Kuweni wapole,wajasiri:kitabu cha mazungumzo na Papa na wajesuit
Vatican News
“Kuweni wapole, jipeni moyo” ndicho kichwa cha kitabu, kilichochapishwa na Garzanti na Nyumba ya Duka la Vitabu Vatican (LEV) na kipo katika maduka ya vitabu tangu tarehe 17 Septemba 2024, ambapo Padre Antonio Spadaro, katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, anakusanya mazungumzo 18 ya Baba Mtakatifu Francisko na Wajesuti waliokutana wakati wa ziara zake za kitume.
Hisia ya utume
Kichwa hicho kinakumbusha maneno ambayo Papa Francisko mwenyewe alizungumza Februari 2022 kwa kikundi cha ndugu aliokutana nao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akituma ujumbe wa upendo ambao pia ni tamko la kujitolea. Aidha, kwa usahihi katika mazungumzo ya faragha na Wanashirika la Yesu wakati wa ziara zake za kitume duniani kote, Baba Mtakatifu mara nyingi aliweza kueleza maana ya ndani kabisa ya utume wake.
Maadili ya Upapa
Padre Spadaro, akisafiri naye, alishuhudia nyakati hizi za kushirikiana na kufahamiana na kukusanya katika kitabu cha mazungumzo kumi na nane ambayo yamefanyika hadi sasa. Wanawasiliana na kufufua maadili ya mwanzilishi wao kauzana na neema hadi faraja, kutoka katika uhuru hadi tumaini, hadi utayari wa kujifungua bila woga hadi kufanywa upya katika imani na vile vile katika sheria na maadili - na zaidi ya yote kuonesha kwa wengine ukaribu na huruma ambayo ni alama ya mtindo wa Mungu.
Uwasilishaji kitabu Septemba 22
Dominika tarehe 22 Septemba 2024, saa 9.00 Alasiri, Padre Antonio Spadaro atawasilisha kitabu huko Pordenonelegge, katika Ukumbi wa Taasisi ya Vendramini, katika mazungumzo na Massimo Recalcati.