Papa kwa Jukwaa,Alpbach:muwe mashuhuda waambukizi wa maadili ya Ulaya!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, alituma ujumbe wake uliotiwa saini tarehe 21 Agosti 2024 kwa washiriki wa Jukwaa la Ulaya huko Alpbach, nchini Austria linaloendelea hadi tarehe 30 Agosti 2024. Katika ujumbe huo Baba Mtakatifu alibainishwa kuonesha furaha ya kuwaelekea baadhi ya maneno. “Ninapofikiria Ulaya, nafikiria kwanza kabisa bara la haki za binadamu. Kwa kiasi kikubwa, haki muhimu za binadamu kwa wote zimepokea maendeleo yao hapa. Kwa sasa tunaishi katika wakati wa shida Ulaya, ambapo kama kila shida huleta hatari na fursa; wakati ambapo harakati mbalimbali za watu wengi hufurahia umaarufu mkubwa.” Sababu zake ziko katika mambo ya kiuchumi na kisiasa.
Mazingira ya kiutamaduni yamebadilika na kanisa linaisha na jamii isiyo na dini
Papa Francisko anabainisha kuwa "Kwa hiyo tunaona kwamba katika Ulaya, kufuatia “wimbi” hili la watu wengi, baadhi ya maadili yametoweka na baadhi ya kanuni, zinazohusiana na tabia kwa wanachama dhaifu wa jamii, zimewekwa nyuma. Mawazo na kanuni hizo, ambazo kati ya zile za hadhi na udugu zinastahili kutiliwa mkazo maalum, daima zimekuwa zikilinganishwa na tumbo la Injili. Kwa njia hiyo Papa Francisko amebainisha kuwa “Leo mazingira ya kiutamaduni yamebadilika, na Kanisa linaitwa kuishi ndani ya jamii isiyo na dini; hili lisishangaze au la kuogopesha, kwa sababu tunajua vyema kwamba Mungu yupo huko pia. Badala yake, kwa motisha mpya, tujitahidi, kama Wakristo, kuleta utajiri wa mafundisho ya kijamii ya Kikatoliki pamoja na mahitaji yake kwa ulimwengu wote. Hata Umoja wa Ulaya, tangu kuanzishwa kwake, umekuwa na sifa za ulimwengu wote, na inatumainiwa kwamba haitazipoteza.”
Ulaya itafute njia za kupunguza ubaguzi
Kwa kukazia zaidi Papa Francisko amebainisha kuwa "Kwa maana hiyo, kipengele cha udugu ni muhimu sana. Kwa hivyo inafuata kwamba Jamii za Ulaya zinaitwa kutafuta njia na mbinu za kupunguza ubaguzi ndani yao wenyewe na kubaki wazi kwa ulimwengu unaowazunguka.” Papa Francisko kwa washiriki katika Jukwaa la Ulaya huko Alpbach, amewashukuru kwa kujitolea kwao, katikati ya changamoto za kijamii za wakati wetu, na amewatakia wawe mashuhuda waambukizi wa maadili ya Ulaya. Amewabariki kutoka ndani ya moyo wake na kuwaomba tafadhali wamuombee.