Mama yake Kard.Parolin afariki dunia,Papa ametuma rambirambi
Vatican News
Tarehe 31 Agosti 2024, “amelala usingizi wa utulivu katika Bwana” Bi Ada Miotti Parolin, Mama yake Kardinali Petro Parolin, Katibu wa Vatican. Alikuwa na miaka 96. Katika taarifa iliyotolewa: “kwa huzuni, lakini katika imani kwa Yesu Kristo Msulibiwa na mfufuka, watoto: Padre Pietro, Mariarosa na Giovanni, wake zao, watoto, vitukuu na ndugu wote ambao wameorodheshwa katika tangazo wanaandika: “Mimi ni Ufufuko na Maisha. Maisha hayaondolewi, bali yamebadilishwa.”
Baba Mtakatifu Francisko ameguswa na msiba huo na ametuma salamu za rambi rambi na ukaribu wa sala.
Mazishi yatafanyika tarehe 3 Septemba 2024, saa 3.30 asubuhi katika Kanisa la Parokia ya Schiavon, katika Wilaya na Jimbo la Vicenza nchini Italia. "Mara baada ya ibada ya mazishi, mpendwa Ada atalazwa katika makaburi ya Schiavon.” Tarehe 2 Septemba saa 1.30 jioni kutakuwa na mkesha wa sala, katika Kanisa hilo hilo la Schiavon. Familia inashukuru kwa wale wote ambao wamekuwa “wakarimu kwa ukaribu wa Mpendwa Ada” na wale wote watakaoshiriki mazishi ambapo wanaomba “pasiwepo maua bali matendo ya wema.”