Papa kwa Maaskofu wa Kanda za Kiarabu:Muwe ishara za matumaini hai
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 28 Agosti 2024 amekutana na wajumbe wa Baraza la Maaskofu wa Kilatini katika Kanda za Kiarabu. Katika hotuba yake amefurahi kukutana nao katika fursa ya mkutano wao wa mwaka ambao unafanyika katika siku hizi jijini Roma. Baba Mtakatifu Francisko akimulia maeneo watokayo amesema “Mashariki ya Kati inakabiliwa na nyakati za mvutano mkali sana, ambao katika baadhi ya mazingira husababisha mapigano ya wazi na vita. Mgogoro huo, badala ya kutafuta suluhisho la haki, unaonekana kuwa sugu, na hatari ya kusambaa hadi kuwasha moto eneo zima. Hali hii imesababisha maelfu na maelfu ya vifo, uharibifu mkubwa, na mateso makubwa na kuenea kwa hisia za chuki na hasira, ambazo huandaa mazingira ya majanga mapya.”
Baba Mtakatifu aidha akikumbuka yale aliyosema baada ya katekesi yake: “Leo nimepata nafasi ya kueleza moja kwa moja ukaribu wangu kwenu na kwa Makanisa mnayowakilisha. Bwana awapatie nguvu kila wakati kushuhudia imani yenu kwake, pia kwa mazungumzo ya heshima na ya dhati na kwa wote. Mnaweza kuweka tumaini hai! Iweni wenyewe, kwa kila mtu, ishara za matumaini, uwepo mnaolisha maneno na ishara za amani, za udugu, za heshima. Uwepo ambao, wenyewe, unaalika busara, upatanisho, kushinda kwa nia njema migawanyiko na uadui uliogawanyika na kuwa mgumu kwa muda, ambao unazidi kutoweza kutenganishwa.”
Baba Mtakatifu Francisko, ameshukuru kwa sababu wao "ni mwali wa matumaini mahali ambapo unaonekana kuzimika! Na pia anawatakia mafanikio mema katika mipango yao ya uchungaji. Hasa, kwamba "wanaweza kutambua njia bora zaidi ya kuhakikisha elimu ya Kikristo ya kutosha kwa wanafunzi wa shule za umma, katika mazingira ambapo uwepo wa Wakristo ni wachache. Malezi haya yana umuhimu mkubwa, ili yaliyomo katika imani yajulikane na kuambatana na tafakari na hivyo imani, kwa kulinganisha na utamaduni, inaweza kuwa na nguvu na kuwa na njia ya kutoa maana kwa ajili ya matumaini ya Kikristo (taz 1 Pt 3:15). . Kwa kuhitimisha, Papa Francisko amewashukuru kwa ziara hiyo na Mama Yetu awalinde na kuwafariji. Amewabariki kutoka ndani ya moyo wake na kuomba waoombeane.