Tafuta

Mabadiliko yanayoletwa na mapinduzi ya habari,kwa mfano,ukuzaji wa akili mnemba na maendeleo ya  sayansi,yanalazimisha binadamu wa leo kufikiria upya utambulisho wao, ukumu lao katika ulimwengu na jamii na wito wao kuvuka mipaka. Mabadiliko yanayoletwa na mapinduzi ya habari,kwa mfano,ukuzaji wa akili mnemba na maendeleo ya sayansi,yanalazimisha binadamu wa leo kufikiria upya utambulisho wao, ukumu lao katika ulimwengu na jamii na wito wao kuvuka mipaka.  (ANSA)

Papa:Mabadiliko ya kianthropolojia ni mapinduzi ya kweli!

Mbele ya kukabiliwa na mapinduzi ya kianthropolojia yanayoendelea haiwezekani kuguswa tu na kukataa na kukosolewa.Badala yake,tafakari ya kina inahitajika,inayoweza kufanya upya fikra na maamuzi yatakayof anywa.Changamoto hii inawagusa Wakristo wote.Na hii ni pamoja na Warthodox.Ni katika ujumbe wa Papa kwa washiriki wa Warsha ya XVII ya Wakristo huko Trani,Agosti 28-30.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ametuma Ujumbe kwa washiriki wa Warsha ya XVII Wakristo ( Inter-Christian) kwa Kardinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo. Katika hisia za ukaribu mzuri ametoa salamu zake  kwa wazungumzaji mashuhuri na kwa wote walioandaa pamoja na Taasisi kiroho ya Kifranciskani ya Chuo Kikuu cha Antonianum na Kitengo cha Kitaalimungu ya Kiorthodox cha Chuo Kikuu cha “Aristoteles” cha  Salonicco, kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti 2024 huko Trani, kwa kuongoza na tema “ Binadamu ni nani” (Zab  (Sal 8,5)  katika wakati wa mabadiliko ya anthropolojia.”  Kwa namna ya pekee Papa amewapongeza waandaaji wa uzoefu wa dhati wa ushirikiako kati ya wakatoliki na waorthodox ambao sasa imekuwa tamaduni nzuri.

Mapinduzi ya habari

Kichwa cha Warsha kinazungumza juu ya wakati wa mabadiliko ya kianthropolojia, lakini kile kinachotokea leo hii kinaweza kufafanuliwa kama mapinduzi ya kweli. Mabadiliko yanayoletwa na mapinduzi ya habari, kama vile, kwa mfano, ukuzaji wa akili mnemba na maendeleo ya ajabu ya sayansi, yanalazimisha wanaume na wanawake wa leo kufikiria upya utambulisho wao, jukumu lao katika ulimwengu na katika jamii na wito wao kuvuka mipaka. Kwa hakika, umaalumu wa mwanadamu katika uumbaji wote, upekee wake ikilinganishwa na wanyama wengine, na hata uhusiano wake na mashine, unatiliwa shaka daima. Zaidi ya hayo, jinsi wanaume na wanawake wa leo hii wanavyoelewa uzoefu wa kimsingi wa kuwepo kwao, kama vile kuzalisha, kuzaliwa, kufa, inabadilika kimuundo.

Changamoto inawagusa Wakristo

Mbele yakukabiliwa na mapinduzi haya ya anthropolojia yanayoendelea haiwezekanikuguswa tu na kukataa na kukosolewa. Badala yake, tafakari ya kina inahitajika, inayoweza kufanya upya fikra na maamuzi yatakayofanywa (tazama Ujumbe wa Video kwenye hafla ya Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni kuhusu mada "Kuelekea Ubinadamu unaohitajika", 23 Novemba 2021). Changamoto hii inawagusa Wakristo wote, Kanisa lolote walilo nalo. Kwa sababu hii inavutia sana kwamba Wakatoliki na Kiorthodox wanaendeleza tafakari hii pamoja. Hasa, kwa kuzingatia mafundisho ya Maandiko Matakatifu na Mapokeo ya Kikristo, ni muhimu kurudia kwamba kila mwanadamu anastahili hadhi kwa ukweli wa kuwepo, kama chombo cha kiroho, kilichoundwa na Mungu na kilichowekwa kwa uhusiano wa Umwana na Yeye ( rej Ef 1,4-5),bila kujali kama anatenda kwa mujibu wa hadhi yake mwenyewe, hali ya kijamii na kiuchumi anamoishi au hali yake ya kuwepo.

Baba Mtakatifu amesema: "Utetezi wa heshima hii dhidi ya matishio madhubuti kama vile umaskini, vita, unyonyaji na vingine vinawakilisha dhamira ya pamoja kwa Makanisa yote, ambayo kwayo yatafanya kazi pamoja. BabaMtakatifu anawasindikiza katika  na warasha hili la  XVII la Wakristo pamoja na sala zake na, kwa maombezi ya Mtakatifu Nicola Pellegrino, Mlinzi Mtakatifu wa Trani. Na amewaombea baraka za Bwana kwa washiriki wote, akiamini kwamba wao pia watakuwa na wema wa kukumbuka yeye katika maombi yao."

Papa ametuma Ujumbe kwa washiriki wa Warsha huko Trani

 

28 August 2024, 12:27