Papa kwa Wanasheria:Tunahitaji kuamua,mazungumzo,upatanisho na suluhisho!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 24 Agosti 2024, alikutana na Wajumbe wa wa Kimataifa wa Wanasheria Kikatoliki katika fursa ya Mkutano wao wa 15 wa Mwaka. Amemsalimia Kardinali Christoph Schönborn na Dk. Christiaan Alting von Geusau, na kushukuru maneno ya utungulizi wake ambao aliusoma mapema kwa sababu ya kuokoa muda ili kupata muda zaidi wa kuzungumza nao. Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu waliyochagua ni: "Dunia katika vita: migogoro ya kudumu na vurugu.” Baba Mtakatifu ameuliza: "je ina maana gani kwetu?, ni muhimu zaidi kuliko hapo awali. Hali ya sasa ya vita vya tatu vya dunia vilivyo gawanyika vipande vipande na vipo kweli ambavyo vinaonekana kuwa vya kudumu na visivyozuilika.
Mgogoro unaoendelea unatishia pakubwa juhudi za subira zinazofanywa na jumuiya ya kimataifa, hasa kupitia diplomasia ya kimataifa, kuhimiza ushirikiano katika kushughulikia dhuluma kubwa na kusukuma mbele changamoto za kijamii, kiuchumi na kimazingira zinazoikabili familia ya binadamu. Na ndivyo hivyo zinazidi, Papa Francisko amesisitiza. Lakini Je, basi, ni mwitikio gani unaotarajiwa, si tu kutoka kwa wanasheria, bali kutoka kwa wanaume na wanawake wote wenye mapenzi mema, hasa wale waliochochewa na maono ya Kiinjili ya umoja wa familia ya binadamu na wito wake wa kujenga ulimwengu kutunza bustani(Mwa 2:15; Is 61:11) - yenye sifa ya udugu, haki na amani? Hili ndilo swali. Katika hili Papa Francisko ameomba atoa maoni kadhaa kuhusu tafakari ya mada yao.
Kwanza kabisa Papa amesisitiza kuwa kuna“ umuhimu wa kuacha vita kama njia ya kutatua migogoro na kuanzisha haki. Tusisahau kwamba “kila vita huiacha dunia ikiwa mbaya zaidi kuliko ilivyoikuta. Hii ni kwa hakika na tuna uzoefu nayo. Vita ni kushindwa kwa siasa na ubinadamu, ni kujisalimisha kwa aibu, kushindwa mbele ya nguvu za uovu (Wataka wa kitume wa Fratelli tutti, 261). Kujisalimisha sio nchi moja kuelekea nyingine, kujisalimisha ni vita yenyewe. Kweli ni kushindwa. Kiukweli, uwezo mkubwa wa uharibifu wa silaha za kisasa umefanya vigezo vya jadi vya kuzuia vita kuwa vya kizamani. Katika hali nyingi, tofauti kati ya malengo ya kijeshi na ya kiraia yanazidi kuwa na ukungu. Dhamiri zetu haziwezi kujizuia kuguswa na matukio ya kifo na uharibifu ambayo tunaona mbele ya macho yetu kila siku. Tunahitaji kusikiliza kilio cha maskini, cha wajane na yatima ambacho Biblia inazungumza, ili kuona shimo la uovu ambalo liko katikati ya vita na kuamua kwa kila njia iwezekanayo kuchagua amani.
