Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 11 Septemba 2024 amehitimisha hija yake Kitume nchini Timor ya Mashariki na kuanza hija yake nchini Singapore, nchi ambayo iko Kusini Mashariki mwa Bara la Asia. Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 11 Septemba 2024 amehitimisha hija yake Kitume nchini Timor ya Mashariki na kuanza hija yake nchini Singapore, nchi ambayo iko Kusini Mashariki mwa Bara la Asia.  (AFP or licensors)

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Nchini Singapore: Majadiliano ya Kidini

Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 11 Septemba 2024 amehitimisha hija yake Kitume nchini Timor ya Mashariki na kuanza hija yake nchini Singapore, nchi ambayo iko Kusini Mashariki mwa Bara la Asia; inayonogeshwa na kauli mbiu “Umoja na Matumaini”, kielelezo cha umoja, ushirika, maelewano na mafungamano ya kijamii kati ya waamini na ndani ya Kanisa na katika muktadha wa kijamii na mahusiano ya kifamilia katika ujenzi wa udugu wa kibinadamu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 11 Septemba 2024 amehitimisha hija yake Kitume nchini Timor ya Mashariki na kuanza hija yake nchini Singapore, nchi ambayo iko Kusini Mashariki mwa Bara la Asia; inayonogeshwa na kauli mbiu “Umoja na Matumaini”, kielelezo cha umoja, ushirika, maelewano na mafungamano ya kijamii kati ya waamini na ndani ya Kanisa na katika muktadha wa kijamii na mahusiano ya kifamilia. Hija hii ya kitume inadokeza mwanga wa matumaini kwa Wakristo nchini Singapore hasa wale wanaobaguliwa, kuteswa na kudhalilishwa utu, heshima na haki zao msingi. Baba Mtakatifu Francisko akiwa njiani kutoka Timor ya Mashariki, amemtumia Rais José Ramos-Horta wa Timor ya Mashariki, ujumbe wa shukrani na matashi mema kwa wema, upendo na ukarimu waliomwonesha wakati wa hija yake ya kitume nchini Timor ya Mashariki. Anamwomba Rais amfikishie salam na matashi mema kwa viongozi na watu wateule wa Mungu nchini Timor ya Mashariki. Anawatakia na kuwaombea amani na mshikamano na hatimaye, anawapatia baraka zake za kitume!

Papa Francisko tarehe 11 Septemba 2024 amewasili nchini Singapore
Papa Francisko tarehe 11 Septemba 2024 amewasili nchini Singapore

Baba Mtakatifu Francisko kabla ya kuondoka nchini Timor ya Mashariki, amepata nafasi ya kukutana na kuzungumza na Wayesuit 41 wanaoishi na kufanya utume wao nchini Timor ya Mashariki. Amepata bahati ya kukutana na kuzungumza na Padre João Felgueiras, mwenye umri wa miaka 103 ambaye ni kati ya Wayesuit wenye umri mkubwa kuliko wote duniani. Padre huyu katika umri wake, ameshikwa na mshangao mkubwa kukutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko. Hawa ni Wajesuit wanaotoka Vietnam, Malaysia na Ufilippini wanaoendelea kujisadaka katika sekta ya elimu na malezi kwa vijana wa kizazi kipya; pamoja na utume Parokiani.

Papa Francisko akizungumza na wajesuit nchini Timor ya Mashariki
Papa Francisko akizungumza na wajesuit nchini Timor ya Mashariki

Hiki kimekuwa ni kipindi cha maswali na majibu kwa kujikita katika misingi ya Haki Jamii, Mafundisho Jamii ya Kanisa na umuhimu wake katika maisha na utume wa Kanisa. Mama Kanisa anataka kujikita katika mchakato wa kutamadunisha Injili ili kuinjilisha tamaduni mintarafu tunu msingi za Kiinjili na utu wema. Itakumbukwa kwamba, hija hii imenogeshwa na kauli mbiu “Que a vossa fé seja a vossa cultura” yaani “Imani yako itokane na utamaduni wako.” Ni himizo linalopania kutia moyo kuishi imani mintarafu utamaduni na mila njema za watu wa Timor ya Mashariki. Watambue kwamba, wao ni vyombo na mashuhuda wa furaha ya Injili, watu ambao wanapaswa kuwa tayari kujisadaka kwa ajili ya uinjilishaji unaopania kuleta upyaisho katika maisha ya watu na kama njia ya kutamadunisha Injili ili kuinjilisha tamaduni mintarafu tunu msingi za Kiinjili.

Papa Nchini Singapore
11 September 2024, 14:38