2024.09.29 Ziara ya Papa : katika Misa kwenye Uwanja wa Mfalme Baudouin. 2024.09.29 Ziara ya Papa : katika Misa kwenye Uwanja wa Mfalme Baudouin.  (Vatican Media)

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Ubelgiji:sitisheni vita,watu wamejeruhiwa

Papa mara baada ya Misa aliendelea na sala ya Malaika wa Bwana huko Bruxelles na ameto wito wa usitishaji mapigano mara moja huko Lebanon,Gaza,Palestina,Israel na maeneo mengine kama Ukraine,Sudan na Myanmar.Hali ya uhamaji ni fursa ya kukua kwa udugu,alisema katika Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi.Na alitoa tangazo la ufunguzi wa mchakato wa kumtangaza Mfalme Baudouin kuwa mwenyeheri.

Na Angella Rwezaula  - Vatican.

Baada ya misa Takatifu iliyoongozwa na Papa Francisko katika Uwanja wa Mfalme Baudouin huko Bruxelles, Dominika tarehe 29 Septemba 2024, Baba Mtakatifu ametoa shukrani kwa Askofu Mkuu kwa maneno yake mazuri. “Ninatoa shukrani za dhati kwa Wakuu, Mfalme na Malkia, na vile vile Wakuu wa Kifalme, Mtawala Mkuu na Malkia wa Luxembourg, kwa uwepo wao na ukarimu wao katika siku hizi. Vile vile, ninatoa shukrani zangu kwa wote ambao, kwa njia nyingi, mmefanya kazi pamoja kuandaa Ziara hii. Kwa namna ya pekee, ninawashukuru wazee na wagonjwa ambao wamesali sala zao.

Shukrani za Papa
Shukrani za Papa

Leo tunaadhimisha Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani yenye mada "Mungu anatembea na watu wake". Kutoka nchi hii, ya Ubelgiji, ambayo imekuwa na bado ni kivutio cha wahamiaji wengi, ninarudia wito wangu kwa Ulaya na Jumuiya ya kimataifa kuzingatia hali ya uhamiaji kama fursa ya kukua pamoja katika udugu, na ninakaribisha kila mtu kuona katika kila jambo kaka na dada mhamiaji uso wa Yesu ambaye alifanyika mgeni na msafiri kati yetu.

Wasiwasi wa mgogoro wa kivita huko Lebanon

Ninaendelea kufuatilia kwa uchungu na wasiwasi mkubwa upanuzi na kuimarika kwa mzozo nchini Lebanon. Lebanon ni ujumbe, lakini kwa sasa ni ujumbe wa kuteswa na vita hivi vina madhara makubwa kwa idadi ya watu: watu wengi sana wanaendelea kufa siku baada ya siku katika Mashariki ya Kati. Tunawaombea wahanga, familia zao, tunawaombe amani. Ninatoa wito kwa pande zote kukomesha moto mara moja huko Lebanon, huko Gaza, katika maeneo mengine ya Palestina, huko Israeli. Mateka waachiliwe na misaada ya kibinadamu iruhusiwe. Tusisahau Ukraine inayoteswa.

Misa  Ubelgiji
Misa Ubelgiji

Pia ninawashukuru wengi wenu mliokuja kutoka Uholanzi, Ujerumani, Ufaransa kushiriki siku hii: asanteni. Kwa wakati huu pia ningependa kukupatia habari fulani. Nikirudi Roma nitaanza mchakato wa kutangazwa mwenyeheri kwa Mfalme Baudouin: mfano wake kama mtu wa imani uwaangazie watawala. Ninaomba Maaskofu wa Ubelgiji wajitolee katika kuendeleza jambo hili.

Bikira Maria Kikao cha hekima
Bikira Maria Kikao cha hekima

Papa ameomba kumgeukia Bikira Maria wakati wa kusali Sala ya Malaika wa Bwana pamoja. "Haya yalikuwa maombi maarufu sana katika vizazi vilivyopita. Na inapaswa kuhuishwa, kwa kuwa ni muunganisho wa fumbo la Kikristo, na Kanisa inatufundisha kulijumuisha katika shughuli zetu za kila siku." Papa amewaomba.

