Tafuta

Jumatano, tarehe 31 Julai 2024, Baba Mtakatifu Francisko aliwatembelea wasanii na wanasarakati walipo kwenye kitongoji cha Ostia, Lido Jijini Roma. Jumatano, tarehe 31 Julai 2024, Baba Mtakatifu Francisko aliwatembelea wasanii na wanasarakati walipo kwenye kitongoji cha Ostia, Lido Jijini Roma.   (ANSA)

Wasanii na Wanasarakasi ni Mashuhuda na Vyombo Vya Furaha ya Injili

Jumatano, tarehe 31 Julai 2024, Baba Mtakatifu Francisko aliwatembelea wasanii na wanasarakati walipo kwenye kitongoji cha Ostia, Lido Jijini Roma. Baba Mtakatifu amewashukuru kwa mchango wao katika kuwafurahisha watu, hasa katika kipindi hiki cha mateso na mahangaiko makubwa ya watu kutokana na vita, majanga na mahangaiko ya kijamii. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kubariki Sanamu ya Bikira Maria, Mlinzi wa Wasanii Wasafiri pamoja na Wanasarakasi hawa!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Michezo ya Sarakasi ni chanzo cha fursa za ajira kwa binadamu na wanyama wanaotumika kunogesha michezo hii. Michezo hii ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 250 kwa sasa inakabiliwa na ukata mkubwa wa fedha kutokana na athari za Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19. Wanamichezo hawa wanahitaji kuwezeshwa kiuchumi ili waweze kuendelea na shughuli zao ambazo kimsingi ni chemchemi ya furaha, amani na utulivu wa ndani. Msamaria mwema anawekwa mbele ya walimwengu kuwa ni mfano bora wa kuigwa katika kutangaza na kushuhudia Injili ya upendo kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii kutokana na utandawazi usiojali wala kuguswa na mahangaiko ya wengine. Watu washirikiane na kushikamana kwani wasanii na wanasarakasi wanateseka lakini wanataka kuanza upya kutabasamu na kuwaonjesha wengine Injili ya furaha katika maisha hasa wagonjwa na maskini.

Sanamu ya B. Maria Mlinzi wa Wasanii Wasafiri na Wanasarakasi
Sanamu ya B. Maria Mlinzi wa Wasanii Wasafiri na Wanasarakasi

Huu ni mwaliko kwa wasanii na wanasarakasi, kuanza shughuli zao, kwani kimsingi wao ni chemchemi ya furaha kwa watazamaji wao; hasa watoto na wagonjwa. Ni katika muktadha huu wa huruma, upendo na mshikamano ambapo Jumatano, tarehe 31 Julai 2024, Baba Mtakatifu Francisko aliwatembelea wasanii na wanasarakasi walipo kwenye kitongoji cha Ostia, Lido Jijini Roma. Baba Mtakatifu amewashukuru kwa mchango wao katika kuwafurahisha watu, hasa katika kipindi hiki cha mateso na mahangaiko makubwa ya watu kutokana na vita, majanga na mahangaiko ya kijamii. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kubariki Sanamu ya Bikira Maria, Mlinzi wa Wasanii Wasafiri pamoja na Wanasarakasi, muhimu sana kwa Wasanii na Wanasarakasi hawa katika maisha na utume wao.

Wasanii na Wanasarakasi ni vyombo vya furaha Injili
Wasanii na Wanasarakasi ni vyombo vya furaha Injili

Baba Mtakatifu alimtembelea pia Sr. Geneviève Jeanningros mwenye umri wa miaka 81, kwa muda wa miaka 56 anatembelea kwenye kiti cha wagonjwa, aliyekuwa ameambatana na Sr. Anna Amelia wa Shirika la Masista Wadogo wa Yesu; Jumuiya ya kitawa inayoongozwa na maisha na nyaraka za Mtakatifu Charles de Foucauld, iliyoanzishwa na Dada Mdogo Magdeleine wa Yesu (Madeleine Hutin) tarehe 8 Septemba 1939. Hawa ni watawa wanaojishughulisha na maskini pamoja na watu wote wanaosukumizwa pembezoni mwa vipaumbele vya jamii. Baba Mtakatifu amepata fursa pia ya kutembelea na kusalimiana na Wasanii pamoja na Wanasarakasi, akashuhudia baadhi ya michezo yao na mwishoni akawashukuru kwa utume wao, unaowafurahisha watu. Watoto ambao mwaka 2018 walishiriki katika Ibada ya Misa Takatifu, Sherehe ya Ekaristi Takatifu “Corpus Domini” kwenye Parokia ya Mtakatifu Monika.

Katika shida na Mungu, Mwenyezi Mungu awe ndiye kimbilio letu
Katika shida na Mungu, Mwenyezi Mungu awe ndiye kimbilio letu

Baba Mtakatifu amewashukuru na kuwapongeza watawa hawa ambao wanaendelea kujisadaka kwa ajili ya maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa vipaumbele vya jamii. Pia anawaunga mkono katika maisha na utume wao huo wenye changamoto nyingi. Isitoshe amesalimiana na wagonjwa, kundi la sala la akina Mama, ambao wameahidi kumkumbuka katika sala. Wasanii pamoja na Wanasarakasi wamemshukuru Baba Mtakatifu kwa kuwatembelea na kuwajulia hali nao kwa upande wao, wamemshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa moyo wake wa unyenyekevu. Hii ni mara ya pili, Baba Mtakatifu anawatembelea Wasanii na Wanasarakasi hawa.

Papa Ostia
01 August 2024, 14:29