Papa:Imani na sala ya kweli inafungua akili na moyo na haifungi!

Katika Injili ya leo inatuambia mtazamo wa Wayahudi kuhusu uthibitisho wa Yesu asemaye:“nimeshuka kutoka Mbinguni”na wanabaki na mitazamo ya kuhukumu.Tuwe makini kwa sababu wakati mwingine inawezekana kutokea hata kwetu sisi,katika maisha yetu ya imani na katika sala zetu,badala ya kujiweka katika usikivu kwa Bwana.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika dominika ya 19 ya mwaka wa Kawaida wa Kanisa, Dominika tarehe 11 Agosti 2024, Baba Mtakatifu akiwa katika dirisha la Nyumba ya Kitume amewageukia waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kutoa tafakari yake kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana. Papa Francisko akianza amesema: “Katika  Injili ya leo (Yh 6,41-51) inatuambia mtazamo wa Wayahudi kuhusu uthibitisho wa Yesu ambaye anasema:“nimeshuka kutoka Mbinguni(Yh 6,38). Walikashifu. Wao walianza manung’uniko kati yao kwamba: “Huyu siye Yesu, mwana wa Yosefu? Kwake  yeye wanamjua baba yake na mama yake,  ni kwa jinsi gani anaweza kusema kuwa “Nimeshuka kutoka mbinguni?(Yh 6,42). Papa Francisko ameongeza: “Tuwe makini kwa yale wanayosema. Wanaamini kwamba Yesu hawezi kuja kutoka mbinguni, kwa sababu ni Mtoto wa seremala na kwa sababu mama yake na nduguze ni watu wa kawaida,watu wanaojulikana, kawaida kama watu wengine. Kwa jinsi gani inawezekana Mungu kujionesha kwa namna hiyo ya kawaida?

Sala ya Malaika wa Bwana
Sala ya Malaika wa Bwana

Kwa njia hiyo “Hawa wamezuiwa, katika imani, na mantiki za kuhukumu mbele ya asili yake ya unyenyekevu na kutokana na dhana, kwa hiyo hana lolote la kuweza kujifunza kutoka kwake. Mawazo na dhana, yana madhara kiasi gani yanayotuletea! Yanazuia mazungumzo ya dhati, maelewano kati ya ndugu... Kuwa waangalifu na dhana hizo, Papa ameonya. Mitazamo yao ni migumu, na hakuna nafasi katika mioyo yao, kwa hiyo kile ambacho hakiingii na kile ambacho kinaweza kuorodhesha na kutunzwa kwenye makabati ya kusafishwa uhakika wao. Papa ameongeza “Na hiyo ni kweli, hee? Mara nyingi dhamana zetu zimefungwa, zinakuwa na vumbi, kama vitabu vya zamani.”

Sala ya Malaika wa Bwana 11 Agosti
Sala ya Malaika wa Bwana 11 Agosti

Licha ya hayo ni watu ambao wanashikilia sheria, wanatoa sadaka, wanaheshimu kufunga na vipindi vya sala. Na Kristo alikuwa tayari ametenda miujiza (Yh 2,1-11; 4, 43-54:5,1-9;6,1-25).” Baba Mtakatifu ameongeza: “Je ni kwa nini hayo yote hayakuwasaidia kumtambua Yeye kuwa ni Masiha?, Baba Mtakatifu ameuliza na kujibu: “ kwa sababu wanatimiza mazoe yao ya kidini, si kwa sababu ya kujiweka katika usikivu wa Bwana, bali kwa ajili ya kupata kutoka kwake uthabiti wa kile ambacho wao tayari wanafikiria.  Wamefungwa kwa Neno la Bwana na kutafuta uthibitisho wa mawazo yao.” Hii inajionesha kutokana na kwamba hawahangaiki kumuuliza ufafanunuzi Yesu bali wanaishia kunung’unika kati yao dhidi yake (Yh 6,41), kama kujihakikisha wao kwa wao ya kuona ambacho wao wanaamini, wakijifunga wenyewe kama vile ngome isiyopitika. Na ndivyo wanashindwa kuamini. Kufungwa kwa moyo: ni kiasi gani kunaumiza, na ni madhara gani.” Hata hivyo “Tuwe makini kwa hayo yote kwa sababu wakati mwingine inawezekana kutokea hata kwetu sisi, katika maisha yetu ya imani na katika sala zetu. Inawezakana kutokea,  yaani badala ya kujiweka katika usikivu kweli wa kile ambacho Bwana anataka kutuambia sisi tunatafuta kwake na kwa wengine kile cha uthibiti tu ambao sisi tunafikiria, kwa imani zetu na  kwa hukumu zetu.”

Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 11 Agosti
Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 11 Agosti

Lakini kwa mtindo huo wa kumwelekea Mungu hautusaidii kukutana naye kweli, na wala kujifungulia zawadi ya mwanga wake na wa neema yake ili kukua katika wema, kufanya mapenzi yake na kushinda vifungo na matatizo. Imani na sala ya kweli inafungua akili na moyo na wala havifungi. Papa amesema tena “Unapomkuta mtu amefunga akili, katika maombi, imani hiyo na maombi hayo si ya kweli.” Kwa njia hiyo Papa ameomba tujiulize: je maisha yangu ya imani yana uwezo wa kufanya ukimya wa kweli katika ndani yangu na kujiweka katika usikivu wa Mungu? Niko tayari kupokea sauti yake mbali na mipango yangu na kushinda hata kwa msaada wake, hofu zangu? Maria atusaidie kusikiliza kwa imani sauti ya Bwana na kuwa jasiri wa mapenzi yake.” Amehitimisha.

Tafakari ya Papa katika sala ya Malaika wa Bwana 11 Agosti 2024
11 August 2024, 15:15