Mtandao wa Kikanisa wa Jumuiya Zilizopangwa “Red Eclesial de Comunidades Organizadas”, Jumatano tarehe 28 Agosti 2024 umekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Mtandao wa Kikanisa wa Jumuiya Zilizopangwa “Red Eclesial de Comunidades Organizadas”, Jumatano tarehe 28 Agosti 2024 umekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican.  

Sera na Mbinu Mkakati wa Kumwilisha Mafundisho Jamii ya Kanisa

Mtandao wa Kikanisa wa Jumuiya Zilizopangwa “Red Eclesial de Comunidades Organizadas”, Jumatano tarehe 28 Agosti 2024 umekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Hii ni jumuiya inayoundwa na waamini walei, makleri na watawa. Ni mtandao unaopania pamoja na mambo mengine, kutekeleza kwa vitendo Mafundisho Jamii ya Kanisa, ili kuleta mtindo wa maisha unaosimikwa katika tunu za Kiinjili kwa ajili ustawi, mafao na maendeleo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mtandao wa Kikanisa wa Jumuiya Zilizopangwa “Red Eclesial de Comunidades Organizadas”, Jumatano tarehe 28 Agosti 2024 umekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Hii ni jumuiya inayoundwa na waamini walei, makleri na watawa. Ni mtandao unaopania pamoja na mambo mengine, kutekeleza kwa vitendo Mafundisho Jamii ya Kanisa, ili kuleta mtindo wa maisha unaosimikwa katika tunu msingi za Kiinjili. Mafundisho Jamii ya Kanisa yanapata chimbuko lake mintarafu kanuni na muundo wa elimu fahamu, taalimungu, hususan taalimungu maadili ambayo ni dira na mwongozo wa maisha ya watu. Yanachota amana na utajiri wake kutoka katika Maandiko Matakatifu na Mapokeo ya Kanisa na imani thabiti ambayo inamwilisha Neno la Mungu katika matendo, kielelezo cha imani tendaji. Mambo msingi katika mchakato wa kudumisha haki msingi za binadamu: Amani katika ukweli, haki, upendo na uhuru.

Tume ya Kipapa Kwa Ajili ya Amerika ya kusini: Changamoto za uinjilishaji
Tume ya Kipapa Kwa Ajili ya Amerika ya kusini: Changamoto za uinjilishaji

Hizi ni tunu ambazo ni urithi mkubwa kwa binadamu wote kwani zinabubujika kutoka katika asili ya binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu hivyo zinapaswa kulindwa, kutetewa na kuheshimiwa na wote; kwa kuzingatia kwamba, haki inakwenda sanjari na wajibu; hakuna haki pasi na wajibu. Hii ni haki ya kuishi, kupata huduma bora ya makazi, afya, elimu, kuabudu, uhuru wa dhamiri, uhuru wa kuchagua mfumo wa maisha; haki za kiuchumi na kisiasa pamoja na uhuru wa kwenda unakotaka kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo. Kanisa Katoliki lina amana na utajiri mkubwa wa Mafundisho Jamii ya Kanisa yanayopata chimbuko lake katika Waraka wa Kichungaji wa Baba Mtakatifu Leo XIII; Mambo Mapya; Rerum Novarum. Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake amekazia pamoja na mambo mengine, ujenzi wa jamii inayosimikwa katika tunu msingi za kiinjili kwa ajili ya ustawi, maendeleo na wokovu wa roho zao.

Sera na mchakato wa umwilishaji wa mafundisho jamii ya Kanisa
Sera na mchakato wa umwilishaji wa mafundisho jamii ya Kanisa

Mtandao huu usaidie jamii kujenga umoja, upendo, udugu na mshikamano kwa kujali na kuguswa na mahitaji ya ndugu na jirani zao, na hasa zaidi maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Mtandao wa Kikanisa wa Jumuiya Zilizopangwa “Red Eclesial de Comunidades Organizadas” unaundwa na Makanisa, Mashirikisho ya Vyuo vikuu na kwamba, kuna ushiriki mkubwa wa waamini wa Kanisa Katoliki kama sehemu ya mchakato wa majadiliano ya kiekumene na kidini. Wawakilishi wa Taasisi ya Maeneo ya Viwanda-Magharibi/Kusini Magharibi wamekutana na Emilce Cuda, Katibu wa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini (PCAL) ili kuendeleza kazi ambayo wamekuwa wakiifanya kuhusu utekelezaji wa sera na mikakati ya kujenga madaraja kati ya nchi za Amerika ya Kusini na Amerika ya Kaskazini, kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote
Utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote

Mtandao wa Kikanisa wa Jumuiya Zilizoandaliwa (RECOR) ulizaliwa katika Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Amerika Kusini (CELAM) kunako mwaka 2021 walipokutana kwa mara ya kwanza na Baba Mtakatifu Francisko kutokana na pendekezo lililotolewa na Askofu Cantù wa Jimbo Katoliki la San Josè, Calfonia. Tangu wakati huo, wamejadili kwa kina na mapana kuhusu mamlaka fundishi ya Kanisa “Magisterium” kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko; wameendelea kujikita katika kukuza na kudumisha mawasiliano kwa kufanya mikutano miwili mmoja ni ule utakaofanyika mwaka 2025 nchini Marekani na mwingine utaadhimishwa Barani Ulaya.

Mtandao wa Kikanisa
29 August 2024, 14:36