Papa,katekesi kuhusu Wahamiaji:bahari na jangwa visiwe makaburi!

Katekesi ya Papa,Agosti 28 imejikita kwa wahamiaji,jangwa na bahari:Lazima kuunganisha nguvu kupambana na biashara haramu ya binadamu, kukomesha wahalifu wanaotumia vibaya mateso ya wengine bila huruma.Ni dhambi kubwa kuwakataa wahamiaji wasioonekana,Mungu anateseka nao.Hapana sheria zenye vizuizi zaidi na uwekaji kijeshi katika mipaka na tusikubali kuambukizwa na utamaduni wa kutojali.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatano tarehe 28 Agosti 2024, Mama Kanisa akiwa anamkumbua Mtakatifu Agostino wa Hippo, Askofu na Mwalimu wa Kanisa, Baba Mtakatifu Framncisko kama kila Jumatano amefanya katekesi yake kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Kabla ya tafakari ilisomwa zaburi ya 107, 1.4-7 isemayo: “Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema,kwa maana upendo wake ni wa milele. […]Wengine walitangatanga jangwani kwenye barabara zilizopotea, bila kupata mji wa kuishi.Walikuwa na njaa na kiu, maisha yao yalipotea. Katika dhiki zao walimlilia Bwana akawaokoa na shida zao. Leo hii naahirisha katekesi iliyozoeleka na ningependa nitafakari nanyi kuwaza kuhusu watu ambao- hata wakati huu  wanavuka bahari na majangwa ili kufikia nchi ambayo wanaweza kuishi kwa amani na usalama. Bahari na jangwa: maneno haya mawili yanarudi katika shuhuda nyingi ninazopokea, kutoka kwa wahamiaji na kutoka kwa watu ambao wamejitolea kuwasaidia. Na ninaposema “bahari”, katika muktadha wa uhamiaji, ninamaanisha pia bahari, ziwa, mto, mabwawa yote ya maji yenye hila ambayo kaka na dada wengi katika kila sehemu ya dunia wanalazimika kuvuka ili kufikia lengo lao.”

Baba Mtakatifu Francisko vile vile alisema: na "jangwa" sio tu la mchanga na matuta, au miamba, lakini pia maeneo yote ambayo hayafikiki na hatari, kama vile misitu, vichaka, nyika ambapo wahamiaji hutembea peke yao, wameachwa peke yao. Kwa njia hiyo Papa amefafanua mambo matatu: Wahamiaji, bahari na jangwa. Njia za uhamaji za leo hii mara nyingi zina alama ya kuvuka bahari na majangwa, ambayo kwa watu wengi sana ni mbaya. Ndiyo maana leo hii ninataka kuakisi janga hili na  maumivu haya. Tunajua baadhi ya njia hizi vizuri zaidi, kwa sababu mara nyingi huwa zinaakisiwa; wengine, wengi wao, wanajulikana kidogo, lakini si siyo kidogo. Papa amesisitiza jinsi ambavyo amezungumzia “juu ya Mediterania mara nyingi, kwa sababu mimi ni Askofu wa Roma na kwa sababu ni ishara: Bahari Yetu, mahali pa mawasiliano kati ya watu na ustaarabu, imekuwa kaburi.”

Papa wakati wa katekesi yake
Papa wakati wa katekesi yake

Na janga ni kwamba wengi, na wingi wa vifo hivi, wangeweza kuokolewa. Ni lazima kusema wazi: kuna wale wanaofanya kazi kwa utaratibu na kwa kila njia ya kukataa wahamiaji. Na hili, linapofanywa kwa dhamiri na wajibu, ni dhambi kubwa. Tusisahau kile ambacho Biblia inasema: “Usimdhulumu mgeni wala kumkandamiza” (Kut 22:20). Yatima, mjane na mgeni ni watu walio duni ambao Mungu huwatetea na kututaka tuwatetee. Hata baadhi ya jangwa, kwa bahati mbaya, huwa makaburi ya wahamiaji. Na hata hapa mara nyingi hatushughulikii vifo vya "asili". Hapana.” Papa Francisko amefafanua: " Wakati wengine katika Jangwa waliwapelekwa hapo na kuwaacha. Sote tunajua picha ya mke na binti wa Pato, wakifa kwa njaa na kiu jangwani. Katika nyakati za satelite na droni, kuna wanaume wahamiaji, wanawake na watoto ambao hakuna mtu anayepaswa kuwaona: wanawaficha. Mungu pekee ndiye anayewaona na kusikia kilio chao. Na huu ni ukatili wa ustaarabu wetu.”

