Hija ya Kitume ya Papa Francisko Ubelgiji:Uinjilishaji,furaha&huruma!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko akikutana na Maaskofu, Mpadre, mashemasi, waliowekwa wakfu kike na kiume, waseminari na wahudumu wa kichungaji katika Basilika ya Moyo Mtakatifu, huko Koekelberg tarehe 28 Sptemba 2024, kwanza alisikiliza shuhuda kutoka kwa Mhudumu wa kichungaji, Padre anayehudumu katika Kikanisa cha Magereza, Padre mwingine mmoja, mwingine kutoka kituo cha makaribisho ya waathirika wa nyanyaso, ushuhuda wa Sr wa Shirika la Udugu wa Tiberiade na Mtaalimungu. Baba Mtakatifu alianza hotuba yake akibainisha alivyo na furaha kiwa katikati yao. Alimshukuru Askofu Mkuu Terlinden kwa maneno yake na kuwakumbusha kipaumbele cha kutangaza Injili. Katika njia panda ambayo ni Ubelgiji, wao ni Kanisa katika Upyaisho. Kiukweli kwa muda mrefu wamekuwa wakitafuta kubadilisha uwepo wa Parokia katika eneo, ili kutoa nguvu ya Kanisa katika mafunzo ya walei; hasa kwa kufanya kuwa Jumuiya karibu na watu, ambao wanasindikiza watu na kushuhudia kwa ishara za huduma. Kwa kuchochewa na maswali yao, Papa Francisko alipenda kupendekeza baadhi ya tafakari zinazozungukia maneno matatu: Unjilishaji, furaha na huruma.
Njia ya kwanza ya kupitia ni Unjilishaji. Mabadiliko ya nyakati zetu una mgogoro wa imani ambao tunafanya uzoefu Nchi za Magaharibi, umetusukuma kurudi katika msingi, yaani Injili, kwa sababu iweze kupyaishwa katika kutangaza Habari Njema ambayo ililetwa na Yesu Ulimwenguni, kwa kuifanya iangaze uzuri wake wote. Mgogoro, Baba Mtakatifu amesema kila mgogoro, ni wa nyakati ambao tumepewa ili kujikung’uta, “kujiuliza na ili kubadilika. Ni fursa mwafaka, katika lugha ya kibiblia inaitwa Kairos- fursa maalum,”kama iliyomtokea Ibrahimu, Musa na Manabii. Kwa hakika, tunapopitia ukiwa, lazima tujiulize ni ujumbe gani ambao Bwana anataka kutujulisha. Na mgogoro unatuonesha nini? Tumetoka katika Ukristo uliowekwa katika mfumo wa kijamii wa ukarimu hadi Ukristo wa "wachache", au tuseme, moja ya ushuhuda. Na hii inataka ujasiri wa uongofu wa kikanisa, ili kuanzisha mabadilko yale ya kichungaji, ambayo yanatazama hata ukawaida, mitindo, lugha za imani, kwa sababu ziwe kweli katika huduma ya Uinjilishaji (Evangelii gaudium, 27).
Papa ameongeza kuwa anataka kusema kwamba Helmut: hata mapadre wanaombwa ujasiri huo. Kuwa Padre haimanishi kutunza au kuendesha urithi wa wakati uliopita lakini kuwa mchungaji anayependa Kristo na Mchungaji makini katika kukubali maswali ya Injili ambayo mara nyingi ni magumu, wakati anatembea na Watu wa Watakatifu wa Mungu na kutembea kidogo mbele, kidogo katikati na kidogo nyuma kabisa. Iwapo tunabeba Injili, Papa amefikiria kile ambacho alisema Yanika kuwa: “Bwana anafungua mioyo yetu kukutana na yule aliyetofauti nasi. Ni vizuri na zaidi lazima kwamba vijana wawe na ndoto na tasaufi tofauti. Inapaswa kwa hakika kuwa hivyo, kwa sababu tunaweza kupitia katika michakato binafsi au kijumuiya ambayo inatufikisha, lakini ni katika hatima moja ya kukutana na Bwana: Katika Kanisa kuna nafasi kwa wote na hakuna ambaye ni nakala ya mwingine. Umoja katika Kanisa sio sare, bali ni kupata maelewano katika utofauti! Na pia namwambia Arnaud: mchakato wa sinodi lazima uwe ni kurudi katika Injili; ni lazima usiwe na baadhi ya mageuzi "ya mtindo" kati ya vipaumbele vyake, bali ijiulize: tunawe kufanys nini ili Injili ifikie jamii ambayo haisikilizi tena au imekwenda mbali na imani? Tujiulize sote."
Na njia ya Pili ni Furaha. Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa “hatuwezi kuzungumza hapa furaha zinazohusiana na jambo linalopita na wala kuendana na mitindo inayovamia na kujiburudisha katika kutumia hovyo. Inayozungumza ni furaha kubwa zaidi, ambayo inasindikiza na kusaidia maisha hata wakati wa giza na uchungu, na hiyo ni zawadi ambayo inakuja kutoka kwa aliye Juu kwa Mungu. Ni furaha ya Moyo itokayo katika Injili; ni kujua kwamba katika safari ndefu hatuko peke yetu na kwamba hata katika hali za umaskini, za dhambi, vipingamizi, Mungu yuko karibu, anatutunza na hawezi kuruhusu kifo kiwe neno la mwisho. Mapema kabla ya kuwa Papa, Joseph Ratzinger aliandika kwamba katika Kanuni ya kufanya mang’amuzi ni hii: “Mahali panapokosekana furaha, mahali ambapo matani yamekwisha, hapa hakuna hata Roho Mtakatifu(…) na kinyume chake: ni mahali ambapo furaha ni ishara ya neema (MUNGU YA YESU KRISTO, Brescia 1978, 129). Ni vizuri! “Kwa hiyo ninataka kuwambia: “Kuwa kuhubiri kwenu, kuadhimisha kwenu, huduma yenu na kufanya utume iache ioneshwe furaha ya moyo kwa sababu hiyo inatoka katika swali na kuvutia hata wale walio mbali. Furaha ya Moyo na siyo tabasamu la uongo, la wakati, badala yake furaha ya moyo. Papa amemshukuru Sr Agnes na kumwambia: furaha ni njia.” Ikiwa imani inajionesha kuwa ngumu, lazima kuonesha kama alivyosema yeye kwamba ni njia kuelekea furaha.” Na kwa hiyo kwa kutazama mahali njia inampeleka ndipo kuna utayari zaidi wa kuanza safari.
