Papa Francisko akabidhi ziara yake huko Asia kwa Maria Salus populi romani!
Dominika asubuhi tarehe 1 Septemba,Papa alifika kwenye Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu na akakaa kitambo kwa sala,kama kawaida,mbele ya Picha ya Bikira Salus populi romani,akimkabidhi ziara ya kitume ya Indonesia,Papua New Guinea,Timor ya Mashariki na Singapore,ambayo itaanza Jumatatu tarehe 2 Septemba 2024 mchana na itamalizika Septemba 13.
Vatican News
Kwa mujibu wa msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican kwa waandishi wa habari, Dk. Matteo Bruni amethibitisha kuwa: “Dominika asubuhi tarehe 1 Septemba, Papa Francisko alifika kwenye Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu akajikita katika sala, kama kawaida, mbele ya Picha ya Bikira Salus Populi romani,(Afya ya watu wa Roma) akimkabidhi kwake Ziara inayofuata ya Kitume kwenda Indonesia, Papua New Guinea, Timor ya Mashariki na Singapore. Mwishoni alirudi Vatican.” Hii ni safari ndefu zaidi ya upapa, itakayoanza tarehe 2 hadi 13 Septemba 2024.
01 September 2024, 11:23