Hija ya Kitume ya Papa Francisko Ubelgiji:Uovu lazima ufunuliwe wazi!

Katika Maadhimisho ya Misa huko Bruxelles nchini Ublegiji ikiwa ndiyo hitimisho la Ziara yake ya 46 ya Kitume Papa baada ya kutafakari kuhusu ufunguzi,ushirika na ushuhuda,amerudia kulaani vikali juu nyanyaso na kwamba “hakuna mahali pa unyanyasaji katika Kanisa,uovu lazima uonekane wazi” na kuwaomba maaskofu wasiwafunike!“Wanyanyasaji lazima wahukumiwe.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ikiwa ni siku yake ya Mwisho wa Ziara ya 46 ya Kitume katika Nchi za Luxemborurg na Ubalgiji, Dominika tarehe 29 Septemba 2024, ameongza Ibada ya Misa  Takatifu katika Uwanja wa Taifa wa Mflame Baudouin huko Bruxelles nchini Ubalgiji. Katika Ibada ya Misa Takatifu kulikuwa pia na kutangazwa kwa Mwenyeheri mpya Anna wa Yesu -Anna de Lobera, wa Shirika la Wakarmeli. Kwa kuongozwa hivyo na Injili iyosomwa, Baba Mtakatifu alisema: “Na yeyote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini,”(Mk 9,42.) Katika maneno haya yaliyoelekezwa kwa mitume, Yesu anaonesha hatari ya kashfa  yaani kuweka vizingiti vya safari ya “wadogo.” Ni onyo la nguvu, kali, ambapo tunapaswa kusimama na kutafakari. Papa Francisko amependa kutafakri nao hata kwa nuru ya maandishi matakatifu mengine  kwa njia ya maneno matatu msingi: ufunguzi, ushirika na ushuhuda.

Misa nchini Ubelgiji 29 Septemba 2024
Misa nchini Ubelgiji 29 Septemba 2024

Papa akianza na neno ufunguzi, alisema:“Katika somo la kwanza, linazungumza na Injili inatuonesha tendo huru la Roho Mtakatifu ambaye katika simulizi ya kitabu cha Kutoka, anajaza zawadi yake ya unabii, sio tu kwa wazee waliokwenda na Mungu katika hema, bali hata watu wawili walikuwa wamebaki katika kambi. Hii inatufanya tufikirie kwa nini iwapo mwanzo kulikuwa na kashfa ya kutokuwapo kwao katika kundi la waliochaguliwa, baada ya zawadi ya Roho ni kashfa kuzuia wao wasiweze kutenda utume ambao licha ya hayo yote walipokea.” Papa aliongeza kusema kuwa “Alitambua vizuri Musa, mtu mnyenyekevu na mwenye hekima, ambaye kwa akili na moyo ulio wazi alisema: “ingekuwa heri kama watu wote wa Bwana wangekuwa manabii na kama Bwana angewatia roho yake”(Hes 11,29). Ni matashi mema! Papa alisema.

Haya ni maneno ya hekima ambayo yanatanguliza kile ambacho Yesu alisisitiza akithibitisha katika Injili(Mk 9,38-43.45.47-48). Haya yalitokea huko Cafarnaum na mitume walitaka kwa mara nyingine tena kumzuia mtu kutoa mapepo kwa jina la Mwalimu, kwa sababu walisema: “alikuwa hatufuati, ina maana ya kusema: “hakuwa katika kundi letu”(Mk9,38). Wao walikuwa wanafikiria hivi: “Hasiyetufuata, hasiyekuwa katika kundi letu hawezi kufanya miujiza, hana haki.” Lakini Yesu aliwashangaza, kama afanyavyo daima aliwakaripia, na akiwaalika waende zaidi ya mipango yao  na “wasikashfu” uhuru wa Mungu , na aliwambia wao: “ Msiwakataze (…) kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu.”(Mk 9, 39-40). Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu aliomba kuchunguza vizuri maneno mawili, lile la Musa na lile la Yesu, kwa sababu yanatazama hata sisi, na maisha yetu ya kikristo. Wote kiukweli  kwa Ubatizo, tulipokea utume katika Kanisa. Lakini hii ni zawadi na siyo jina la kujivuna.