Kiukweli, bahari na jangwa pia ni sehemu za kibiblia zilizojaa thamani ya mfano. Ni matukio muhimu sana katika historia ya kutoka, uhamiaji mkubwa wa watu walioongozwa na Mungu kupitia Musa wakitoka Misri hadi Nchi ya Ahadi. Maeneo haya yanashuhudia janga la kutoroka kwa watu, wanaotoroka kutokana na dhuluma na utumwa. Ni mahali pa mateso, hofu na  kukata tamaa, lakini wakati huo huo ni mahali pa kupita kwa ukombozi  na ni watu wangapi wanapita baharini, majangwa ili kujikomboa leo hii. Papa amesisitiza tena “Ni mahali pa kupita kwa ukombozi, kufikia uhuru na utimizo wa ahadi za Mungu”(Rej.Ujumbe wa Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi duniani 2024).

Papa akisalimiana na makundi ya walioudhuria katekesi
Papa akisalimiana na makundi ya walioudhuria katekesi

Kuna Zaburi ambayo, ikimwambia Bwana, kwamba: “Njia yako iko baharini / mapito yako juu ya maji mengi” (Zab77,20). Na mwingine anaimba hivi: “Aliongoza watu wake jangwani, / kwa sababu upendo wake ni wa milele” (Zab 136,16). Maneno haya matakatifu yanatuambia kwamba, ili kuwasindikiza watu katika njia ya uhuru, Mungu mwenyewe anavuka bahari na jangwa; Mungu hakai mbali, hapana, anashiriki majanga haya ya wahamiaji, Mungu yu pamoja nao, pamoja na wahamiaji anateseka nao, analia na kutumaini pamoja nao hao wahamiaji.”

Itatufaa kufikiria leo hii kwamba: Bwana yu pamoja na wahamiaji wetu katika ‘nostrum ya mare’, yaani ‘bahari yetu’, Bwana yu pamoja nao, sio pamoja na wale wanaowakataa.” Kutokana na hilo Papa Francisko ameisitiza kwa waamini na mahujaji kaka na dada kwamba “sote tunaweza kukubaliana juu ya jambo moja: katika bahari na majangwa hayo hatari, wahamiaji wa siku hizi hawapaswi kuwepo na  kwa bahati mbaya wapo. Lakini sio kupitia sheria zenye vizuizi zaidi, sio kwa uwekaji kijeshi wa mipaka, sio kwa kukataliwa ndipo tutafikia matokeo haya. Badala yake tutafanikisha hili kwa kupanua njia salama za kufikia na njia za kufikia mara kwa mara kwa wahamiaji, kuwezesha hifadhi kwa wale wanaokimbia vita, ghasia, mateso na majanga mengi; tutafanikisha hili kwa kuendeleza kwa kila namna utawala wa kimataifa wa uhamiaji unaozingatia haki, udugu na mshikamano. Na kwa kuunganisha nguvu kupambana na biashara haramu ya binadamu, kukomesha wasafirishaji wahalifu ambao wanatumia vibaya mateso ya wengine bila huruma.

Furaha ya kusalimia na kupiga picha na makundi
Furaha ya kusalimia na kupiga picha na makundi

Papa Francisko ameendelea kusema kuwa: “Wapendwa kaka na dada, fikiria majanga mengi ya wahamiaji: ni wangapi wanakufa katika Mediterania. Fikiria Lampedusa, Crotone... ni mambo mangapi mabaya na ya kusikitisha.” Kwa kuhitimisha Papa amesema amalizie “kwa kutambua na kupongeza dhamira ya wasamaria wema wengi, wanaofanya kila wawezalo kusaidia na kuokoa wahamiaji waliojeruhiwa na kutelekezwa katika njia za matumaini yaliyokata tamaa, katika mabara matano. Wanaume na wanawake hawa jasiri ni ishara ya ubinadamu ambao haujiruhusu kuambukizwa na tamaduni mbaya ya kutojali na ubadhirifu: Papa aliongeza: "kinachoua wahamiaji ni kutojali kwetu na tabia hiyo ya kuwatupilia mbali.”

Askofu wa Roma alisema: "Na wale ambao hawawezi kuwa kama wao “kwenye mstari wa mbele - ninafikiria watu wengi wazuri ambao wako mstari wa mbele, wa  Huduma ya kibinadamu ya kuokoa ya Mediterranea na vyama vingine vingi vya juu, hawajatengwa na mapambano haya ya ustaarabu kwa sababu hiyo, hatuwezi kuwa mstari wa mbele lakini hatujatengwa; kuna njia nyingi za kutoa mchango wetu kwanza kabisa maombi. Papa Francisko  ameuliza swali: “je, mnawaombea wahamiaji hawa wanaokuja katika nchi zetu kuokoa maisha yao? Na ninyi mnataka kuwafukuza? Wapendwa kaka na dada, tuunganishe mioyo na nguvu zetu ili bahari na majangwa yasiwe makaburi, bali ziwe nafasi ambapo Mungu anaweza kufungua njia za uhuru na udugu."

Katekesi ya Papa 28 Agosti
28 August 2024, 10:53