Papa Francisko:tufikirie juu ya nchi zilizo kwenye vita
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika salamu zake kwa waamini wanaozungumza lugha ya kiitaliano, Papa Francisko: Ninawakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano. Kwa namna ya pekee, ninawasalimu washiriki wa mkutano wa majira ya kiangazi kwa Waseminari, ambao ni matarajio ya kuendeleza malezi yaoyanayolishwa na Neno la Mungu na Mkate wa Uzima; Pia ninasalimia vikundi vya parokia, hasa vile vya Marinella-Bagnara Calabra na Rovato.
Ninakaribisha kwa furaha Wanakipaimara wa Jimbo la Chiavari: "wapendwa wavulana na wasichana, pamoja na zawadi za Roho Mtakatifu, mlizopokea kwa Kipaimara, urafiki wenu na Yesu umekuwa wa karibu zaidi na unalishwa na Ekaristi. Kwa sababu hiyo ninawahimiza kushiriki kwa uaminifu Misa ya Dominika pia kukaribia Sakramenti ya Kitubio Kuungama ni kukutana na Yesu ambaye anatusamehe dhambi zetu na kutusaidia kutenda mema.” Papa aliongeza kusema "Inasemwa - lakini ni lugha mbaya, kwa sababu wanasema kuwa kipaimara ni sakramenti ya kuaga, ambayo mara moja ikipokelewa, hakuna mtu anayerudi tena kanisani. Nadhani hii sio kweli: kila wakati lazima kurudi kanisani!" Papa amewahimiza.
Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa:Na tufikirie juu ya nchi zilizo kwenye vita, nchi nyingi kwenye vita. Tufikirie Palestina, Israeli, Ukraine inayoteswa, tunafikiria Myanmar, Kivu Kaskazini na nchi nyingi kwenye vita. Bwana awape karama ya amani. “Hatimaye, mawazo yangu yanawaendea vijana, wagonjwa, wazee na waliooa hivi karibuni. Kwa kumwiga Mtakatifu Agostino, ambaye kumbukumbu yake ya kiliturujia tunaadhimisha leo hii, kuwa na kiu ya hekima ya kweli na bila kukoma mtafute Bwana, chanzo hai cha upendo wa milele. Kwa ninyi nyote, baraka yangu!