Misa ya mwisho ya Papa akiwa ziara ya Kitume nchini Ubelgiji
Misa ya mwisho ya Papa akiwa ziara ya Kitume nchini Ubelgiji

Jumuiya ya waamini siyo mzunguko wa waliobahatika, ni familia ya waliokombolewa, na sisi hatukutumwa kupeleka Injili katika ulimwengu kwa sifa zetu, bali kwa neema ya Mungu , kwa ajili ya huruma yake na kwa ajili ya imani ambayo mbali na vizingiti vyetu na dhambi, Yeye anaendelea kutupatia sisi kwa upendo wa Baba, kwa kutazama ndani mwetu kile ambacho sisi tunajaribu kutambua. Kwa njia hiyo anatuita, anatutuma na kutusindikiza kwa uvumilivu siku baada ya siku. Na kwa hiyo ikiwa tunataka kushirikiana kwa upendo ulio wazi na upole wa tendo huru la Roho, bila kuwa na kashfa,  vizingiti kwa wengine  kwa majivuno yetu na ugumu, tunahitaji kujikita katika utume wetu kwa unyenyekevu, shukrani na furaha. Hatupaswi kuchukia, zaidi ya kufurahia kwa sababu, kwanza hata wengine wanaweza kufanya kile ambacho tunafanya sisi, ili Ufalme wa Mungu ukue na tujikute wote tunakutana siku moja katika mikono ya Baba.

Waamini katika Misa Takatifu
Waamini katika Misa Takatifu

Baba Mtakatifu amesema kuwa “ Na hii inatupeleka katika neno la pili la Ushirika. Katika hilo linazungumzwa na Mtakatifu Yakobo katika Somo la Pili(Yk 5,1-6) kwa kutumia picha mbili za nguvu: utajiri unaoharibika(Yk 5,3) na vilio vya waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana(Yk 5,4). Hii inatukumbusha kwamba njia moja pekee ya maisha ni ile ya zawadi, ya upendo ambayo inaunganisha katika kushirikishana. Njia ya ubinafsi inazalisha kujifungia tu, kuweka kuta na vizingiti na “kashfa” kwa hiyo inatufunga katika mambo na kutupeleka mbali na Mungu na ndugu. Ubinafsi kama na yale yote yanayotuzuia upendo ni “kashfa” kwa sababu, unakandamiza wadogo,  hunyenyekeza hadi ya watu na kusonga kilio cha masikini (Zab 9,13). Na hii ilikuwa kweli wakati wa Mtakatifu Paulo kama ilivyo kwetu leo hii. Hebu tufikirie, kwa mfano, kile kinachotokea wakati maisha ya watu binafsi na jumuiya yanaegemezwa tu kwenye kanuni za maslahi na mantiki ya soko.(Evangelii gaudium, 54-58).

Papa Francisko
Papa Francisko

Papa Francisko akemea nyanyaso.

 Hebu tufikirie nini kinatokea watoto wanapofanyiwa kashfa, kupigwa, kunyanyaswa na wale wanaopaswa kuwatunza, kuhusu majeraha ya uchungu na unyonge kwanza kabisa kwa waathirika, lakini pia katika familia zao na katika jamii. Kwa akili na moyo wangu ninarudi kwenye historia za baadhi ya hawa wadogo niliowakuta nao jana yake. Niliwasikia, nilihisi mateso yao kama walionyanyaswa na ninarudia hapa: Kanisani kuna nafasi kwa kila mtu, kila mtu, kila mtu lakini sisi sote tutahukumiwa na hakuna nafasi ya unyanyasaji, hakuna nafasi ya kufunika unyanyasaji. Ninaomba wote: msifiche unyanyasaji! Ninawaomba maaskofu: msifiche unyanyasaji! Walaani wanyanyasaji na muwasaidie kupona kutokana na ugonjwa huu wa unyanyasaji. Uovu hauwezi kufichwa: uovu lazima ufunuliwe wazi, ili ujulikane, kama watu wengine walionyanyaswa wamefanya, na kwa ujasiri. Ifahamike. Na mnyanyasaji ahukumiwe. Mnyanyasaji na ahukumiwe, ikiwa ni mlei, kasisi au askofu: na ahukumiwe.”

Ni kuunda ulimwengu ambao kuna nafasi kwa mwenye matatizo, kuna huruma kwa anayekosea, kuna huruma kwa anayeteseka na hawezi, kuonekana kana kwamba walikuwa noti mbaya katika tamasha kamili la ulimwengu wa ustawi, wala hawawezi kuzuiwa na aina fulani ya ustawi wa kuonekana. Kinyume chake, ni sauti ya Roho ambayo inatukumbusha sisi ni nani, wote ni maskini wadhambi, na watu waliodhulumiwa ni maombolezo yanayoinuka hadi mbinguni, yanayogusa nafsi ambayo hututia aibu na kutualika kuongoka. Tusitie vizingizi katika sauti za kinabii, na kuzizima kwa kutojali kwetu. Tusikilize kile ambacho Yesu anasema katika Injili: nenda mbali jicho la kukashfu, ambalo linaona maskini na kugeuzia kisogo! Mbali na sisi mkono wa kashfu ambao unakunja ngumu ili kuficha hazina zake na kuziingiza  kwa pupa kwenye mifuko!