Misa na sala ya Malaika wa Bwana

Hata hivyo amewapongeza vijana na kuwakabidhi wote kwa Mama yetu Mbarikiwa, ambaye ameoneshwa hapo, kando ya madhabahu, kama Kika cha Hekima. “Hakika, jinsi tunavyohitaji hekima ya Injili! Hebu tumwombe Roho Mtakatifu mara nyingi.” “Kwa maombezi ya Maria, tumwombe Mungu zawadi ya amani, kwa ajili ya Ukraine iliyokumbwa na vita; kwa Palestina na Israeli; kwa Sudan; kwa Myanmar na nchi zote zilizokumbwa na vita. Asanteni wote! Wacha en route, avec Espérance”!"yaani “tuendelee na safari kwa matumani” kama ilivyokuwa kauli mbiu ya ziara yake."

Bikira Maria kikao cha Hekima
Bikira Maria kikao cha Hekima

Askofu Mkuu wa Bruxelles

Baada ya misa hata hivyo Askofu Mkuu Luc Terlinden, wa Jimbo Kuu la Malines -Bruxelles ametoa maneno ya shukrani kubwa na furaha kwa niaba ya maskofu wenzake, waamini wa Kanisa  la Ubelgiji kwa ziara yake katika nchi hiyo. Yeye amefika kama Mchungaji ndugu na rafiki. "Shukrani kwa kutfikia na kuwasha tena cheche  za tumaini ambazo zinatoka kwa Yesu na kuruhusu kuwa daima uwepo katika Kanisa". Jumuiya zao na wachungaji wao hasa vijana wamefika idadi kubwa katika Uwanja wa Mfalme Baldovino na wana moyo wa kutangaza kwa furaha Injili, kama Yeye alivyowatia moyo kufanya hivyo. Wanataka kufuata hivyo nyayo za Mwenyeheri Mpya Anna wa Yesu ambaye aliunganisha tafakari ya kina katika matendo na kuchangia kujenga Ulaya bila mipaka.

Masalia ya Mkarmeli aliyetangazwa kuwa Mwenyeheri
Masalia ya Mkarmeli aliyetangazwa kuwa Mwenyeheri

Amemshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa kwenda kukutana na wazalendo na wahusika na kwa namna ya pekee wale walioko kwenye matatizo, au majeraha ya kina ya nyanyaso. Kwa kuingia katika mazungumza na wanafunzi, watafiti na wanafunzi katika fursa ya miaka 600 ya Chuo Kikuu dada cha KULeuven na UCLouvain, na kwamba Papa  anawafundisha "wasitengenishe utafutaji wa ukweli, hekima na haki kijamii." Hekima inaweza kusaidia hadhi ya mtu binadamu, na kwa namna ya pekee katika Siku ya 110 ya Dunia ambayo imewekwa kwa ajili ya Wahamiaji na wakimbizi. Na inasaidia hata kulinda sayari yetu, “nyumba yetu ya pamoja.” Amesisitiza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Bruxelles.

Uwanja ulifurika kweli waamini wa Ubelgiji
Uwanja ulifurika kweli waamini wa Ubelgiji

Kwa kuhitimisha, alimwambia Papa kwamba "Ujio wako kidugu utabaki umesimkwa kwa kina katika mioyo yetu , utaongeza kwa nguvu sana urafikia ambao unatuunganisha. Tunaamini katika salamu zako za wema. “Uwe na uhakika mpendwa Papa Francisko, katika sala zetu kwa ajili yako na kwa Huduma yako ambayo tunaikabidhi kwa Mama, Kikao cha Hekima na Mwenyeheri Anna wa Yesu."

Papa baada ya Angelusi 29 Sept
29 September 2024, 13:10