Hija ya Kitume ya Papa Francisko Ubelgiji:Kanisa lina utajiri katika waamini dhaifu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amefungua kinywa pamoja na kundi la wanaume na wanawake kutoka Afrika na Ulaya Mashariki au kutoka Brussels kwenye parokia ya Mtakatifu Gilles, jengo takatifu lililojenga katikati ya karne ya 19 ambalo kila asubuhi, kwenye meza ya kituo kama meli katika mtindo wa Kiromania wa Gothic hutoa “kahawa ya asubuhi kila siku kwa makundi ya watu wasio na makazi, wakimbizi, watu maskini katikati ya jiji. Kwa njia hiyo Jumamosi tarehe 28 Septemba 2024 ikiwa ni sehemu ya tukio la Hija ya kitume ya Papa Francisko hata bila kupangwa amekula Croissants na kunywa kahawa kwenye meza pamoja na maskini na wakimbizi na pia kupewa bia ya ufundi. Walakini, hiyo i"napaswa kuonjwa alasiri," kama alivybainisha.
Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo akiwa nao alisikiliza kwanza baadhi ya shuhuda na kupokea zawadi ya bia ya ufundi iliyoundwa ili kufadhili kazi za hisani. Akitoa neno na salamu Baba Mtakatifu alianza kushukuru kwa mwaliko wa kufungua kinywa. "Ni vizuri kuanza siku na marafiki, na ndivyo hali ilivyo hukoMtakatifu Gilles. Ninamshukuru Marie-Françoise, Simon na Francis kwa kile walichosema na ninafurahi kuona jinsi upendo unavyoendelea kuchochea ushirika na ubunifu wa kila mtu hapa: hata umeunda La Biche de saint Gilles, na ninafikiri ni bia nzuri sana! Kisha alasiri nitawambia ikiwa ni nzuri au la.” Alisema Papa Francisko.
Papa ameongeza kusisitiza kuwa "Kama Marie-Françoise alivyosema, "huruma inaelekeza njia ya kutumaini," hii nzuri sana! na kutazamana kwa upendo husaidia kila mtu! yaani kutazama siku zijazo kwa ujasiri na kurudi njiani kila siku. Sadaka ni kama hiyo: ni moto unaotia moyo joto na hakuna mwanamke au mwanamume duniani asiyehitaji joto." Papa Francisko akiendelea alisema: “Ni kweli, kuna matatizo mengi sana ya kukumbana nayo mnajua hili vyema - kama Simon alivyotuambia, na wakati mwingine mnakutana na kukataliwa na kutokuelewana, kama Francis alivyotuambia, lakini furaha na nguvu zinazokuja kutoka katika upendo wa pamoja ni kubwa zaidi kuliko ugumu wowote, na kila wakati tunapojihusisha katika harakati ya mshikamano na kujaliana tunatambua kwamba tunapokea zaidi ya tunavyotoa.” (Rej Lk 6,38; Mdo 20,35).
Baba Mtakatifu alisisitiza kwamba mwishoni mwa mkutano wao kungekuwa na zawadi kwa Parokia ya sanamu ya Mtakatifu Laurenti, shemasi na shahidi wa karne za kwanza, ambaye pia alikuwa maarufu kwa kuwasilisha kwa washtaki wake, waliotaka apeleke hazina za Kanisa, naye akawakilisha washiriki dhaifu zaidi ya jumuiya ya Kikristo ambao ni mali yake, ya Roma, kwa hiyo jambo muhimu zaidi, lakini pia tete zaidi ya maskini, na wahitaji.” Papa ameongeza kusema: “Haikuwa namna ya usemi, wala hata uchochezi rahisi. Ilikuwa na ndiyo ukweli ulio safi: Kanisa lina utajiri wake mkubwa zaidi katika washiriki wake walio dhaifu zaidi, na ikiwa kweli tunataka kujua na kuonesha uzuri wake, utatusaidia sisi sote kujitoa wenyewe kwa kila mmoja namna hii, katika udogo wetu, katika umaskini wetu, bila kujifanya na kwa upendo mwingi." Papa amerudia kutoa asante kwa kumkaribisha miongoni mwao na asante kwa safari waliyosafiri pamoja. Na asante kwa kifungua kinywa! Aliwabariki wote na kuwaombea. Papaaliomba ikiwapendekeza, wamwombee pia na kuhitimisha.