Waamini vijana
Waamini vijana

Papa ametoa mfano binafsi kuwa: “Bibi yangu alikuwa anasema: “shetani uingia kwenye mifuko.” Mkono ule ambao unashangaza kwa kutenda nyanyaso za kijinsia , nyanyaso  za matumizi mabaya ya madaraka, unyanyasaji wa dhamiri dhidi ya wale ambao ni dhaifu zaidi: na ni kesi ngapi za unyanyasaji tunazo katika historia yetu, katika jamii yetu.” Papa ameendelea “Nenda mbali na sisi, kashfa ya mguu ambao unakimbia haraka ili usiwe karibu na anayeteseka na kupitia mbali ! Yote hayo yaondoke , kwenda mbali nasi! Hakuna kizuri na chenye msimamo wa kujenga hivyo! Papa ameendelea kutoa mfano ambao anautumia mara kadhaa, kwamba mara kadhaa anauliza mtu ikiwa anatoa sadaka, na mwingine huji Ndiyo Baba”...  Papa huliza tena "niambei unapokuwa unafanya hivyo je unagusa mtu huyo maskini mikononi mwake au unatupa ela hivyo ukitazama mahali pengine? Je unatazama machoni pa yule unayemtolea sadaka?” Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu ameomba wafikirie hilo.

Ikiwa tunataka kujenga wakati ujao hata kwa ngazi ya kijamii na kiuchumi, itakuwa vizuri kurudi kuweka katika msingi wa changuzi zetu  za Injili ya huruma.  Yesu ni huruma; wote tulihurumiwa: Vinginevyo, haijalishi ikiwa ni ya kuvutia sana, makaburi ya utajiri wetu daima  na ambayo yatakuwa makubwa na miguu ya udongo (rej.Dan 2,31-45). Tusijidanganye: bila upendo hakuna kinachodumu, yote yanaisha, yanaanguka chini na kutuacha wafungwa wa maisha ya kukimbia, matupu na bila maana, katika ulimwengu unaoyumba ambao mbali na  kuonekana umepoteza uaminifu, kwa sababu umekashfu wadogo.

Papa alibariki watoto wengi
Papa alibariki watoto wengi

Na hivyo tunafikia neno la tatu, ushuhuda. Katika hilo Papa ametumia mfano wa maisha na kazi ya Anna wa Yesu -Anna de Lobera katika siku yake ya kutangazwa mwenyeheri. Mwanamke huyo alikuwa mstari wambele katika Kanisa la wakati wake, katika harakati moja ya mageuzi, katika nyayo za roho kubwa sana ya Teresa wa Avila, ambaye alieneza mawazo makuu ya Hispania, Ufaransa na hata Bruxelles, kwa nchi zile ambazo ziliitwa wakati ule za Kihispania. Katika wakati ambao ulikuwa na kashfa za uchungu, ndani na nje ya Jumuia ya kikristo, yeye na wenzake kwa maisha yao rahisi na maskini yaliyojikita nao  kwa kazi na upendo walijua kupeleka imani kwa watu wengi, kiasi kwamba kuna aliyemfafanua kama mwanzilishi wa mji huo kama “sumaku ya kiroho.”

Wakati wa kuwakilisha Mwenyeheri mpya
Wakati wa kuwakilisha Mwenyeheri mpya

Kwa uchaguzi hakuacha maandishi. Alijikta kinyume chake kuweka kwenye matendo ambayo alikuwa amejifunza(1 Kor 15,3) na kwa mtindo wake wa kuishi alichangia katika Kanisa la wakati wa matatizo makubwa. Kwa njia hiyo Papa ameomba: “Basi na tuukaribishe kwa shukrani kielelezo cha “utakatifu wa kike” ambao ametuachia (Gaudete et exsultate, 12), maridadi na wenye nguvu, uliotengenezwa kwa uwazi, ushirika na ushuhuda. Hebu na tuombe kwa maombezi yake, tuige fadhila zake na tufanye upya ahadi yetu ya kutembea pamoja katika nyayo za Bwana.”

Mhubiri ya Papa 29 Septemba 2024
29 September 2024, 13:00