Papa Francisko:mshangao na shukrani mbele ya muujiza wa Ekaristi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Dominika ya 20 ya Kawaida ya,mwaka wa Kanisa, Dominika tarehe 18 Agosti 2024, Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari yake, kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana, kwa mahujaji na waamini waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu akianza tafakari hiyo amesema “Injili ya leo inazungumza juu ya Yesu ambaye anatudhibitishia kwa urahisi: Mimi ni mkate wa uzima, ulioshuka toka mbinguni(Yh 6,51). Mbele ya umati, Mwana wa Mungu anajifananisha na mwilisho wa kawaida wa kila siku, mkate “Mimi ni Mkate.” Kati ya wale waliokuwa wakisikiliza, baadhi walianza kujiuliza(Yh 6,52): Inawezekanaje Yesu kutupatia kula mwili wake? Hata sisi leo hii tujiulize swali hilo, lakini kwa mshangao na kwa shukrani. Na tazama ndizo tabia mbili za tafakari juu ya mshangao na shukrani mbele ya muujiza wa Ekaristi,” Papa amesisitiza.
Kwanza: mshangao, kwa sababu maneno ya Yesu yanatushangaza. “Lakini Yesu daima hutushangaza. Hata leo hii katika maisha Yesu hutushangaza,”Papa amekazia kusema. Mkate kutoka Mbinguni ni zawadi ambayo inazidi matarajio yote. Asiyeupokea mtindo wa Yesu anabaki na mashaka: utafikiri haiwezekani, na zaidi yasiyo ya kibinadamu kula mwili wa mtu na kunywa damu yake (Yh 6, 54). Mwili na damu, kinyume chake ni ubinadamu wa Mwokozi, maisha yenyewe aliyoyatoa kwa ajili ya chakula chetu. Papa ameongeza kuwa "Na hiyo inatupeleka katika tabia ya pili ambayo ni kutoa shukrani kwa sababu tunamjua Yesu pale ambao anakuwapo kwa ajili yetu sisi. Yeye anajifanya mkate kwa ajili yetu. “Anayekula mwili wangu anabaki ndani yangu nami ndani yake (Yh 6,56).”
Kristo, mtu kweli, anajua vizuri kwamba lazima kula ili kuishi. Lakini anajua pia kuwa hiyo haitoshi. Baada ya kugawa mikate mingi duniani (Yh 6, 1-14), Yeye anaandaa zawadi ambayo bado ni kubwa zaidi: Yeye mwenyewe anajifanya chakula kweli na damu yake kweli (Yh 6,55). Shukrani kwa Bwana Yesu” Papa Francisko ameongeza kusema: "kwa moyo tunaweza kusema Asante, asante.” Akiendelea kudadavua Papa alisema: “Mkate wa mbinguni, unaoshuka kutoka kwa Baba ni Mkate hasa ambao Mwanae alifanyika mwili kwa ajili yetu. Umwilisho huo ni zaidi ya mahitaji yetu, kwa sababu mkate wa matumaini unashibisha njaa ya kweli, njaa ya wokovu ambayo sisi sote tunahisi kutokuwa nayo katika tumbo, lakini katika moyo. Ekaristi ni ya lazima kwa wote.”
Ni jinsi gani neno lilivyo la sasa, la Injili. Wakati shida, ukosefu wa haki na vurugu zinatoa mkate wa kila siku kwa waamini. Yesu anatutunza kwenye mahitaji makubwa zaidi: anatuokoa, kwa kumwilisha maisha yetu na yake, na hiyo daima. Na shukrani Kwake tunaweza kuishi na umoja na Mungu kati yetu. Mkate wa uzima na wa kweli siyo jambo la viinimacho, hapana; sio jambo jingine ambalo linasaidia kutatua matatizo yote kwa haraka, bali ni Mwili ule ule wa Kristo, unaowapatia maskini tumaini na kushinda kiburi cha wale wanaojishibisha kwa hasara yao. Tujiulize kwa hiyo sasa: Je nina njaa na kiu ya wokovu, na si kwa ajili yangu tu, bali kwa ajili ya kaka na dada wote? Ninapokea Ekaristi ambayo ni muujiza wa huruma? je ninajua kushangaa mbele ya Mwili wa Bwana, aliyekufa na kufufuka kwa ajili yetu? Kwa kuhitimisha Papa Francisko ameomba kwamba "Tusali pamoja na Bikira Maria ili atusaidie kupokea zawadi ya mbingu katika ishara ya mkate."