Papa:ujumbe wa matumaini kwa watu wa China,mwalimu wa matumaini
Na Isabella Piro na Angella Rwezaula – Vatican.
Moyo wa mahojiano yaliyotolewa na Baba Mtakatifu Francisko kwa Padre Pedro Chia, mkurugenzi wa Ofisi ya waandishi wa habari wa Shirika la Yesu, Jimbo la China katika Maktaba ya Jumba la Kitume, ni ‘ujumbe wa matumaini’ na baraka kwa watu wote hasa watu wa China. Katika mahojiano hayo yaliyochapishwa kwenyemitandao husika za kijamii, yalifanyika mnamo tarehe 21 Mei 2024, ikiwa ni kumbukumbu ya Bikira Maria Msaada wa Wakristo, mlinzi wa Madhabahu ya Sheshan, huko Shanghai. Na ni hasa katika Madhabahu hayo ambapo Papa Francisko anataka kwenda, kama alivyosema katika mazungumzo, yenye sifa ya mbinu dhabiti ya kiroho na kuakisiwa na kumbukumbu za kibinafsi za Papa na tafakari yake kwa mustakabali wa Kanisa.
Kupeleka mbele urithi wake
Katika nchi ya Asia, Papa Francisko alisema, angependa kukutana na maaskofu mahalia na watu wa Mungu ambao ni waaminifu sana. Hao ni watu waaminifu. Wamepitia mambo mengi na wameendelea kuwa waaminifu.” Kwa Wakatoliki Vijana wa China, hasa, Papa alisisitiza tena dhana ya tumaini, hata kama, “inaonekana kuwa mbaya kwangu kutoa ujumbe wa matumaini kwa watu ambao ni waalimu wa matumaini na uvumilivu wakati wa kusubiri. Na hili, ni jambo zuri sana. Wachina ni watu wakuu ambao lazima wasipoteze urithi wao, kinyume chake lazima iendeleze mbele urithi wake kwa subira."
Ukosoaji na upinzani unasaidia
Wakati wa mahojiano, Papa pia alizingatia upapa wake, uliofanywa kwa ushirikiano, kusikiliza na kushauriana na wakuu wa Mabaraza ya Kipapa na kila mtu. “Kukosoa kila wakati kunasaidia, hata kama sio kujenga, kwa sababu siku zote ni muhimu, hutufanya tutafakari juu ya jinsi tunavyotenda. Na nyuma ya upinzani kunaweza kuwa na ukosoaji mzuri. Wakati mwingine inabidi kusubiri na kuvumilia hata kwa uchungu kama unapopata upinzani dhidi ya Kanisa, kama inavyotokea wakati huu kutoka katika makundi madogo.” Papa alikazia kuwa “Nyakati za shida au ukiwa daima hutatuliwa kwa faraja ya Bwana.”
Vita na changamoto zingine
Kuhusu changamoto nyingi zilizopatikana hadi sasa kwenye kiti cha Kharifa wa Mtume Petro, Papa alikumbuka hasa changamoto kubwa ya janga la uviko, na changamoto ya sasa ya vita, hasa huko Ukraine, Myanmar na Mashariki ya Kati. Siku zote mimi hujaribu kusuluhisha kupitia mazungumzo. Na wakati haifanyi kazi, inabidi kuwa na subira na pia kwa hali ya ucheshi, kulingana na mafundisho ya Mtakatifu Thomas More.”
Migogoro ya kibinafsi hapo awali
Katika ngazi ya kibinafsi, Papa alikumbuka kuwa alipitia baadhi ya migogoro wakati wa maisha yake ya kitawa kama Mjesuit. Ni ukweli wa kawaida, vinginevyo isingekuwa mwanadamu. Lakini mikasa inashindwa kwa njia mbili: inafuatwa na kuvuka kama kupitia njia isiyo na mwisho (labyrinth), ambayo mtu hutokea juu, na kisha mtu hatoki peke yake, lakini anasaidiwa, akisindikizwa, kwa sababu ukijiruhusu kusaidiwa ni muhimu sana.” Kwa Bwana, Papa Fransisko aliendelea kusema, “Ninaomba neema ya kusamehewa na anivumilie.”
Mafungo ya kiroho, maskini, vijana, nyumba ya kawaida
Baba Mtakatifu pia alimulika juu ya mapendeleo manne ya kitume ya Wanashirika wa Wajesuit, yaliyooneshwa mnamo mwaka 2019 kwa miaka kumi ijayo: kukuza mafungo ya kiroho na utambuzi, kutembea na maskini na waliotengwa, kusindikiza vijana katika kujenga mustakabali wa matumaini na kutunza nyumba ya wote ya kawaida. Hizi ni kanuni nne “zilizounganishwa ambazo haziwezi kutenganishwa,” Papa, pia alisisitiza kwamba usindikizaji, utambuzi na roho ya kimisionari ndiyo msingi wa Jumuiya ya Yesu.
Ukleri na ulimwengu, mapigo mawili ya Kanisa
Kwa hiyo, akitazama mustakabali wa Kanisa, Papa Francisko alikumbusha kwamba, kulingana na baadhi ya watu, itakuwa kidogo zaidi na itabidi"kuwa waangalifu ili wasianguke katika pigo la ukasisi na ulimwengu wa kiroho ambao unawakilisha, katika maneno ya Kardinali Lubac “uovu mbaya zaidi ambao unaweza kulipiga Kanisa, mbaya zaidi kuliko wakati wa mapapa wa masuria" alinikuu Papa. Hatimaye, Baba Mtakatifu Fransisko alimkumbusha yule ambaye atakuwa mrithi wake kwenye kiti cha Mtume Petro juu ya "umuhimu wa kusali, kwa sababu Bwana hunena katika maombi.”