Neno la Tatu ni huruma: Baba Mtakatifu Francisko Injili , ikikaribishwa na kushirikishwa, kupokelewa na kutolewa , inapelekea katika furaha kwa sababu inatufanya kugundua kuwa Mungu ni Baba wa huruma ambaye anahisia kali kwetu, na anatunyanyua katika kuanguka kwetu na ambaye haondoi kamwe upendo wake kwa ajili yetu. Tukazie hayo katika moyo: kamwe Mungu hatoi upendo wake kwetu. “Lakini hata tunapofanya makosa makubwa? Mungu kamwe haondoi upendo wake kwetu. Hii mbele ya uzoefu wa ubaya wakati mwingine inaweza kufananishwa kuwa siyo haki, kwa sababu sisi kiurahisi tunatanguliza haki ya kidunia ambayo inasema: “anayekosea lazima apate adhabu.” Hata hivyo haki ya Mungu ni kuu: anayekosea anaalikwa kufanya malipizi ya makosa yake, lakini kwa kuponesha katika moyo anahitahiji upendo wa huruma ya Mungu. Na kwa huruma yake ambayo Mungu anatuhalalishia, yaani kutufanya wenye haki kwa sababu anatupatia moyo mpya na maisha mapya. Kwa hiyo…Papa amesema: “nashukuru kwa kazi kubwa ambayo mnafanya ili kubadilisha hasira na uchungu kwa msaada, ukaribu na huruma. Nyanyaso zilizofanywa mbaya za mateso na majeraha zinahatarisha hata safari ya imani.
Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa kuna haja ya huruma nyingi, ili tusibaki na moyo wa jiwe mbele ya mateso ya waathirika, ili kufanya kuhisi wao ukaribu wetu na kutoa msaada wote wa uwezekano, ili kujifunza kutoka kwao, kama alivyosema aliyetoa ushuhuda, ya kuwa Kanisa ambalo linakuwa mtumishi wa wote bila kukandamiza yeyote. Ndiyo, kwa sabababu mzizi wa mateso unatokana na matumizi ya madaraka, tunapotumia nafasi tulizo nazo ili kuwakandamiza wengine au kwa kuwatumia. Na huruma, Papa amefikiria huduma ya Pieter, ni neno, ufunguo kwa wafungwa. “(Papa amesema hii haipo kwenye maandishi lakini nikiinga magerea hujiuliza, swali kwa nini wao na siyo mimi." Yesu anajionesha kwetu kwamba Mungu hajiweki mbali na majeraha yetu na maovu. Yesu anajua kuwa wote tunaweza kukosea, lakini hakuna aliyekosewa. Daima hakuna anayepotea."
Ni sawa, basi, kufuata njia zote za haki ya kidunia na njia za kibinadamu, kisaikolojia na adhabu; lakini adhabu lazima ipelekee uponeshaji. Lazima kusaidia watu kuamka na wao kupata njia katika maisha na katika jamii. “ Tunaruhusa mara moja katika maisha ya wote kutazama mtu kutoka juu hadi chini, hasa unapoinama kumwinua mtu aliye chini. Hiyo tu.” Papa amekazia: “Tukumbuke: wote tunakosea, lakini hakuna aliyekosewa, hakuna aliye potea daima. Daima ni huruma. Papa Francisko amewashukuru. Na katika salamu amependa kukumbuka kazi ya Magritte, mchoraji wao mashuhuri, yenye kichwa: "Tendo la Imani." Kazi yake inawakilisha mlango uliofungwa kutoka ndani, ambao hata hivyo umevunjwa katikati na umefunguliwa angani. Ni taswira, ambayo inatualika kwenda mbele zaidi, kutazama mbele na juu, tusijifungie kamwe.
Papa wa Roma amesisitiza kwamba:"Hii ni taswira ninayowaachia, kama ishara ya Kanisa lisilofunga kamwe milango yake, tafadhali: lisifungwe kamwe milango yake, Kanisa ambalo linampatia kila mtu fursa ya kuingia kwenye yale yasiyo na kikomo, ambayo yanajua jinsi ya kutazama zaidi. Hili ndilo Kanisa linaloinjilisha, linaloishi furaha ya Injili, linalotenda huruma." Papa kwa kuhitimisha amewasihi watembee pamoja na Roho Mtakatifu, kwa pamoja wafanye huruma. Watembee wakiwa na Roho Mtakatifu na huruma ya kuwa Kanisa kwa namna hiyo. Bila Roho, hakuna Mkristo anayetokea. Bikira Maria, Mama yetu, anatufundisha jambo hilo. Awaongoze, awalinde. Amewabariki kila mtu kutoka ndani ya moyo wake na kuwaomba tafadhali wasisahau kumuombea.