ya wahanga wa ajali mbaya nchini Brazil na kusema: “Tusali kwa ajili ya waathirika wa ajali ya Ndege iliyotokea huko Brazil”.
Uchunguzi wa ajali
Shirika la ndege la Voepass lilitangaza hivi karibuni kwamba bado halijaweza kupata sababu za ajalihiyo. Kulingana na vyanzo vya habari, vinabainisha labda baridi inaweza kuwa moja ya sababu kutokana na kwamba ndege ilikuwa inaruka kwa urefu wa futi elfu 17, urefu ambao uundaji wa barafu unaweza kuwa hatari kubwa, kama ilivyoripotiwa na mamlaka ya kimataifa ya anga. Hata hivyo, Voepass alihakikisha kuwa mfumo wa kupambana na icing ulikuwa ukifanya kazi kikamilifu wakati wa kuondoka. Na hata Anac, shirika la udhibiti wa anga la Brazil, tayari limefahamisha kuwa ndege hiyo iliyotengenezwa mwaka 2010 ilikuwa imepitisha mara kwa mara ukaguzi wote wa usalama.
Wakati huo huo, Jeshi la Wanahewa la Brazil (Fab) limetuma wachunguzi wa ajali za angani (Seripa) kwenye tovuti ili kufanya uchunguzi wa kiufundi. Wataalamu wa uchunguzi wa kimahakama wa Brazil badala yake wanafanya kazi ya kutambua mabaki ya watu 62 waliofariki katika ajali hiyo: mamlaka za eneo hilo zimeeleza kuwa miili ya rubani, Danilo Santos Romano, na rubani mwenzake, Humberto de Campos Alencar e Silva, walikuwa wa kwanza, kutambuliwa.
Salamu za Papa kwa wote
Na kwa wote Papa amewasalimia waroma na mahujaji kutoka Italia na nchi nyingi, hasa kikundi cha wanafunzi kutoka Seminari Ndogo ya Bergamo, waliofika kwa miguu kutoka Assisi, kwa hija iliyochukua siku chache. Amewauliza “Je, mmechoka? Wakatibu: Hapana? Papa akasema “ Sawa. Ni vizuri!” Hatimaye amewatakia wote Dominika njema. Na kwa wote pia, watoto wa Parokia ya Moyo safi. Na tafadhali wasisahau kumuombea: Watu wa Brazil pia, aliwaona uwanjani vizuri. Kila mtu, na kuwashukuru huku akiwatakia mlo mwema, mchana mwema na kwaheri ya kuonana.