Maisha yangu nikiwa mmisionari huko Papua New Guinea
Andrea Tornielli
“Duc in altum,” yaani “Tweka mpaka kilindini,” ndiyo maneno haya ya Yesu yaliyochaguliwa kuwa kauli mbiu ya kiaskofu ya Askofu Mkuu Francesco Panfilo, Askofu Msalesiani, ambaye alihudumu kama mmisionari huko Ufilippino kwa miaka 32, kabla ya kufika Papua New Guinea, ambapo alikuwa wa kwanza huko Alotau na kisha akaongoza Jimbo Kuu la Rabaul, pia akawa rais wa Baraza la Maaskofu wa nchi hiyo. Kwa maneno yake alisema kwamba “Utume, ni suala la moyo, shauku kwa Kristo na shauku kwa watu wake.
Ufuatano ni hushuhsda wa Askofu Mkuu mkuu Francesco Panfilo, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo la Rabaul akihojiwa na Vyombo vya Vatican kuhusu utume wake ambapo anaanza kuelezea kuwa: “Mtu fulani aliniuliza uzoefu wangu ulivyokuwa, kwa sababu hivi karibuni nilisherehekea jubilei ya kuwekwa wakfu kwangu miaka 50 iliyopita. Nilikaa Ufilipino kwa miaka 32, kisha nikaja Papua New Guinea kama mjumbe wa ukaguzi wa Wasalesiani kwa miaka minne, kisha Papa Yohane Paulo II akaniteua kuwa askofu wa Alotau, kisha nikahamishiwa huko Rabaul: na nilipokumbuka miaka hii ya utume niliguswa kidogo, kwa sababu siku zote nilijisikia kama mmisionari, hata katika Ufilipino, ambapo hata hivyo nilikuwa shuleni, nikiwa mkufunzi."
Askofu akiendelea alisisitiza kuwa:"Nilipokuja Papua New Guinea niliweza kuwa mmisionari jinsi nilivyokuwa nikitamani siku zote nikiwa kijana. Yalikuwa maisha magumu. Nilipokuwa Alotau - vyote vilikuwa visiwa, bahari yote na ilinibidi kusafiri kwa mitumbwi, tulikula popote tulipoweza... Huko Rabaul ilinibidi nitembee sana, ilinibidi niende milimani... Naam, nilijihisi kama mmisionari na mchungaji. Papa Francisko baada ya kuchaguliwa kuwa Papa 2013, mwishoni mwa mwaka huo aliandika Waraka wa Kitume wa Evangelii gaudium na katika kifungu 268 alisema kwamba: “utume wakati huo huo ni shauku kwa Kristo na shauku kwa watu wake.” Na tazama, maneno haya yalinigusa)mimi. Kama Askofu nilichagua kama kauli mbiu yangu “Duc in altum” yenye maana: “Tweka hadi Kilindini” ambayo ni maneno ya Yesu aliyomweleza Petro... Nimeishi (haya), ninahisi kwamba nimeishi maisha yangu kama mmisionari. Papa alisema alichosema hapo: utume wakati huo huo ni shauku kwa Kristo na shauku kwa watu wake, kama hakuna upendo huu, hakuna(utume)… Utume ni upendo, ni kujitoa kwa ajili ya watu na kwa ajili ya watu wa Bwana. Ikiwa tunampenda Bwana, hii inatusaidia kuwasaidia watu na ikiwa tunawapenda watu hii inaturudisha kwa Yesu."