Pili Baba Mtakatifu amebainisha kuwa hitaji la ustahimilivu na subira, ile methali ya ‘fadhila ya wenye nguvu’, katika kutafuta njia ya amani, katika kila tukio linalofaa na lisilofaa, kwa njia ya mazungumzo, upatanisho na suluhisho. “Mazungumzo […] lazima yawe roho ya jumuiya ya kimataifa” (Hotuba kwa Wanadiplomasia, 8 Januari 2024), ikiwezeshwa na uaminifu mpya katika miundo ya ushirikiano wa kimataifa. Licha ya ufanisi wao, uliothibitishwa kwa miaka mingi, katika kukuza juhudi za kimataifa kwa ajili ya amani na heshima kwa sheria za kimataifa, miundo hii daima inahitaji marekebisho na upya ili kukabiliana na hali ya sasa, kwa hali mpya. Katika suala hili, umakini maalum lazima ulipwe katika kuunga mkono sheria ya kimataifa ya kibinadamu na kuipatia misingi thabiti ya kisheria. Hili kwa kawaida linahitaji kufanyia kazi mgawanyo unaozidi kuwa sawa wa bidhaa za dunia, kuhakikisha maendeleo shirikishi ya watu binafsi na watu, na hivyo kuondokana na ukosefu wa usawa wa kashfa na ukosefu wa haki unaochochea migogoro ya muda mrefu na kuzalisha makosa zaidi na vitendo vya vurugu duniani kote.
Katika uzoefu wao wa kila siku wa wanasheria wakatoliki na viongozi wa kisiasa, wanajua pia maana ya kukabili migogoro, kwa kiwango kidogo, lakini labda kikubwa zaidi, ndani ya jumuiya wanazowakilisha na kuzitumikia. Kama Wakristo, Papa ameongeza kusema “tunatambua kwamba mizizi ya migogoro, mgawanyiko na ubaguzi wa jamii lazima utafutwe, hatimaye, kama Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican ulivyosisitiza, katika mzozo wa kina, uliopo ndani ya moyo wa mwanadamu (rej.Katiba ya Gaudium et spes,10). Wakati mwingine migogoro inaweza kuepukika, lakini itawezekana kusuluhisha kwa matunda katika roho ya mazungumzo na usikivu kwa wengine na sababu zao, na kwa kujitolea kwa pamoja kwa haki katika kutafuta faida ya wote. Papa alitoa mkazo kuwa: “Msisahau hili: huwezi kutoka kwenye mgogoro peke yako. Hapana. Unatoka na wengine. Peke yako, hakuna mtu yeyote anayeweza kutoka nje ya mzozo.”
Hatimaye, Papa Francisko akiwatakia heri kwa ajili ya mazungumzo yao kwa maombi, akipenda kuruhusiwa na pengine kuliko kitu kingine chochote, ulimwengu wetu uliochoshwa na vita kwamba inaonekana hauwezi kuishi bila vita na hivyo unahitaji kufanya upya roho ya matumaini ambayo yalipelekea kuanzishwa kwa miundo ya ushirikiano katika huduma ya amani baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Papa amependa kuwaomba wao ambao utumishi wao kwa kaka na dada zetu wanatiwa msukumo na kuungwa mkono na amani hiyo ambayo ulimwengu hauwezi kutoa (rej.Yh 14:27), kuwa mashuhuda wa matumaini, hasa kwa vizazi vipya. Vita sio tumaini, vita haitoi tumaini. Jitoleeni kwenu kwa manufaa ya wote, kukiungwa mkono na imani katika ahadi za Kristo, kiwe kielelezo kwa vijana wetu.”
Ni muhimu jinsi gani kwao kuona mifano ya matumaini na maadili ambayo yanapingana na jumbe za kukata tamaa na kutokuwa na matumaini – “tusisahau jumbe za kejeli: ni za kutisha! - na mara nyingi vijana wanaoneshwa ujumbe huu wa kukata tamaa, kutokuwa na wasiwasi! Kwa kifupi, kwa sisi tunaoishi katika dunia yenye vita, yenye migogoro na kinzani za kudumu. Inahusu kupata hekima na nguvu za kuona ng'ambo ya mawingu, kusoma alama za nyakati na kwa matumaini yanayotokana na imani, kuwatia moyo wengine, hasa vijana, kufanya kazi kwa ajili ya kesho iliyo bora. Na kwa hisia hizo, Papa aliwahakikishia maombi yake kwa ajili yao na kwa ajili ya familia zao na kwa wale watakaowatumikia. Papa amehitimisha kwa kuwabariki kwa baraka kutoka ndani ya moyo wake na kuomba tafadhali wamwombee.