Tafuta

Baba Mtakatifu katika ujumbe huu anasema, anaungana na washiriki wote katika maisha ya kiroho na sala. Baba Mtakatifu katika ujumbe huu anasema, anaungana na washiriki wote katika maisha ya kiroho na sala.  

Ujumbe wa Papa Francisko Kwa Padre James Martin, SJ. Mlezi wa Lgbtq

Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi lililowasilishwa kwake na Padre James Martin, SJ, anayewahudumia watu wenye shauku ya jinsia ya aina moja nchini Marekani “LGBTQ” la kuwatakia heri na baraka katika mkutano wao ulioanza tangu tarehe 2 Agosti hadi tarehe 4 Agosti, 2024 huko kwenye Chuo Kikuu cha Georgetown, kilichoko nchini Marekani. Baba Mtakatifu katika ujumbe huu anasema, anaungana na washiriki wote katika maisha ya kiroho na sala.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Katekisimu ya Kanisa Katoliki, muhtasari wa: Imani, Sakramenti za Kanisa, Maisha adili na Sala kuhusu makosa dhidi ya usafi wa moyo inasema: “Shauku ya jinsia ya aina moja inamaanisha uhusiano kati ya wanaume au kati ya wanawake wanaoonja mvuto wa kijinsia kuelekea kwa watu wa jinsia ileile tu au wanaoonja mvuto zaidi kwa watu wa jinsia ileile. Shauku hii imechukua sura mbalimbali katika mwenendo wa karne na katika tamaduni mbalimbali. Mwanzo wake kisaikolojia unabaki kwa vikubwa hauelezeki. Yakijitegemeza katika Maandiko Matakatifu yanayaonesha matendo ya kujamiana ya jinsia moja kama matendo yenye uovu mkubwa, mapokeo yametamka daima kwamba “matendo ya kujamiana ya jinsia moja ni maovu kwa yenyewe.” Ni matendo dhidi ya sheria ya maumbile. Yanatenga paji la uhai na tendo la kijinsia. Kwa namna yoyote ile hayawezi kuidhinishwa.

Uhusiano na Lgbtq unapaswa kuwa wa heshima, huruma na uangalifu
Uhusiano na Lgbtq unapaswa kuwa wa heshima, huruma na uangalifu

Idadi ya wanaume na wanawake waliozama katika maelekeo ya shauku ya jinsia ya aina ileile sio ya kupuuzia. Hawayachagui maelekeo haya na kwa walio wengi ni swala la kujaribu. Uhusiano nao wapaswa kuwa wa heshima, huruma, na uangalifu. Kila ishara ya ubaguzi usio wa haki iepukwe. Watu hawa wanaitwa kutimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yao, na kama Wakristo, kuunganisha magumu wanayoweza kukutana nayo kutokana na hali yao na sadaka ya Msalaba wa Bwana. Watu wa shauku ya jinsia moja wanaitwa kuwa na usafi wa moyo. Kwa fadhila za kujitawala zinazowafundisha uhuru wa ndani na mara nyingine kwa kushikizwa na urafiki usiojitafuta, kwa sala na neema ya Sakramenti, wanaweza, na wanatakiwa polepole na kwa uthabiti kukaribia ukamilifu wa Kikristo.” KKK 2357-2359.

Ujumbe kwa Padre James Martin, SJ, Mlezi wa LGBTQ, USA
Ujumbe kwa Padre James Martin, SJ, Mlezi wa LGBTQ, USA

Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi lililowasilishwa kwake na Padre James Martin, SJ, anayewahudumia watu wenye shauku ya jinsia ya aina moja nchini Marekani “LGBTQ” la kuwatakia heri na baraka katika mkutano wao ulioanza tangu tarehe 2 Agosti hadi tarehe 4 Agosti, 2024 huko kwenye Chuo Kikuu cha Georgetown, kilichoko nchini Marekani. Baba Mtakatifu katika ujumbe huu anasema, anaungana na washiriki wote katika maisha ya kiroho na sala. Kristo Yesu Mkombozi wa Ulimwengu awabariki na Bikira Maria awalinde. Hii ni mara ya nne, Baba Mtakatifu Francisko kuwaandikia ujumbe na matashi mema, watu wenye maeleko ya shauku ya jinsia ya aina ileile. Baba Mtakatifu Francisko anakaza kusema, ikiwa kama watu hawa wangekutana na Kristo Yesu, kimsingi, hasinge wageuzia kisogo hata kidogo!

Padre James Martin SJ.,
03 August 2024, 14:28