Mfungwa aliyehukumiwa kifo Mfungwa aliyehukumiwa kifo 

Papa:hukumu ya kifo haileti haki,ni sumu kwa jamii

Mkristo katika hukumu ya kifo.Juhudi zangu karibu na waliohukumiwa,ni kichwa cha kitabu cha Dale Racinella,toleo la I la LEV,kitachapishwa Agosti 27,na dibaji ya Papa Francisko.Mwandishi Recinella,miaka 72 aliwahi kuwa Wakili maarufu wa Wall Street.Tangu 1998 anasindikiza kiroho waliohukumia kifo katika Magereza ya Florida pamoja na mkewe Susan.Kitabu kinasimua uzofu wa kukutana na Yesu.

Papa Francisco

Injili ni kukutana na Mtu hai ambaye anabadili maisha: Yesu ana uwezo wa kubadilisha mipango yetu, mitazamo yetu na matarajio yetu. Kumjua Yeye, ina maana ya kujaza maana ya kuishi kwetu kwa sababu, Bwana anatoa furaha ambayo haiishi. Kwa sababu ni furaha ile ya Mungu. Matukio ya kibinadamu ya Dale Recinella, ambaye nilikutana naye kwenye mkutano, nilimjua vema kupitia makala zake alizoandika kwa miaka katika Gazeti la “Osservatore Romano” na sasa kwa njia ya kitabu hiki kinagusa moyo na ni uthibitisho kwa kile alichosema: “Ni kwa njia hiyo tu inawezakana kueleza jinsi ilivyowezekana kwamba mwanadamu na malengo mengine mengi akilini ya kufikia katika siku zijazo, nimekuwa msimamizi wa kikanisa, kutanzia mlei mkristo, mwanaume wa ndoa na baba wa waliohukumiwa hukumu ya kifo.”

Kitabu cha Dale Recinella "Mkirsoto katika hukomu ya  Kifo
Kitabu cha Dale Recinella "Mkirsoto katika hukomu ya Kifo

Ni kazi ngumu sana, ya hatari na vigumu kufanya mazoezi, kwa sababu inagusa uovu katika vipimo vyake vyote: uovu uliofanyika kwa waathirika,  ambao hauwezi kukarabatiwa; uovu ambao mhukumiwa yuko anaishi, kwa kujua kamba hatua ya kifo ni ya uhakika: uovu ambao kwa mazoezi ya hukumu ya kifo, imewekwa katika jamii. Ndiyo kama nilivyosema mara nyingi, hukumu ya kifo siyo namna ya kuleta suluhisho mbele ya vurugu ambayo inaweza kuwakumba watu wasio na hatia. Kufanya mazoezi ya adhabu ya kifo, mbali na kutenda haki, huchochea hisia ya kulipiza kisasi ambayo inageuka kuwa sumu hatari kwa mwili wa jamii zetu za kiraia. Serikali zinapaswa kushughulikia, kwa kuruhusu wafungwa uwezekano wa kubadili hali halisi, zaidi ya kuwekeza fedha na rasilimali katika kuwakandamiza, kana kwamba ni wanadamu ambao hawastahili tena kuishi na hivyo kutupwa.

Katika riwaya yake ya (L‘idiota Fëdor Dostoevskij)-(Mjinga Fyodor Dostoevsky) anafupisha kwa namna  hii juu ya  hukumu ya kifo ya kutokuwa endelevu kimantiki na kimaadili, akizungumzia mtu aliyehukumiwa adhabu ya kifo.” Ni ukiukwaji wa roho ya binadamu, hakuna kingine! Na ilisemwa “Usiue,” na badala yake kwa sababu aliua, na wengine wanaua yeye.” Hapana, ni kitu ambacho hakipaswi kuwapo.” Ni katika Jubilei kwa hakika inabidi kutia juhudi ya waamini wote ili kuomba kwa sauti moja, ya kuondoa adhabu ya kifo, mazoezi ambayo kama isemavyo Katekisimu ya Kanisa Katoliki: “hairuhusiwi kwa sababu isishambulie na kudhulu hadhi ya utu wa mtu!” (KKK 2267).

Dale Recinella na Kenny
Dale Recinella na Kenny

Zaidi ya hayo, tendo la Dale Recinella, bila kusahau umuhimu wa msaada wa mkewe Susan, kama inavyoonesha wazi katika Kitabu ni zawadi kubwa kwa Kanisa na kwa ajili ya Jamii ya Marekani, mahali ambapo Dale anaishi na kutenda. Kujitolea kwake kama mlei, katika sehemu isiyo na ubinadamu hasa kama vile kunyongwa, ni ushuhuda hai na wa shauku kwa shule ya huruma ya Mungu isiyo na kikomo, kama vile Jubilei ya kawaida ya Huruma ilivyotufundisha, hatupaswi kamwe kufikiria kwamba kunaweza kuwa na  dhambi zetu, kosa letu au tendo letu ambalo hakika hutuweka mbali na Bwana. Moyo wake tayari umesulubishwa kwa ajili yetu. Na Mungu anaweza tu kutusamehe.

Bila shaka, huruma hii isiyo na kikomo ya kimungu inaweza pia kuwachukiza, kwani iliwashtua watu wengi wakati wa Yesu, wakati Mwana wa Mungu alipokula pamoja na wenye dhambi na makahaba. Ndugu Dale mwenyewe anapaswa kukabiliana na ukosoaji, malalamiko na kukataliwa kwa kujitolea kwake kiroho pamoja na waliohukumiwa kifo. Lakini je, si kweli kwamba Yesu alimkaribisha katika kumbatio lake mwizi aliyehukumiwa kifo? Naam, Dale Recinella ameelewa kweli na kushuhudia kwa maisha yake, kila wakati anapopita mlango wa gereza, hasa kile anachoita "nyumba ya kifo", kwamba upendo wa Mungu hauna mipaka na hauna kipimo. Na kwamba hata dhambi zetu mbaya zaidi haziharibu utambulisho wetu machoni pa Mungu: tunabaki kuwa watoto wake, tunapendwa naye, tunalindwa naye na kuchukuliwa kuwa wa thamani.

Kwa hiyo ningependa kusema asante za dhati na za kugusa moyo kwa Dale Recinella: kwa sababu kitendo chake kama mhudumu wa kikanisa kwenye mstari wa kunyongwa ni mshikamano wa dhati na wa shauku kiukweli wa ndani kabisa wa Injili ya Yesu, ambayo ni huruma ya Mungu, upendo bila malipo, na kutochoka kwa kila mtu, hata kwa wale ambao wamefanya makosa. Na kwamba hasa kutokana na mtazamo wa upendo, kama ule wa Kristo msalabani, wanaweza kupata maana mpya katika kuishi kwao na, pia, katika kufa kwao.

DIBAJI YA PAPA KATIKA KITABU JUU YA HUKUMU YA KIFO

 

 

18 August 2024, 09:52